Seriously nimekata tamaa ya maisha.

Seriously nimekata tamaa ya maisha.

Mkumbuke AYUBU mkuu baada ya kupitia yote aliendelea kumwamini MUNGU. Mkuu hayo ni mapito kila unalopitia jipe moyo kwamba ipo siku utasimama na kuwa ngangari zaidi ya mara ya kwanza....
 
Anything happen its happen for a reason,sasa hivi huwezi kuijua hiyo reason,but na hakika Mungu amekuandalia lililojema na mafanikio zaidi..sometime Mungu anatuondoa tulipo ili kutupeleka sehemu ya juu zaidi.unachotakiwa ni kuamini na kumuomba yeye aliejuu.kukata tamaa ni dhambi.usimkaribishe shetani kamwe.
 
siku izi watu wanaacha kazi wanafanya ishu zao we kama wamekutimua ulitakiwa ufurahi na uende kwa plan b.
 
Jipe moyo mkuu. Mungu ni mwaminifu juu ya maisha yetu na siku zote huwa anatuwazia mema. Unachopaswa kufanya kwa sasa ni kumkabidhi Yesu maisha yako na kila kitu kitanyooka kama awali. Huna haja ya kukata tamaa. Kukata tamaa ni roho ya ibilisi.
 
NiPM nikupe ushauri wa kitaalamu kuhusiana na sheria za kazi. Usiwe mtu wa kukata tamaa bali mpambanaji hadi dakika ya mwisho.
 
Rafiki yako mpweke na.wewe sasa umeachishwa kazi!!!!!!!!

Poleni sana ila fuata ushauri hapo juu upewe utaratibu wa kisheria
 
pole kwa kipindi kigumu usikate tamaa pambana mungu atakusaidia kupata ajira/kujiajiri...unaweza kuwashitaki kukufukuza kazi bila kosa
 
Maandiko matakatifu yanasema hivi niite nami nataitika na nitakuonyesha makubwa usilolijua.
 
Pambana kiume, Mungu hamtupi mja wake
 
pole sana ndugu, usikate tama endelea kutafuta nyingine. MLANGO MMOJA UKIFUNGWA MWINGINE HUFUNGULIWA
 
Usikate tamaa ndugu yangu ukikata tamaa unampa shetani utukufu unachotakiwa sasa ni kumuomba Mungu atakupa kazi nzuri zaidi ya hiyo biblia inasema kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana akiomba kwa bidii na katika Isaya60:11 biblia inasema malango yako hayatafungwa yatakuwa wazi daima usikate tamaa kabisa better days are coming
 
Yaani kwa kuachishwa kazi tu unajiuliza umemkosea nini Mungu?! Kwani ulipopata hiyo hiyo kazi ulimfurahisha nini Mungu?! Tatizo halipo kwenye kuachishwa kazi ila lipo kwenye namna unavyoona kuwa na kazi ni kila kitu katika maisha yako. Nakupa ushauri tu wengu wamepitia njia hiyo, wengine hawakuachishwa bali kampuni ilifilisika au kwa sababu ya ajali walipoteza uwezo wa kufanya kazi, hawakukata tamaa. Kama uliipata hiyo basi jipe moyo kuwa utapata nyingine kijana.Pole sana ila usifanye kosa la kukata tamaa. Mungu akubariki unapojipanga kwa ajira nyingine. Mimi naamini Mungu ana njia elfu katika kukupatia ufumbuzi.
 
habari za jioni wanajamvi.naombeni maombi yenu nimeachishwa kazi bila kosa, yaani nimekata tamaa na maisha,ukizingatia ilivyo kazi kupata kazi,najiuliza cjui nimemkosea nini mungu,najiona sina bahati katika dunia hii.
WanduguWeeee! hiyo ni pindo tu na siyo mwisho !! " its only a Bend and not an End " weka imani kuwa mambo mazuri yaja kwa wingi hivi karibuni/mustakabali. ubarikiwe
 
habari za jioni wanajamvi.naombeni maombi yenu nimeachishwa kazi bila kosa, yaani nimekata tamaa na maisha,ukizingatia ilivyo kazi kupata kazi,najiuliza cjui nimemkosea nini mungu,najiona sina bahati katika dunia hii.

Mwaka 2004 niliachishwa kazi bila sababu ya msingi na wale waajiri wangu pale New Afrika hoteli..niliwaza mengi lakini at last nilichukua ile experience kama challenge,Mungu ana mipango ktk kila kitu,nilikaa kijiweni kwa mwezi na kitu,siku niliamka nikaenda internet cafe nikafanya application kwenye hoteli moja maarufu duniani(Burj al Arab-Dubai)bila usumbufu waliniita!!mkataba ulikuwa mzuri sana salary ya mwezi ilikuwa almost mara tatu niliyokuwa napata pale New Afrika hoteli.Nilipokwenda Tz likizo wa kwanza kumtafuta alikuwa HR DIRECTOR wa New Afrika maana alinifungulia mlango aliponiachisha kazi pale NA..Niliowaacha pale bado wana life ya kuungaunga tu!!!hivyo chukulia hiyo kama challenge
 
Leo ndo nimejua...! Kumbe jf kuna watu wazuri. Mi nilijua ni kejeli na matusi tu. Nimefurahi sana the way wachangiaji walivyo mtia moyo kijana.
 
Mwaka 2004 niliachishwa kazi bila sababu ya msingi na wale waajiri wangu pale New Afrika hoteli..niliwaza mengi lakini at last nilichukua ile experience kama challenge,Mungu ana mipango ktk kila kitu,nilikaa kijiweni kwa mwezi na kitu,siku niliamka nikaenda internet cafe nikafanya application kwenye hoteli moja maarufu duniani(Burj al Arab-Dubai)bila usumbufu waliniita!!mkataba ulikuwa mzuri sana salary ya mwezi ilikuwa almost mara tatu niliyokuwa napata pale New Afrika hoteli.Nilipokwenda Tz likizo wa kwanza kumtafuta alikuwa HR DIRECTOR wa New Afrika maana alinifungulia mlango aliponiachisha kazi pale NA..Niliowaacha pale bado wana life ya kuungaunga tu!!!hivyo chukulia hiyo kama challenge

ushauri mzuri ie kila kitu kinatokea kwa sababu!
 
Kila tukio lina sababu yake na huenda kwa kuachishwa kwako kazi mungu akawa amekuandalia sehemu nyingine nzuri hivyo usikate tamaa maisha yapo na utatoboa tu kama ukiamini inawezekana kwani wote walioweza maisha walianza na sifuri mpaka leo hii wanamilki vitu vya thamani, chukulia kama changamoto ya kuweza kufikiri zaidi nini cha kufanya na ndio maana kwa upande wangu nikimuona mtu amefanikiwa alafu anatoa ushuhuda kwamba alinyanyasika na ndugu yake ambae alikuwa anamlaza jikoni tena chini huwa inanisikitisha sana maana wakati mwingine yale masimango ndio ilikuwa chachu ya yeye kufanikiwa hivyo hata kuacha kwako kazi ni sehemu pia ya kutafuta sehemu nyingine nzuri zaidi pia ni kukumbusha kwamba kwenye maisha lolot laweza tokea hivyo ni kujiandaa. Usikate tamaa fuatilia NSSF zako huku ukisoma ramani zaidi
 
Back
Top Bottom