Shairi: Mpishi asiye na bahati

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,136
4,292
MPISHI ASO BAHATI.

Babu nakusalimia,nadhani umeitika
Swali limenifikia,lazima litajibika
Wengi wamelikimbia,na mimi sitoliruka
Sababu ulinambia,kwa hilo sitosifika
Mwiko nimefikiria,kwanini ulivunjika
Tatizo bahati mbaya,mpishi huna bahati.



Hakujua kuchagua,kipi unaweza pika
Kuni alizibagua,chungu akakiinjika
Moshi darini kutua,ukaanza miminika
Na mpishi hukujua,mwiko ungeharibika
Chungu ungekiepua,mambo yangesawazika
Tatizo bahati mbaya,mpishi huna bahati.



Jikoni ulisogea,huku unalalamika
Kuni zikiteketea,kwako lilisaulika
Ukasaka mtetea,ni yupi wa kuchinjika
Ulipokuja otea,jogoo wanung’unika
Mayai yashapotea,viza likuhitajika
Tatizo bahati mbaya,mpishi huna bahati.





Mwiko kujichagulia,wakati ulishavuka
Jikoni kukimbilia,majivu ukayavuka
Kuja kujishitukia,moto umekanyagika
Unyayoni waingia,kabla haujazimika
Maji ungejimwagia,chungu yasinge sikika
Tatizo bahati mbaya,mpishi huna bahati.



Chini kujiangukia,ndo mwiko ukapasuka
Vipi uliuachia,ukaogonga ukuta
Lakini nilisikia,hakuna kufurukuta
Mambo ya kujiachia,mezani hutoyakuta
Mwiko ukafikiria,kweli nimekurupuka
Mpishi huna bahati,hukujua cha kupika.



SHAIRI-MPISHI ASO BAHATI
MTUNZI-Idd Ninga,Tengeru,Arusha
iddyallyninga@gmail.com
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom