Shairi: HASIRA ZA MBINGU

Shairi: HASIRA ZA MBINGU

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,539
Reaction score
4,854
1>ya kale siyo ya sasa,dunia ya tetereka.
Inayotisha mikasa,ulimwengu weweseka.
Imeshamezwa na kasa,mdogo kuliko paka.
Hasira za mbingu kali,zaangamiza dunia.

2>yaangamia dunia,wenyewe tumeyataka.
Tumetia mbaya nia,tumeiruka mipaka.
Haki tunaikimbia,maovu tunayashika.
Hasira za mbingu kali,zaangamiza dunia.

3>dini tumeweka kando,shetani tunamtaka.
Ulimwengu kama pindo,lililojawa na shaka.
Inaanguka kishindo,wala hatujashituka.
Hasira za mbingu kali,zaangamiza dunia.

4>mafisadi wamezidi,na tena tunawataka.
Tumekuwa wakaidi,akili wametushika.
Kwingine ni ugaidi,mauaji na mateka.
Hasira za mbingu kali,zaangamiza dunia.

5>uchochezi kila kona,kama akili zaruka.
Wenye macho wasoona,akili zimepofuka.
Akili zimetubana,maono yametoboka.
Hasira za mbingu kali,zaangamiza dunia.

6>ukahaba na ushoga,hata frika umefika.
Kama viza wametaga,na kuku tushamzika.
Zimesha vunjika chaga,kwa laana twayosaka.
Hasira za mbingu kali,zaangamiza dunia.

7>mapambano kila mara,kwa vita tutayotaka.
Hatutoweza kung'ara,mbingu itapodondoka.
Tutaipata hasara,dunia itatoweka.
Hasira za mbingu kali,zaangamiza dunia.

8>yote yale yalofichwa,yanaanza dhihirika.
Dunia pasua kichwa,vipande inapasuka.
Hasubuhi hijakuchwa,ulimwengu wameguka.
Hasira za mbingu kali,zaangamiza dunia.

9>mvua inayonyesha,kama moto tulokoka.
Walimwengu wamekwisha,mafisadi watuteka.
Na mbingu twaichemsha,twasingizia mizuka.
Hasira za mbingu kali,zaangamiza dunia.

10>mvua inaunguza,na jua linachimbika.
Tumeingia kwa giza,hatutoweza kutoka.
Shetani ameagiza,wakupinga katoweka.
Hasira za mbingu kali,zaangamiza dunia.


Mtunzi: Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
0755519736/ 0655519736
 
shairi zuri linatufundisha nini.

kufumbua funzo lililopo ndani ya shairi hilo mhhh haifai,ila subiri watakuja watu wataweka wazi.
Mi nikisema nilichokusudia hapo,utazuka mjadala mwingine.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom