Shairi: Mtatiro..

Shairi: Mtatiro..

Mkuu Dotto
1. Mtamlaumu bure, kuhama halali yake,
Kujiunga ni kwa bure, kuhama ni haki yake,
Ukizoea vya bure, tavunja heshima yake,
Mtatiro amehama, sababu ya matatizo,

2. Sababu ya matatizo, Mtatiro amehama,
Upinzani ni tatizo, na wengine watahama,
Wapinzani matatizo, wote watakuja hama,
Mtatiro amehama, sababu ya matatizo.

3. Nchi yetu ni tatizo, watu wetu matatizo,
Viongozi ni tatizo, wananchi matatizo,
Vyama vyetu ni tatizo, serikali matatizo,
Mtatiro amehama, sababu ya matatizo.

4. CUF ina matatizo, CCM ni tatizo,
Amehama matatizo, amehamia tatizo,
Chama chenye matatizo, ameongeza tatizo,
Mtatiro amehama, sababu ya matatizo.

5. Chadema ni matatizo, viongozi ni tatizo,
Sera zake matatizo, na misingi ni tatizo,
Wakimbia matatizo, waenda kwenye tatizo,
Mtatiro amehama, sababu ya matatizo.

P.

Salute Mkuu
 
Back
Top Bottom