Shahidi aeleza alivyoingiliwa kimwili na mganga

Magazetini

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
588
1,698

mahakamaz_300_173.jpg

SHAHIDI wa pili katika kesi ya kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu inayomkabili mganga wa kienyeji, Yahaya Michael (34) ameieleza Mahakama ya Wilaya ya Ilala jinsi alivyoingiliwa kimwili na mganga huyo kwa madai kwamba atampatia dawa ya kupata mtoto.

Mwanahamisi Omary (26) alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Hassan Juma kuwa alimfahamu mganga huyo baada ya kusumbuliwa na tumbo la uzazi kwa muda mrefu.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali Felista Mosha, Mwanahamisi alidai alikuwa akitibiwa ugonjwa huo bila ya kutoa taarifa kwa mumewe Edrick Elinezer. Alidai alitibiwa kwa miezi sita bila ya mafanikio.

Shahidi huyo alidai Aprili, mwaka huu, Michael alimwambia kuwa ana majini hivyo hawezi kupata mtoto na kumpatia dawa kwa ajili ya kunywa na kuoga.

Alidai mganga huyo alikuwa akimtibu nyumbani kwake lakini baadaye alihamishia ofisi yake katika nyumba ya kulala wageni iliyopo Kigogo Luhanga na kudai kuwa mganga huyo alikuwa akipaka dawa katika uume wake na kumuingilia kimwili huku akiwa hajitambui kwa madai kwamba atamsaidia kupata mtoto.

Aliendelea kudai kwamba baada ya kutokuwa na mawasiliano kwa muda mrefu na mumewe, alipata taarifa kuwa mume wake alipigiwa simu na mganga huyo na kumtaka apeleke gari lake Toyota Rav4 lenye namba za usajili T 139 BSG maeneo ya Jangwani kwa kuwa majini ya mkewe yanataka mtoto.

Awali, Hakimu Juma alisema wadhamini wa mshitakiwa wanatakiwa kumtafuta mshitakiwa huyo na kumfikisha Mahakamani hapo, aliwatahadharisha wasipofanya hivyo kwa wakati watalipa faini ya Sh milioni sita kwa kila mmoja.

Michael alidaiwa Aprili 29, mwaka jana, maeneo ya Jangwani Wilaya ya Ilala, alijipatia gari aina ya Toyota Rav4 T 139 BSG lenye thamani ya Sh milioni 12 mali ya Eliezer kwa njia ya udanganyifu. Kesi hito itasikilizwa tena Septemba 18, mwaka huu.

CHANZO: Habari leo
 
Wote mazuzu.
Mtoto anapatikana kwa Maombi yako wewe na mungu.
Mumewe Zoba mkewe Zoboka.

Halafu Serikali iangalie,huu mtindo wa waganga wa kienyeji kufikia magesti ni wa zamani sana.Hizi gesti hasa za uchochoroni ndio balaa.

Mie mke wangu nilikaa nae miaka mitatu bila mtoto wala hata sikustuka,maana kw age yangu ile ya 25 mtoto haikuwa concern kubwa kwangu,ila baada ya muda huo mtoto wa kwanza na baada ya miaka mitatu wa pili and all are doing very well shuleni.
Sasa unaweza kulazimisha madawa haya ya ukapata mtoto ukapata chizi

Milioni Sita?kisa mtoto?mie ningekuwa hakim ningemuamrisha mganga amuingilie tena hapo hapoa.
Na huyo mama ni muongo,hajapewa dawa wala nini,walikubaliana,kuna makabila ni watu wa dili asije kuwa huyo mama kapiga dili likagoma.
Maana unaweza kukuta na hili ushahidi ninao kwamba mwanamke akiona hali hiyo anageuza mtaji,maana anajua mwanaume unataka mtoto basi atakomba pesa zote kwa kushirikiana na waganga,sasa inawezekana kwenye dili hili mgao wa mganga ulikuwa kidogo ndio wakaona wachomane.
Huyo mume aulizwe vizuri kwamba mkewe aliisha sababisha hasaraya kiasi gani kwa ajili ya waganga.Hawa madada siku hizi noma.
Kwanza Demu muislam mumewe mkristo,na huyo Dada ni kwamba kwao wamemtenga kiimani.Sasa utakuta yeye anamipango yake mingine kabisa na wala sio ndoa.ufupi Dada kapiga issue nyingi sana kwa mumewe kwa kisingizio cha kupata mtoto,sasa hii mganga kagoma kutoa mgao,ndio mwanamama kampeleka Mahakamani
 
Daaah kuna watu akili zao upeo wao umefichwa na Adui kwenye mashimo. Daah hii ni Balaa kwa kweli. Yesu ndo jibu la kila kitu
 
Duh kweli wewe ni "Zanzibar Spices" una uwezo mkubwa saana wa kutia viungo kwenye story utadhani ulikuwepo!
 
Nnachokiona mie kuna uongo upande wa mgonjwa kama alikua anaingiliwa akiwa hajitambui alijuaje?uyo kila k2 alikiona mwanzo hd mwisho wa mchezo ila kaona hkn matumaini ya kupata mtt ndomana anasema ivo,ujinga tu.
 
Tukio la kupaka dawa uume,shahidi aliliona lkn wakati wa kuingiliwa anakuwa hajitambui!! Hapa ndo najiuliza,nilichokisoma nimekielewa kweli!!? Ngoja nisome tena ntarudi.
 
duh dunia hii kweli kuta zinaficha mengi...unahamia gesti kwenda kupata matibabu
 
Hapa inaonyesha kuwa Shetani yuko kazini kiweli-kweli.

Yaani mtu mzima unakubali kuingiliwa na mganga ili upate mtoto.

Yaani mtu unakubali kupeleka gari lako kwa mganga eti majini yamefanya nini sijui..!!!

Hapo utakuta watu hao hao, ukiwaambia kuwa huyo mtoto wanayemtafuta anaweza kupatikana kwa kuombewa kanisani, tena bure kabisa, na kwa usalama kabisa, watabisha mpaka kesho.
Ila kwa mganga wanaenda mbio-mbio kwenda kuingiliwa..!!!

Yesu alisema kwenye Maandiko....

Mathayo 11:28 - 30 inasema....

28 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.
 
huyo dada msanii, wakati uume unapakwa dawa aliona, wakati anaingiliwa alikua hajitambui, sasa alijuaje kama kaingiliwa?
 
Hata huyo hakimu ana lake jambo. Mtu kaingiliwa, kwenye tundu sahihi, mchana peupe, tena anaangalia dawa ikiwekwa kwenye sindano inayotumika, jamani. Hakimu, ka unasomaga jf, mwambie huyo mmama akatafute kesi nyingine. Hii so kesi. Ulitaka aiwekeje hiyo dawa mahali stahiki?? Mbona tunapochomwa xpen lazima iingizwe mwilini kwa syirinji tena nene tu unasikia maumivu mpaka unalia.
Hao manesi mbona hatuwapeleki mahakamani kwa kutuchoma misindano yao hiyo. Tena siku hizi unaruhusiwa kwenda nayo kwani ni desposable? Huo si ndo ushahidi mahakamani??
Nilidhani aliingiliwa kinyume na maumbile mpaka akachanika kumbe ujinga tu. Tangu lini mtoto akapatikana kwa mbegu ya mganga wala sio mumeo??
Mama eleza aliyekupa hilo limbwata ulilomlisha mumeo mpaka akawa zuzu. Nasema, huyo mganga ni dokta sahihi kabisa. Dawa zake haziingizwi kivingine, tena ilitakiwa mumewe akae pale aangalie dawa ikiingizwa. Full stop
 
mahakama inapoteza muda kushughulikia kesi za kijinga kama hizi..
siamini hadi leo kuna watu wanaenda kufanya uchawi! hahaha
 
Mbulula ni mbulula tu hata karne ya 21 bado mambulula wapo kibao tena katikati ya Mji.
Kweli nimeamini hata Washngton bado utawakuta hawa mambulula .. wataendelea kuliwa wakishtuka kumekucha!!
 
Back
Top Bottom