Shahidi wa sita kumzamisha Zitto Kabwe

Shahidi wa sita kumzamisha Zitto Kabwe

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2019
Posts
319
Reaction score
755
ZITTO Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, anayetuhumiwa na tuhuma za uchochezi, kesho shahidi wa sita anatarajiwa kutoa ushahidi dhidi yake. Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Shahidi huyo atatoa ushahidi wake kesho tarehe 13 Agosti 2019 pale Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini atakapopanda kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusikiliza ushahidi huo.

Zitto anatuhumiwa kutoa maneno ya uchochezi kuhusu mauaji yaliyotokea Nguruka, Kigoma. Kesi hiyo ipo katika hatua ya usikilizwaji ambapo upande wa Jamhuri umefikisha shahidi wake wa tano Dk. Ernest Nsumila ambaye aliyetoa ushahidi wake tarehe 16 Julai 2019.

Upande wa utetezi unaongozwa na wakili Peter Kibatala, Dickson Matata na Steven Mwakibolwa ambapo upande wa Jamhuri unawakilishwa na wakili wa serikali mwandamizi Nassoro Katuga.

Huruma Shahidi, ndiye Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo ambapo inatarajiwa upande wa Jamhuri kumpeleka shahidi wa sita.

Dk. Nsumila katika ushahidi wake, alieleza kuwa yeye ni daktari katika kituo cha afya Nguruka, wilayani Nguruka, Kigoma ambapo aliwatibu majeruhi watatu wanaodaiwa kuwaua askari polisi wawili.

Akiongozwa na wakili Katuga ambapo, Dk Nsumila alidai tarehe 18, Oktoba 2018 akiwa kituo hapo alipokea majeruhi watatu wote wakiwa ni wanaume.

“Nilikuwepo kazini tangu asubuhi, ilipofika saa 12 jioni nilipokea majeruhi watatu, wote wanaume wanaotokea Kijiji cha Mpeta wakidai wamepigwa risasi na askari polisi kwa madai kuwa, walivamia maeneo ambayo hayatakiwi kufanya kilimo,” alidai.

Alieleza kuwa, majeruhi hao walikuwa na majeraha ya risasi huku wakiwa hawawezi kusimama na kuongea vizuri ambapo katika kuwahoji zaidi, walisema wamepigwa risasi na polisi katika pori la Mwanduhubandu lililopo Kijiji cha Mpeta, Uvinza

Katika kesi hiyo, Zitto anakabiliwa na mashtaka matatu ya uchochezi ambayo anadaiwa kuyatenda tarehe 28 Oktoba 2018 katika mkutano na waandishi wa habari, uliyofanyika kwenye Makao Mkuu ya Ofisi ya Chama cha ACT Wazalendo
 
Ngoja akaonje burudani ya segedansi labda atakoma kutumika na mabwanyenye nashauri alambe viboko 6 akiwa anaingia gerezani na akitoka alambe vingine 6 akawasimulie mabeberu wake.
Pamoja sana kiongozi
 
Inategemea ushahidi wenyewe utakuwa na uzito gani, acha kuandika kwa mihemuko
 
Sedition charge si rahisi kuithibitisha, labda kwenye compromised judiciary kama yetu ya juma!

Incitement and sedition is that incitement is a call to act; encouragement to act, often in an illegal fashion while sedition is organized incitement of rebellion or civil disorder against authority or the state, usually by speech or writing.
Sidhani kama Zito alifanya lolote in the context of that definition
 
Kwahiyo na wewe ni mpumbavu, miongoni mwa wapambavu aliowataja katibu mkuu?
 
Ngoja akaonje burudani ya segedansi labda atakoma kutumika na mabwanyenye nashauri alambe viboko 6 akiwa anaingia gerezani na akitoka alambe vingine 6 akawasimulie mabeberu wake.
Kuwa mjinga sio lazima utudhibitishie hapa kuwa uko hivyo
 
sedition charge si rahisi kuithibitisha, labda kwenye compromised judiciary kama yetu ya juma!

Incitement and sedition is that incitement is a call to act; encouragement to act, often in an illegal fashion while sedition is organized incitement of rebellion or civil disorder against authority or the state, usually by speech or writing.
Sidhani kama Zito alifanya lolote in the context of that definition

Kwa jicho langu lisilo la kisheria kosa la Zitto ni kutia chumvi kwenye jambo ambalo inaelekea ni kweli limetokea. Whether that amounts to sedition or incitement it is for the courts to decide. Lakini nadhani pia lengo la jamhuri siyo kumtia hatiani bali kumpotezea muda wa kufanya mambo ya maana zaidi kwake kisiasa!
 
Nadhani uko sahihi kabisa. Wanajua fika kuwa hawawez kumtia hatiani kwa kosa lolote hapo!
 
Back
Top Bottom