Shahidi aeleza alivyoingiliwa kimwili na mganga

Ifike wakati watu wajifunze, na wajue uongo mkubwa wa hawa waganga.
Watu wanadanganywa kama watoto wadogo, halafu baada ya kudanganywa, bado kuna watu wanawatetea humu JF.

Hebu tujikumbushe kuhusu udanganyifu wa mganga huyu....

Mnamkumbuka tapeli huyu aliyesababisha vifo vya watu wengi sana..???

Babu wa Loliondo..

Watu walimuamini sana kwa sababu ya ujinga wao, watu walakiwa pesa zao na hawakupona.
Wakati ule huyu babu angesema kuwa sharti mojawapo la kupona ni 'kuingiliwa' kimwili, kuna watu wangekubali..!!!!
Watu hao hao pia wangepeleka magari yao huko wakampe mganga..!!

Mpaka leo hakuna watu tena wanaoenda huko....

Hapo unaweza kusema kuwa watu hawaugui tena..?? Mbona hawaendi huko Samunge..??

Lukuvi%2B%2526%2BRosemary%2Bin%2BLoliondo_.jpg

Kwa upande mwingine mjinga akifundishwa anaweza kuwa mjanja, ila unapoita wajinga wakati kuna public figure zili attend samunge, unanitia shaka na hii lugha yako.
Kama kuna kiongozi wako wa nchi alifika kule samunge naye ni mjinga? anawezaje kukuongoza?
The truth has to be told in the right way not by calling people bad names.
 
Umeandika mengi sana.
Ila hapo kwenye blue, suluhisho ndio hili hapa chini kwenye Maandiko ya Biblia....
Msikimbilie kwa waganga wa kienyeji, halafu mnakuja kilia-lia baadaye.
Mganga wa kienyeji hakumfuata huyo mwanamke nyumbani kwake.
Badala yake huyo mwanamke alienda kwa mganga kwa hiyari yake mwenyewe...!!! Au hapo utabisha..?????

Kwa hiyo, badala ya kuunga mkono watu wanaoenda kwa waganga, unga mkono watu wanaoenda kwa Yesu.

Yesu alisema kwenye Maandiko....

Mathayo 11:28 - 30 inasema....

28 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.

Ndugu yangu Muisraeli kuja kwa Yesu sijakataa ila;
Mara ngapi hawa wachungaji wa kondoo wamewatumia dada na mama zetu wenye shida kama hizo?
Hapa tuombe neema ya Mungu ili kila mtu apate kadili ya matendo yake.
Hawa watu wanalengwa na makundi yote ya utapeli mpaka huko makanisani shughuli ni moja tu.
 
Back
Top Bottom