samakiurembo
JF-Expert Member
- Dec 8, 2021
- 445
- 684
Habari za usiku huu wanaJamiiForums natumai wote ni wazima wa afya.
Bila kupoteza muda ningependa kwenda moja kwa moja kwenye hoja ya msing juu ya ujenzi wa reli ya kisasa iliyojengwa na serikali yetu tukufu .
Ujenzi una nia njema kabisa nasi tunapongeza kama wananchi ila changamoto umekuja kutenganisha miundombinu ya kibiashara kijamii kielimu na muingiliano wa kila siku wa watu
Ujenzi wa reli hii umeenda kutenga watu waliokuwa wanaingiliana kila siku katika maeneo hayo niliyotajwa hivyo imepelekea usumbufu kero na kuongezeka kwa gharama kusiko kwa lazima
Makundi yanayoathirika ni
Wafanyabiashara baadhi ya maeneo yaliyotengwa kama masoko au maduka yalikuwa sehemu muhimu ya watu kupata mahitaji yao lakini reli imeenda kuweka uzio na umbali mrefu kulifikia soko au duka hiki ni kilio kikubwa cha wananchi
Kundi la pili watoto wadogo wa shule na wakina mama ambao wanalazimika kwenda umbali mrefu ili kufuata kivuko kilichotengwa kwa mfano eneo la Banana Ukonga Dar es Salaam watoto wadogo inawalazimu watembee umbali mrefu mpaka Majumba Sita na kurudi tena Banana ili wafike shuleni na ni eneo lenye shule zaidi ya sita na zipo eneo la jeshi na wengi wa wanafunzi wanatokea upande uliozibwa wa raia.
Ndani ya week mbili baada ya njia za muda mrefu kufungwa maduka yameanza kufungwa kwa kukosa wateja gharama usafiri zimepanda kwani kwenda kununua dawa ya kikohozi itakulazimu ujumlishe na elfu mbili ya pikpiki
Lengo la kuandika uzi huu ni kujaribu kupata nafasi ya kuwafikia wahusika kwa urahisi kwa JamiiForums ni mtandao mkubwa unaosomwa na wengi
Mapendekezo kuwe na route ya gari kuanzia Pugu kupitia upande wa pili wa reli Hadi Banana ama kuwe na vivuko kama cha Buguruni au Manzese kwa wapita kwa miguu au kuwe na geti kwa raia kupita kwa muda fulani tu kisha geti kufungwa maana wanaoteseka ni wakina mama wanaenda masokoni kuanzia usiku na watoto wanaowahi mashuleni alfajiri.
Nb kilio ni kikubwa wananchi wanateseka