Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,286
Wajomba na mashangazi,wazee mabarobaro,
Pana fungu la ghawazi, latumiwa na kigaro,
Hununua waziwazi, wanati kama nduaro.
Yale yake maongezi, yamejaa chinjarero,
Kanaswa na hajiwezi, kama nswi kwenye vyero,
Ni wa hovyo utetezi, amefanywa nini sero?
Jamani ndarama hizi, zilizo fungasha ziro,
Zimewatia uchizi, Mwikabe na Mtatiro,
Wameushiriki wizi, Buyungu na Simanjiro.
Huyafungua maozi, aone yenye kasoro,
Ni sifa ya kiongozi, kutatua migogoro,
Hakimbii kama bozi, kutafuta kichochoro.
Kiongozi mfumbuzi, katu haleti uchuro,
Hutafuta utatuzi, wala hatafuti guro,
Ila wapo wapuuzi, hununuliwa kwa yuro.
MISAMIATI
Ghawazi...........fedha
Kigaro...............kikundi
Nduaro...........samaki
Nimekishufu.....nimekitazama
Chinjarero......hofu
Nswi.............samaki
Ndarama.......pesa
Maozi............macho
Bozi...............mpumbavu
Katwa...........katu
Vyero.............mtego wa kunasa samaki
Guro.............uhamaji wa sehemu nyingine
Yuro.............fedha ya umoja wa Ulaya.
18 Agosti 2018 Alhamis 18:31
Jina la Mtunzi Dotto Rangimoto
Jina La Utunzi Jini Kinyonga
Simu +255762845394 Morogoro.
Sent using Jamii Forums mobile app