Shahada za kura zachomwa moto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shahada za kura zachomwa moto

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Konaball, Sep 10, 2009.

 1. K

  Konaball JF-Expert Member

  #1
  Sep 10, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 1,776
  Likes Received: 466
  Trophy Points: 180
  SHAHADA za kupigia kura zinazokadiriwa kufikia milioni moja, zimeteketezwa kwa kuchomwa moto katika mazingira ya kutatanisha jijini Dar es Salaam.

  Shahada hizo ziliteketezwa na watu wasiojulikana ndani ya eneo la Bohari Kuu inayohusika na utunzaji wa nyara za serikali, iliyoko eneo la Keko, wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam.

  Baadhi ya shahada hizo zilizoshuhudiwa na waandishi wa habari wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, zilikuwa za wapiga kura wa Mkoa Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es Salaam za mwaka 2005 na 2008.

  Shahada zilizoandikishwa jijini Dar es Salaam, nyingi zimetoka katika maeneo ya Manzese na Mwananyamala.

  Hadi sasa haijulikani namna gani shahada hizo za kupigia kura zimekusanywa kwa wingi na kupelekwa kuteketezwa ndani ya eneo la Bohari Kuu ya Serikali.

  Kuwapo kwa shahada hizo ndani ya Bohari Kuu na mpango wa kutaka kuziteketeza, kuligunduliwa na viongozi wa CUF ambao walipata tetesi kuanzia juzi.

  Inasemekana kuwa, shahada hizo ambazo zinaonyesha picha na majina ya wapiga kura mbalimbali nchini, ziliteketezwa juzi, lakini baadhi yake zilibaki ndipo Profesa Lipumba aliwakusanya waandishi wa habari na kuingia nao kwenye bohari hiyo kwa siri kwa kutumia gari yake yenye vioo vya kiza.

  Mara baada ya kushuka ndani ya eneo hilo la bohari, Profesa Lipumba aliwaongoza waandishi wa habari hadi lilipokuwa lundo hilo la shahada na kuanza kuzichambua moja baada ya nyingine na kisha kuzifunga kwa mafungu kwenye mifuko ya plastiki na kuzipakia kwenye gari lake.

  Wakati Profesa Lipumba aliyeongozana pia na baadhi ya wabunge na viongozi wa CUF wakichambua shahada hizo, wafanyakazi wa Bohari hawakujitokeza, lakini baada ya kuanza kuzungumza na waandishi wa habari juu ya tukio hilo, baadhi yao walijitokeza katika eneo la tukio na kushangaa.

  Akizungumzia tukio hilo ndani ya eneo hilo la Bohari Kuu, Profesa Lipumba, alisema tukio hilo linadhihirisha mbinu chafu zikifanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) chini ya uratibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

  “Angalieni kadi hizi, haya ndiyo matunda ya kutokuwa na Tume Huru ya Uchaguzi, kila kukicha ni wizi tu hakuna uwazi wala ukweli,” alisema Lipumba huku akionyesha mabaki ya shahada zilizoungua.

  Alisema vitambulisho hivyo vinatumika katika kupiga kura za utapeli na viongozi mbalimbali wa CCM wanaovinunua kwa ajili ya kurubuni na kuvuruga uchaguzi.

  Alibainisha kuwa, kamwe demokrasia haiwezi kuendelea kama hila za kupata idadi kubwa ya hesabu za kura hizo zinazofanywa na CCM hazitakomeshwa.

  Aliongeza kuwa, bohari ni sehemu ya kutunzia nyara za serikali, hivyo kukutwa kwa shahada hizo zikichomwa moto katika eneo hilo ni ushahidi kuwa serikali inahusika.

  Alisema serikali inayopora haki ya mpiga kura kwa kupata ushindi kwa njia isiyo halali, haiwezi kuwaletea maendeleo wananchi.

  Naye Mbunge wa Michewani, Shoka Hamisi Shoka, alisema hila hizo za kuwepo kwa shahada bandia, aliwahi kuzizungumzia bungeni kwamba CCM inahusika na ununuzi wa shahada za wapiga kura, lakini walipinga.

  Alisema wakati akiwawasilisha hoja hiyo bungeni, Spika wa Bunge, Samuel Sitta, alipinga kwa nguvu hoja hiyo na kumtaka atoe ushahidi wa hicho anachokisema.

  “CCM walinitolea macho, Spika wa Bunge Samuel Sitta alinitaka kutoa ushahidi wa kununua shahada za kura, na huo ndiyo ushahidi mmojawapo.

  “Bohari ni mali ya serikali ambayo inaongozwa na CCM, kutokana na suala hili wanahusika moja kwa moja na ununuzi wa kura,” alisema Shoka.

  Naye Mkurugenzi wa Ulinzi wa CUF, Mazee Rajabu Mazee, alisema siku zote CUF wamekuwa wakilalamika kutokuwapo kwa tume huru ya uchaguzi, lakini wamekuwa wakipuuzwa.

  Alisema tukio la kukutwa shahada hizo zikiteketezwa, kumedhihirisha jambo hilo ambalo watu walikuwa hawaamini.

  “Siku za mwizi arobaini, CCM walizoea kuiba na leo ndiyo wamefikia tamati, shahada hizi ni nyingi sana, zaidi ya milioni moja. Ni Watanzania wangapi wametangaziwa kiongozi asiye chaguo lao?” alihoji Mazee.

  Akizungumzia sakata hilo kwa njia ya simu jana, Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Rajabu Kiravu, alisema ofisi yake haihusiki kwa aina yoyote ya uchomaji huo wa shahada za kupigia kura.

  Hata hivyo, Kiravu alieleza kushangazwa na namna ujumbe wa Profesa Lipumba na waandishi wa habari walivyoweza kuingia katika eneo la tukio.

  “Ofisi yangu haihusiki na uchomaji huo, kwanza mliingiaje maeneo ya Bohari?” alihoji Kiravu.
   
 2. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #2
  Sep 10, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kwa nini wanazichoma sasa? mi nilifikiri kama lengo ni kuiba kura, sasa ndo wangekuwa wanazinunua kwa wingi for 2010!
   
 3. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #3
  Sep 10, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Na ndio tabia ya wizi wa kura ndio inapoanzia, Sasa kwanini wazichome bila ya kutaarifu watu wale wahusika?? kuna namna hapa ambayo tume ndio inapaswa wajibu na tena wao wanasema kuwa ni sehemu ya IT ya NEC?/ sasa Je unategemea nini kinafuata kama sio wizi wa kura
   
 4. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #4
  Sep 10, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Hii ni hali mbaya ktk ulimwengu wa demokrasia, shame on us...

  Source of picture: Mwananchi news paper Thursday, September 10, 2009
   

  Attached Files:

 5. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #5
  Sep 10, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Usaliti wa halii ya juu wa demokrasia, lazima mkuu wa bohari kuu ajiuzulu bila kupata shinikizo. Unajua tofauti ya kura kilioni oja katika uchaguzi unatranslate kwenye nini?

  Kama mkuu wa upelelzi wa uingereza alijiuzulu kwa baadhi ya documents nyeti kupigwa picha na waandishi kwa nini huyu mkuu wa bohari anayetakiwa kujua na kinachotoka asiwajibishwe?

  awajibishwe kwa kudumaza demokrasia na kuitia hasara serikali, tujiulize gharama za kutoa kitambulisho kimoja ni kiasi gani, assuming ni shs 1,000/= basi vitambulisho 1,000,000/= ni shs 1,000,000,000/=. Kwa hiyo hela tungepata vyandarua 154000 bure kwa wananchi, just going in fire like that i cannot believe.

  Tukumbuke kuwa wakati wa kuaandaa daftari la kudumu la wapiga kura zoezi hili lilikuwa chini ya bohari kuu, hebu tujiulize kwa nini zoezi liwe chini ya bohari badala ya tume ya uchaguzi ambao ndio custodian wa nyaraka za wapiga kura. Simply speaking ina maana kuna shahada nyingi extra zilitenngenezwa, swali ni je kwa faida ya nani?

  Mkuu wa bohari ajibu masuali haya,
   
 6. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #6
  Sep 11, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Jina la sheria na madhumuni yake:

  CHAPTER 309
  THE RECORDS AND ARCHIVES MANAGEMENT ACT
  An Act to establish the Records and Archives Management Department to provide for the proper administration and better management of public records and archives throughout their life cycle, to repeal the Records (Disposal) Ordinance *, and the National Archives Act *, and for connected matters.

  Public Record ni nini?

  "public records" means the records specified in the Schedule to this Act;

  Schedule hiyo inasemaje?

  Save for the records of the Public Trustee or of the Administrator-General which relate to individual trusts or estates, the following are public records–

  1. The records and archives belonging to the United Republic created, received
  and maintained:
  (a) in the offices of the President and of the Cabinet;
  (b) by any ministry, department, commission, committee, office or other body
  under the Government of the United Republic or by the Minister or any
  other officer or employee thereof;
  (c) by any post representing the Government of the United Republic outside
  the country or any officer serving in such a post;
  (d) by any information or unit of the armed forces of the United Republic or any
  officer of such a formation or unit;
  (e) by the Parliament or Electoral Commission or any committee or officer
  thereof;

  (f) by the Court of Appeal, High Court or any other court or tribunal with
  jurisdiction within the United Republic or by any Judge, Management or
  other officer of such a court;
  (g) by any local authority or officer thereof;
  (h) by any predecessor or successor of any of the institutions, bodies or
  individuals designated in (a) to (g) above;
  (i) by any other body or individual so designated by the Minister by regulations
  made in accordance with section 28 of this Act.

  Je shahada ya mpiga kura ni public record?

  Bila shaka soma kifungu ( e ) hapo juu.

  Je Public Record inatakiwa ikae muda gani?

  16. Thirty years rule
  (1) Subject to any written law prohibiting or limiting the disclosure of information in any public record, public records in the National Archives, in any other archival repository under the control of the Director or in a place of deposit appointed under section 15 of this Act, shall be available for public inspection after the expiration of a period of thirty years from their creation, calculated as prescribed in subsection (2) of section 4 of this Act, except in so far as a longer or shorter period may have been prescribed by the Minister by regulations made in accordance with section 28 of this Act at the request of the head of the public office which created the records or its successor in function.

  Je shahada zilitengenezwa lini?

  2004

  Wadau tulijadili hili
   
 7. K

  Kijunjwe Senior Member

  #7
  Sep 11, 2009
  Joined: Mar 3, 2007
  Messages: 182
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Baadhi ya Vitambulisho vilivyookotwa vinaweza kutumiwa kutafuta uwepo wa wamiliki au kama ni vitambulisho hewa, vinginevyo inawezekana wapo wamiliki lkn tayari wana vitambulisho ama wako nje ya maeneo yaliyotajwa kuwa vimetoka.

  Hisia!
  Yawezekana utofauti wa kura katika jimbo la ubungo ulitokana na baadhi ya vitambulisho hivi kutumika mara 2 au zaidi.
   
 8. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #8
  Sep 11, 2009
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Source: Tanzania Daima

  "SIKU moja tangu kutokea kwa tukio la kuchomwa moto kwa shahada za kupigia kura ndani ya eneo la Bohari Kuu lililopo Keko jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Rajabu Kiravu ametolea ufafanuzi tukio hilo. Kiravu katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, alikiri kuwepo kwa uchomwaji moto ndani ya eneo hilo la Bohari Kuu ambapo NEC ina ofisi yake, lakini alisema tukio hilo halina madhara kwani shahada zilizochomwa ni zile zilizorudishwa na wamiliki wake baada ya kubainika kuwa hazifai."

  Jibu hilo hapo wakuu!!!
   
 9. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #9
  Sep 11, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Sheria hiyo hapo juu ipo wazi public document inatakiwa iwe destroyed baada ya muda fulani je hizo zimekuwa destroyed katika muda unaotakiwa kisheria? Ukitokea ubishi leo kuwa xyz ambaye amekufa alikuwa na shahada au la ushahidi utatoka wapi wakati shahada zimeunguzwa. Hebu pitia vipendegele hivyo hapo juu kuhusu sheria ya kuharibu documents.

  Pili hii ni afterthought jibu lake la mwanzo alipoulizwa na waandishi wa habari ni kama ifuatavyo
  " Akizungumzia sakata hilo kwa njia ya simu jana, Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Rajabu Kiravu, alisema ofisi yake haihusiki kwa aina yoyote ya uchomaji huo wa shahada za kupigia kura.

  Hata hivyo, Kiravu alieleza kushangazwa na namna ujumbe wa Profesa Lipumba na waandishi wa habari walivyoweza kuingia katika eneo la tukio.

  “Ofisi yangu haihusiki na uchomaji huo, kwanza mliingiaje maeneo ya Bohari?” alihoji Kiravu

  ona thread ya je Mh Kikwete alishinda 2005- alert
   
Loading...