Shafii Dauda na wenzako, mnajifunza Euro 2016?

mmteule

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
5,878
14,540
Nadiriki kusema hapa Tanzania waandishi wa habari ni kikwazo saaaaana katika nyanja mbalimbali za ustawi wa Taifa letu kutokana na namna wanavyoripoti taarifa mbalimbali.

Mnakuza saaana matukio mabaya ili nchi yenu/yetu ionekane kituko kwenye mataifa mengine. Naamini huwa hamjui madhara yake ni nini, maana kila mtu anajua waandishi wa habari mnatokea wapi. Sijui kama mnapishana kwa chochote na wale watoto waliofukuzwa UDOM.

Tuyaache hayo.....Turejee kwenye EURO 2016, Mashabiki wa Urusi na Uingereza walizipiga kavukavu. Mashabiki wa Uingereza walifunga mtaa kwa vurugu na vipigo na kuziba barabara. Jezi za Uswisi zilichanika takribani 4 kwa mechi moja. Ronaldo alikosa Penati n.k n.k. Yaaaaaaaani nilifurahia saaaaaana jinsi waandishi wa Habari wa Mataifa hayo walivyoripoti ama wengine kuzitetea nchi zao kwa matukio hayo.

Lakini waandishi wa bongo Jezi kuchanika ungesikia TFF jipu kwa kununua jezi za kichina. Mashabiki kupigana ungesikia miafrika ndivyo ilivyo kwa ushamba, kutoelimika, Vurugu nk. Rejeeni mlivyoandika Vurugu za Yanga na Coastal Tanga.Ronaldo kukosa Penati, jibu mnalo mlivyoandika kwa Samatta kukosa Penati na Misri.

Nahitimisha kwa kusema waandishi wetu wa habari za michezo na habari nyingne rudini shuleeee, nyie baaaaaado sana. Kwangu mimi mfumo unaowafanya kuwa waandishi wa habari ndio umekosewa maaana vyuo vingi vinakusanya Failures kuwa waandishi wa habari.

Habari ndiyo hiyo, badilikikeni eboooooooooooooooo!
 
Umesoma magazet yapi??? Au umesoma udaku Wa ulaya??? Maswala ya aibu saana kule ulaya....aibuuuu...unadhan wakiripot kinyume ndio wanajenga???


Ulitaka vurugu za tanga kule waseme hapakuwa na vurugu??? Ulitaka waseme refa alichezesha vzr?? Wakat hajachezesha vema????
 
Upo ki promo zaidi.
Anyway, ni waandishi gani (kwa majina kama ulivyomtaja mmoja hapa) hao wa ulaya unaowazungumzia, ambao walisifu vurugu zilizotokea?
 
Upo ki promo zaidi.
Anyway, ni waandishi gani (kwa majina kama ulivyomtaja mmoja hapa) hao wa ulaya unaowazungumzia, ambao walisifu vurugu zilizotokea?
Hata ikiwa promo, wandishi wetu wa habari mmezidi kuwa vihiyo mnaboa sana. Nimesema rudini shule Elimu haina mwisho!
 
Hivi Shaffi Dauda naye ni mwandishi wa habari au mpiga porojo kama Mbwiga wa mbwiguke? Sasa na Salim Kikeke aitwaje kama Shafi naye ni mtangazaji?
 
Waandishi wa habari na wachambuzi wa habari za michezo ni opportunists tu wanaotegemea matukio ili kukuza umaarufu wao. Kwa mfano Shaffi Dauda bila ya kuikandia Yanga nani atamfuatilia? Yanga ndio fursa ya Dauda ya kuongelewa na kufahamika zaidi,siku akiacha kuiongelea Yanga ndio siku ambayo atapotea ktk medani ya uchambuzi wa habari za michezo.
 
Tatizo waandishi wetu wengi wanakosoa kila kitu bila kutoa suluhisho, kuna wengine wa redio flani wasingekuwa na cha kuongea kama TFF isingekuwepo make ndo story mwanzo mpaka mwisho wa kipindi.
 
Shaffih na Luambano wao ni majungu na kuponda tu! Nammisi sana Maestro na Jeff ktk kipindi cha sports clouds siku hizi, edgar nae kaambikizwa, kaanza kuwa mbea.
 
Shaffii Dauda hata majina ya wachezaji wa ndani na nje anatamka kwa Kilugha.
 
Back
Top Bottom