Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,539
- 4,854
KICHWA CHAKO NDO KITABU.
1)Kurasa ile ya kwanza,hufungui kwa mkono.
Hasa pale upo anza,wayafunua maono.
Kufungua wajifunza,nywele ndo yako maono.
Kichwa ni kitabu chako,acha akili isome.
2)kwenye mwanga funga macho,uone mbali zaidi.
Fungua ulichonacho,tafakari ikibidi.
Mengine fanya vificho,ujipambe kwa juhudi.

3)maandishi yake meusi,ya mulike kwa kalamu.
Ama vumbi la risasi,vizuri ujilaumu.
Jiepushe ni visasi,nyoia usimpe sumu.

4)tazama kivuli chako,na ukifunike na shuka.
Utembee peke yako,milima panda na shuka.
Waza tena peke yako,hofu ondoa na shaka.

5)kurasa hiyo ya mwisho,sasa soma na wenzako.
Ujilinde na vitisho,futa kati moyo wako.
Halitofika angusho,litadondoka anguko.

Shairi=KICHWA CHAKO NDO KITABU.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninga@yahoo.com
Facebook page=Idd ninga mashairi.