Sezibera kumrithi Mwapachu EAC

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Sezibera kumrithi Mwapachu EAC

Imeandikwa na James Gashumba wa EANA; Tarehe: 18th April 2011 @ 23:50 Imesomwa na watu: 172; Jumla ya maoni: 0








WAZIRI wa Afya wa Rwanda, Dk Richard Sezibera, ndiye anayetajwa kurithi nafasi ya Balozi Juma Mwapachu wa Tanzania ambaye ni Katibu Mkuu Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) anayemaliza muda wake.

Kama jina lake litapitishwa na viongozi wa EAC leo Dar es Salaam, atakuwa Katibu Mkuu wa nne tangu EAC kufufuliwa mwaka 1999.


Katibu Mkuu wa kwanza wa EAC yenye wanachama watano sasa, alikuwa ni Mkenya Francis Muthaura (1999-2001) na kufuatiwa na Amanya Mushega wa Uganda (2001-2006) ambaye naye alirithiwa na Balozi Mwapachu.


Awali wakati EAC ikifufuliwa, ilikuwa na wanachama watatu; Kenya, Uganda na Tanzania. Mataifa ya Rwanda na Burundi (ambayo yanafanya EAC kuwa na wanachama watano sasa)

yalijiunga baadaye mwaka 2007.

Habari za kuaminika zilizoifikia Shirika Huru la Habari la Afrika Mashariki (EANA), mjini

Kigali, zinasema jina la Dk. Sezibera limepelekwa katika mkutano wa maraisi wa EAC unaoendelea Dar es Salaam.

Mkutano huo ndio utakaothibitisha mrithi wa Balozi Mwapachu. Dk Sezibera aliteuliwa kuwa Waziri wa Afya wa Rwanda Oktoba 2008.


Kabla ya kuteuliwa kuwa waziri pia aliwahi kushika nafasi kadhaa za uongozi katika Serikali ya Rwanda.


Nafasi hizo ni pamoja na Balozi wa Rwanda nchini Marekani; Balozi Maalumu wa Rwanda kwa nchi za Maziwa Makuu; na Mshauri Mwandamizi wa Rais anayeshughulikia masuala ya amani na usalama, menejimenti ya migogoro na masuala ya ushirikiano ya kikanda.


Pia amechapisha majarida mengi ya chuo kikuu hasa katika masuala ya siasa na uhusiano wa kimataifa; ameandika makala kadhaa kwa ajili ya mashirika ya habari ya kitaifa, kimataifa na ya kikanda likiwamo The Washington Post la Marekani, jarida la Foreign Affairs, televisheni ya Marekani ya CNN, Shirika la Utangazaji la Marekani-VOA, na Shirika la Utangazaji la Uingereza -BBC.


Dk. Sezibera ana Shahada ya Dawa na Upasuaji na amefanya kazi kwa miaka mingi Uganda na Rwanda. Pia ana Shahada ya Sanaa ya Chuo Kikuu cha Georgetown.


Vyanzo vya habari pia vinasema Tanzania imependekeza jina la Dk Enos Bukuku ambaye kwa sasa ni Naibu Gavana wa Kwanza wa Benki Kuu kwa nafasi ya Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia mipango na miundombinu.


Nafasi hiyo ilikuwa inashikiliwa na Alloys Mutabingwa ambaye analazimika kuachia kutokana na makubaliano ya nchi wanachama kwamba Rwanda ndiyo itoe Katibu Mkuu wa EAC.


Dk Bukuku amepata kushika nafasi kadhaa katika serikali ya Tanzania zikiwamo za Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais anayeshughulikia Mipango na Ubinafsishaji na mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).


EAC ilifufuliwa mwaka 1999 wakati nchi tatu za awali za Kenya, Uganda na Tanzania zilipotia saini ya kuanza upya ushirikiano wa EAC kwa lengo la kukuza biashara na uwekezaji ukanda wa Afrika Mashariki.


Jumuiya ya zamani ilikufa mwaka 1977 kwa sababu za tofauti za kisiasa na kiuchumi miongoni mwa nchi wanachama.


 
safi sana! we want young men to steer our region ahead! hongera ndugu Sezibera.
 
May on behalf of JF members, I wish Dr. Richard Sezibera success in his new challenges.......................
 
Jameni this time hawajampata tu mwanamama? Ktk makatibu wote wakuu waliopita wote madume..je hakuna akina mama wanaoweza?
 
Back
Top Bottom