Shabib laua askari magereza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shabib laua askari magereza

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 8, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 8, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  WATU wawili ambao ni maofisa Magereza wamekufa na mmoja kujeruhiwa katika ajali iliyotokea eneo la Pingo wilayani Bagamoyo ikihusisha magari mawili likiwemo gari dogo mali ya magereza mkoa wa Pwani iliyokuwa inatokea maeneo Wami kuelekea Kibaha.

  Ajali hiyo ilitokea majira ya saa nane mchana baada ya basi la kampuni ya Shabib lenye namba za usajili T388 VNH aina ya Yutong likitokea Dar es Salam kuelekea Dodoma kugongana na gari lenye namba za usajili STJ 1030 Land rover ambalo ni mali ya magereza.

  Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani, Absalom Mwakyoma, ametaja watu waliokufa katika ajali hiyo kuwa ni ASS Inspekta Rajab Lusonge ambaye ni mhasibu wa magereza mkoa wa Pwani na mwingine aliyejulikana kwa jina la Twahil.

  Alisema majeruhi wa ajali hiyo ambaye pia alikuwa kwenye gari dogo ni SSPT Shaibu ambaye hali yake si nzuri na amekimbizwa kupatiwa matibabu ya haraka katika hospitali teule ya Tumbi mjini Kibaha.

  Pamoja na ajali hiyo kuua maofisa wa magereza hakuna abiria wa basi la Shabib aliyepata majeraha isipokuwa wa gari ndogo ambalo ni mali ya magereza lililokuwa na abiria watatu ambao wawili walikufa na mmoja kujeruhiwa vibaya.

  Kamanda Mwakyoma alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana na jeshi hilo linaendelea na uchunguzi kubaini aliyesababisha ajali hiyo na hatua za kisheria kuchukuliwa.
   
 2. M

  Mbavu za Mbwa JF-Expert Member

  #2
  Jan 8, 2011
  Joined: Jan 2, 2011
  Messages: 288
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 45
  Innalillah, wayna ilahy rajiun
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  Jan 8, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mabasi ya hawa wabunge yatatumaliza,limeanza ABO0D hatuja2lia SHABIBY,eh
   
 4. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #4
  Jan 9, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Lahaulla walakwata Ilabill Adhimy. Ina Lillaah waina rajiun.
   
Loading...