IsangulaKG
JF-Expert Member
- Oct 14, 2010
- 706
- 386
MAHARAGWE UNILISHE, NKIJAMBA NI MKAIDI?
Chonde Baba sinitishe, Ukimya si yangu Jadi
Ili ujisahihishe, Kukosoa inabidi
Kiakili nijishushe, kisa yako itikadi?
MAHARAGWE UNILISHE, NKIJAMBA NI MKAIDI?
Umenilisha Mandondo, Tumbo kujamba sharti
Njoo unipige Nondo,Kujamba siachi ati
Kamwe sitoenda kando, Nitajamba katikati
MAHARAGWE UNILISHE, NKIJAMBA NI MKAIDI?
Wapika aina aina, Mlaji kunipumbaza
Watiya Udi na Hina, Lengo lako kunilaza
Chumvi izidipo sana, Sauti nache kupaza
MAHARAGWE UNILISHE, NKIJAMBA NI MKAIDI?
Jikoni penye 'Mawingu', umpike Josefati
Kweli uwone majungu, piga kazi Hoti 'poti'
Nkinena watupa Rungu, niridhike na 'Makuti'
MAHARAGWE UNILISHE, NKIJAMBA NI MKAIDI?
Weye uote Kitambi, Miye Nyumba Kichuguu
Wacha nijambe mjambi, Tumbo lipate nafuu
Watatoa rambirambi, Wanangu na Wajukuu
MAHARAGWE UNILISHE, NKIJAMBA NI MKAIDI?
malenga wa Ngumbalu, 2017
Link:Kisima Cha Mashairi
Chonde Baba sinitishe, Ukimya si yangu Jadi
Ili ujisahihishe, Kukosoa inabidi
Kiakili nijishushe, kisa yako itikadi?
MAHARAGWE UNILISHE, NKIJAMBA NI MKAIDI?
Umenilisha Mandondo, Tumbo kujamba sharti
Njoo unipige Nondo,Kujamba siachi ati
Kamwe sitoenda kando, Nitajamba katikati
MAHARAGWE UNILISHE, NKIJAMBA NI MKAIDI?
Wapika aina aina, Mlaji kunipumbaza
Watiya Udi na Hina, Lengo lako kunilaza
Chumvi izidipo sana, Sauti nache kupaza
MAHARAGWE UNILISHE, NKIJAMBA NI MKAIDI?
Jikoni penye 'Mawingu', umpike Josefati
Kweli uwone majungu, piga kazi Hoti 'poti'
Nkinena watupa Rungu, niridhike na 'Makuti'
MAHARAGWE UNILISHE, NKIJAMBA NI MKAIDI?
Weye uote Kitambi, Miye Nyumba Kichuguu
Wacha nijambe mjambi, Tumbo lipate nafuu
Watatoa rambirambi, Wanangu na Wajukuu
MAHARAGWE UNILISHE, NKIJAMBA NI MKAIDI?
malenga wa Ngumbalu, 2017
Link:Kisima Cha Mashairi