Kwahapo naona itakuwa ngumu saana kupata mtu, Kama tayari ulikuwa na sehemu i mean duka tayari ingekuwa rahisi, nani atakubali kukupa pesa za kulipia pango, then na mali?. Kama una nyumba itumie kama collateral kukopa kwenye ma bank, prefarably NMB, Akiba, Access Bank.
Nakushauri kama unataka biashara itoboe mapema, ni vema ukaenda kwenye hizi wilaya mpya kama KILINDI nk, kuna miradi mingi saana ya ujenzi inaendelea, lazima utapata soko la bidhaa zako.
Otherwise kusanya kwanza kamtaji ndugu, idea na uzoefu kila mtu anao,kumbuka hata mabank hawatoi mkopo wa kuanzisha biashara wanatoa mikopo kwa ajili ya biashara ambayo tayari umeshaanzisha
Kila la kheri