Shairi:Maharagwe unilishe, nkijamba ni mkaidi?

IsangulaKG

JF-Expert Member
Oct 14, 2010
706
386
NYONGEZA 13/04/2017

Kujamba kujisafisha, nilisema mwaka Jana
Ndondo nikijazilisha, jambo hutowa laana
Hisi nakukasirisha, uwanja mpana sana
Weza amua kupisha, ama pualo kubana

Maharagwe unilishe, kijambo lazima kutowa
Nache utumbo nioshe, kwa ndani pakae sawa
Ondoa zako kasheshe, najamba kwondoa ukiwa
Hata pingu univishe, nkijamba utapagawa

Yaani kwa mwendo huu, najamba kisasasasa
Nitajambajamba fyuuu, degede nikitikisa
Harufu iende juu, ukome kunusanusa
Watajamba wajukuu, ukinifunga kitasa

Unaninyima vinono, tumboni kizungumkuti
Kwa supu ya Konokono, nisijambe kwa sauti?
Mlaji nina sonono, kumbeba 'mwanapoti'
Kubali yangu maono, pika umekunja Goti

@Malennga wa Ngumbalu, 2017

Facebook/kisimachamashairi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom