Shahada ya uzamivu (PhD) ya Mwakyembe si halali?

Shahada ya uzamivu (PhD) ya Mwakyembe si halali?

Wanafiki wapika majungu hamjambo, endelee kuleta mada za kinafiki hapa ili muweze kuganga njaa. Unaposema PHD ya Dk.mwakyembe ni feki baba yako au wewe unayo, acheni unafiki wa kinjaa njaa, Dk.Mwakyembe ni kichwa.Unafiki wenu hauna maana. Kwanza lzm mtumie akili, Dk.Mwakyembe hayasema lolote kuhusu maelezo ya mnafiki wa Chadema LISSU kwa hiyo mnamhukumu Mwakyembe tu kabla yeye hayajibu kitu. Wajinga kweli. Bahati mbaya mnaochangia humu wote asilimi 98 ni mi-Chadema.
Uko very wrong!Extremely wrong!Mie ni CCM, na kabla ya hii thread fuatilia thread zangu nyingine!Kuhusu kitabu huna haja hata ya kuuliza kama mjomba wangu au bibi anayo hiyo PhD!Umri unaniruhusu kutokuwa nayo,ila for sure nitaipata ambayo nina uwezo kuitetea popote!Taifa kwanza u-chama baadae!
 
Ni ajabu mtu anapotofautiana na utafiti wake wa kitaaluma uliompatia PHD mara baada ya kuipata hiyo PHD. Ni vigumu kuelewa jambo hili. Dr. Mwakyembe atuambie ama aliiba utafiti huo ama alifanyiwa na mtu mwingine. Tafadhali chuo kilichompatia PHd ni kipi watende haki. Sio bure.
 
Huyu FISADI wa ELIMU alisomea PhD yake katika chuo cha Hamburg University. PhD Dissertation title yake: anzania's eighth constitutional amendment and its implications on constitutionalism, democracy and the union question (Printed for mass consumption with ISBN: 3-8258-2424-1)

Kwakweli inasikitisha na inatia aibu kubwa kwa kiongozi mkubwa kama huyu, tena alikwisha kuwa muhadhiri katika chuo kikuu. Kwa tukio hili la kuisaliti utafiti wake uliompatia title kubwa anayoendelea kuitumia mpaka sasa, ni dhahiri hakustahili kufanya majukumu yanayolingana na taaluma aliyohitimu kwa tafiti hii. Msaliti huyu amesimamia wanafunzi wengi na kufanya kazi nyingi zinazolingana na taaluma yake, hivyo output yote inawezekana ni feki. Tunalalamika elimu yetu inashuka kiwango, kumbe kunawatu wamethaminiwa kusimamia, na kufanya utapeli unaoligharimu Taifa. Ni dhahiri pia kazi hii imetumika na watafiti wengine katika kazi zao, kwani it was published for mass consumption. Hivyo imeweza kugharimu kazi nyingine za watu kwa udanganyifu aliouandika kama matokeo ya tafiti yake.
 
Mimi nilishamwambia wazi mapema hapa ingawa modes wlaijitahidi sana izimisha kumbe mzimu unarudia..Mwakyembe na shivji km wanaamini walichofanya ni makosa ua riwaya tuu,basi na matoke ya hizo riwaya ni makosa wangejiwajibisha urudisha tuu....otherwise chuoa lichosoma nacho kinaweza pewa taarifa..ili kianze mchakato kwa kuwasiliana naye ili ajieleze km sababua bad ni hizi warecall tuu PHD yao.
 
Amefanya nini; tufahamisheni tujue.

Tatizo ni kuwa kumnyangaya mtu digrii kunaendana pia na kumwadhibisha mwalimu aliyemsimamia na kutoa mapendekezo kwenye senate kuwa mtu huyo apoewe digrii hiyo. Digirii ya Ph.D hutolewa na chuo kwa mapendekezo ya msimamizi wa mwanafunzi husika; huyo ndiye anayeweza kutoa mapendekezo tena kwa chuo kuwaambia kuwa amepata taarifa mpya zinazooneysha kuwa Mheshimiwa hakustahili rights na privileges za digrii hiyo.
 
Kichuguu kinataka kusema kama huyo mwalimu aliyesimamia na hatimaye kupendekeza mwanafunzi atunukiwe digrii husika amekwisha kufa, basi hakuna njia nyingine yeyote ya kusawajisha makosa ya aina ya mwakyembe!!!!!!

kama ndivyo basi mfumo huu hauna auto-equilibrium formation.

Wasomi wanashirikiana kuiangamiza dunia yetu. Wataalam wanajitahidi kuitengeneza.
 
Last edited by a moderator:
Ni ajabu mtu anapotofautiana na utafiti wake wa kitaaluma uliompatia PHD mara baada ya kuipata hiyo PHD. Ni vigumu kuelewa jambo hili. Dr. Mwakyembe atuambie ama aliiba utafiti huo ama alifanyiwa na mtu mwingine. Tafadhali chuo kilichompatia PHd ni kipi watende haki. Sio bure.

Mtu anaweza kutofautiana na utafiti wake wa mwanzo, kama amefanya tena utafiti wa jambo hilo hilo na kupata matokeo tofauti kabisa na utafiti wake wa mwanzo. Huenda Dr. Mwakyembe alifanya utafiti na kupata matokeo mengine. Kama ni hivyo tunaomba Dr. Mwakyembe atueleze ni lini alifanya utafiti wake huo ambao ulionesha kwamba S2 ndiyo sasa zinafaa kwa JMT badala ya S3 kama ulivyo kwenye utafiti wake wa mwanzo. kama hukufanya huo utafiti uliompatia matakoe tofauti No Research No Right to Speak, basi Dr. Mwakyembe atakuwa amebaka thesis yake na anatakiwa avuliwe huo u doctorate with immediate effect.
 
Tafiti ngapi haziendani na uhalisia?? His paper was just an ideal and some time it is very difficult to put into practice. Maana yake ni kwamba siyo kila kitu kinachoandikwa kwenye makaratasi kinaweza kutekelezeka katika mfumo wa maisha ya watu. Usipaniki brother!
 
Kichuguu kinataka kusema kama huyo mwalimu aliyesimamia na hatimaye kupendekeza mwanafunzi atunukiwe digrii husika amekwisha kufa, basi hakuna njia nyingine yeyote ya kusawajisha makosa ya aina ya mwakyembe!!!!!!

kama ndivyo basi mfumo huu hauna auto-equilibrium formation.

Wasomi wanashirikiana kuiangamiza dunia yetu. Wataalam wanajitahidi kuitengeneza.

Unfortunately huo ndio ukweli wenyewe kwa sababu katika elimu ya juu, academic freedom inatoa mamlaka ya mwisho kwa mwalimu wake, hasa kwa ile doctoral academic committee yake. Iwapo kamati inaridhika, hakuna wa kumnyang'anya digrii hiyo unless Senate ya chuo iwatie kwenye hatia ya academic misconduct waalimu wote waliomsimamia katika kamati yake ya dissertation.
 
mtoa maada nisaidie kuna sehemu mwakyembe kasema anataka.s2
 
Tafiti ngapi haziendani na uhalisia?? His paper was just an ideal and some time it is very difficult to put into practice. Maana yake ni kwamba siyo kila kitu kinachoandikwa kwenye makaratasi kinaweza kutekelezeka katika mfumo wa maisha ya watu. Usipaniki brother!

sio hivyo tu maisha hubadirika

suppose zenj na Tanganyika zingevunja muungano, bado angehoji apokonywe??
 
Kutokana na nukuu zinazoendelea kutolewa na wachambuzi mbalimbali (Hapa namuongelea Lissu) katika mchakato wa katiba mpya, imethibitisha pasipo shaka kuwa Mh. Dr. Mwakyembe anakikana kile alichokiandika miaka ya Tisini ili kupata udaktari wa falsafa (PhD).

Katika kitabu chake alinukuliwa akisema kuwa muundo wa muungano wa Tanzania ni shirikisho pasipo na shaka, na kuthibitisha kuwa migogoro itamalizwa kwa kuwa na serikali tatu! Ni kwa hoja zake hizo aliweza kutunukiwa shahada ya uzamivu (PhD). Sasa kwa kuwa anazikana hoja hizo maana yake ni kuwa alipotosha watu katika utafiti wake!

Aidha aliegemea upande ambao alikuwa anautaka (bias) au aliamua kufuata wengine walisemaje!Sasa kwa kuwa hata yeye hauamini utafiti wake je sio haki yake kuondolewa udaktari wake!?

Prof. Shivji nae ameyakana maandiko yake ya miaka ya 90, ambayo mengine aliyatumia kupanda cheo mpaka kuwa profesor, je nae sio haki yake ashushwe cheo hicho?

Nawasilisha.

siku zote nimekuwa nikisema mwakyembe ni mnafiki na ni janga la taifa.Yeye pamoja na sita ni mijitu minafiki sana.Bado mtaendelea kuona unafiki wao.Hovyooooo
 
Je nyakati tofauti haziwezi kumfanya mtu kuwa na mitizamo tofauti? Najiuliza tu.

inawezekana pia ila ninachoelewa unapaswa kwanza kukili kwamba mtizamo wako wa awali ulikuwa huu na mtizamo wako wa sasa ni huu, lakini pia unapaswa kueleza kwanini umeahama kutoka kwenye mtizamo wa awali kuja kwenye mtizamo mpya
 
Back
Top Bottom