Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,933
MTOTO Shabani Maulidi (15) aliyefariki miaka miwili na miezi tisa iliyopita na kufanyiwa matanga, ameonekana akiwa hai baada ya kukutana na mama yake ana kwa ana juzi nje kidogo ya mji wa Geita wakati akienda kwenye shughuli zake za kibiashara. Maulidi alitoweka ghafla na kushindwa kurudi nyumbani kwao Januari Mosi 2011, wakati alipokuwa amepeleka mbuzi machungani na mwili wake kuonekana baada ya siku tatu akiwa amefia kwenye kisima cha maji.
Kwa mujibu wa baba yake, Maulid Shabani, mtoto wake hakurudi nyumbani siku hiyo. Waliendelea kumtafuta bila mafanikio na ndipo baada ya siku tatu walimkuta akiwa amefia ndani ya kisima cha maji kilicho maeneo ya Kijiji cha Nyankumbu, Kitongoji cha Mwembeni. Baba huyo alisema baada ya hapo walitoa taarifa polisi kisha waliruhusiwa kuuchukua mwili wa mtoto wao na kwenda kuuzika katika Kitongoji cha 14 Kambarage ndani ya mji wa Geita. Alisema kuwa walifanya shughuli zote za matanga na wakajua tayari mtoto wao ameishafariki, kwamba hawakuwa na wazo lolote la kumpata akiwa hai tena kama ilivyotokea. Shabani aliongeza kuwa tukio hilo ni la kustaajabisha kwake.
Naye mama mzazi wa mtoto huyo, Aziza Ramadhani akisimulia namna alivyokutana na mtoto wake, alisema kuwa alikuwa akienda kwenye shughuli zake za ujasiriamali, ndipo akakutana naye eneo la Nyankumbu nje kidogo ya mji wa Geita. Alisema kuwa alipomuona alimwita kwa jina lake akisema mwanagu Shabani ni wewe, naye akamwitikia akiema ni mimi, kisha akamshika mkono huku akiwa haamini macho yake.
Nilimpigia simu mume wangu, akaja tukamchunguza vizuri na kubaini kuwa ni yeye Shabani aliyesadikiwa kuwa alifariki na kuzikwa, alisema mama huyo.
Aliongeza kuwa mtoto huyo alikuwa na alama ya kinundu kwenye paji la uso na mguuni akiwa na alama ya kovu iliyosababishwa na kuchomwa na mwiba. Pia alikuwa na mwanya kwenye meno uliofanana na wa baba yake. Mtoto huyo aliyevuta hisia za watu wengi mjini Geita, ameendelea kuthibitishwa na walimu wake wa Shule ya Msingi Mwatulole pamoja na wanafunzi aliokuwa anasoma nao darasa la tano kabla ya kifo hicho cha utata.
Akizungumza na gazeti hili, makamu mkuu wa Shule ya Msingi Mwatulole, Joseph Nungula aliyekuwa akifuatilia kwa karibu tukio hilo, alisema kweli mtoto huyo anaonekana ni yeye bila kutiliwa shaka yoyote. Mwalimu huyo alisema kuwa alimtambua mtoto huyo kwa sura na alama, hasa ya usoni huku akimwelezea kuwa alikuwa na mahudhurio mazuri shuleni. Pia maendeleo yake kitaaluma yalikuwa mazuri.
Mtoto huyo ambaye anaendelea kupewa huduma ya kitabibu katika Hospitali ya Wilaya ya Geita kwa uchunguzi zaidi wa kiafya, anaongea kwa shida wanapokuwepo watu wengi. Hata hivyo, amewatambua baba na mama yake na kila wanapomuuliza maswali anawajibu.
Jeshi la Polisi mkoani hapa limethibitisha kutokea kwa tukio hilo, huku likiahidi kuendelea kutoa habari zaidi wakati huu ambapo wananchi wanasubiri kibali cha jeshi hilo kwa ajili ya kufukua kaburi alilokuwa amezikwa mtoto huyo.
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida kaburi ambalo alizikwa mtoto Shabani Maulidi (15), ambaye anadaiwa kufariki dunia miaka mitatu iliyopita na kuonekana akiwa hai hivi karibuni, jana lilifukuliwa na viungo vya mwili wake kukutwa ndani.
Kazi hiyo iliyofanyika chini ya ulinzi mkali wa polisi pamoja na Mtafiti wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Mkoa wa Mwanza, Lucas Ndungulu, ilizua taharuki kwa umati wa watu waliokuwa eneo hilo, baada ya nyumba ya jirani lilipo kaburi hilo, Masanja Marwa, kubomoka ghafla wakati ufukuaji huo ukiendelea, huku mwanamke mmoja ambaye hakufahamika jina lake mara moja naye akianguka na kuzirai.
Kwa sasa mtoto huyo ambaye alionekana hai, amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Geita kwa uangalizi wa kitaalamu.
Akizungumza na waandishi wa habari eneo la tukio, Ndungulu alisema kuwa wameamua kufukua kaburi hilo ili kupata sehemu ya viungo vya mwili kwa ajili ya vipimo.
Lengo la kufukua kaburi hili ni kutaka tupate kiungo chochote cha mwili wa marehemu ili tufanye utafiti wa kitaalamu ili tujue kama ni kweli huyu anayedaiwa kuwa ni mtoto wao ndiye, alisema.
Alisema kuwa ufukuaji huo umemalizika na kwamba wamepata baadhi ya viungo vya mwili wa marehemu na kuchukua baadhi ya mifupa ya mapaja yote mawili ambayo itapelekwa katika hospitali ya rufaa kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Kwa mujibu wa Ndugulu, majibu ya vipimo hivyo yatatolewa baada ya wiki mbili kama hakutakuwa na tatizo lolote la kukatika kwa umeme.
Naye Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Geita, Adamu Sijaona, alisema kuwa pamoja na kuchukua viungo hivyo, pia watachukua damu ya wazazi na mtoto mwenyewe.
Tumechukua pia damu ya mama na baba wa Maulidi mwenyewe ili tukapime vinasaba (DNA) na kama alivyosema mtafiti, majibu yatatoka baada ya wiki mbili, alisema.
Akizungumza baada ya kazi ya ufukuaji kumalizika, baba mzazi wa mtoto huyo, Maulidi Shabani, alisema kuwa endapo majibu yatakuja tofauti au vile wanavyokusudia, wapo tayari kuyapokea na kwamba ikigundulika huyo aliyeonekana ni Maulidi, pia watampokea na kuendelea kumtunza.
Lakini nina imani kuwa huyu aliyeonekana ni mwanangu Maulidi kabisa, kwa sababu anazo alama zote, alisema mzazi huyo.
Mtoto Maulidi aliyefariki dunia miaka mitatu iliyopita na kufanyiwa matanga, alionekana akiwa hai baada ya kukutana na mama yake ana kwa ana mapema wiki hii asubuhi wakati akienda kwenye shughuli zake za biashara.
Ilidaiwa na wazazi wake kuwa Maulidi alitoweka ghafla na kushindwa kurudi nyumbani kwao Januari mosi 2011, wakati alipokuwa amewapeleka mbuzi malishoni na mwili wake kuonekana baada ya siku tatu akiwa amefia kwenye kisima cha maji.
Kwa mujibu wa baba yake, Maulidi hakurudi nyumbani siku hiyo, ambapo waliendelea kumtafuta bila mafanikio na ndipo baada ya siku tatu walimkuta akiwa amefia ndani ya kisima cha maji kilicho maeneo ya Kijiji cha Nyankumbu, Kitongoji cha Mwembeni.
Tukio hili ni la tatu kutokea mkoani hapa ambapo wilayani Kasamwa, mwanamke aliyefariki dunia miaka mitano iliyopita alionekana hai na kutambuliwa na ndugu yake. Tukio la pili lilitokea Wilaya ya Chato, wakati kijana aliyefariki dunia miaka miwili iliyopita alionekana akiwa hai.

:A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1:
Update
Kaburi la aliyefufuka lafukuliwa
VIUNGO VYAKE VYAKUTWA NDANI, UCHUNGUZI WAANZAUpdate