Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,214
- 3,587
Uncle wangu aliyekuwa Afisa Mwandamizi EAC walimtengenezea cheti feki cha kifo na wakakomba mafao yake na pensheni zote 100%.
Siku alipozuka kuzichukuwa mwaka 2012 baada ya Mahakama ya Tanzania kuamuru walipwe, wale staffs wa huduma kwa mteja baada ya kuangalia kwenye mfumo wa tarakilishi (computer) wakapiga ukunga/yowe/nduru kuwaita staffs wenzao eti wamezukiwa na mzimu.
Walipofika staffs hao na kuuliza mzimu upi, wakamwonyesha huyo hapo (yaani uncle wangu).
Uncle alipouliza ni kwa vipi wamnyanyapae kiwango hicho kwa kumuita mzimu wakati amekuja kudai haki zake?
Wakasema mfumo unaonyesha wewe ni marehemu tangu mwaka 1985 na kivuli cha cheti cha kifo hiki hapa kwenye tarakilishi na mafao uliishachukuwa ushahidi huu hapa na mwenzi wako alichukuwa nusu pensheni hadi 1986.
Wale staffs walioitwa kushuhudia mzimu wakayeyuka, uncle puuuuu.... chini, pepewa pepewa pale na walinzi, fahamu ziliporudi akaacha laana ya karne (kama serikali inalaanika sijui!?) na kuondoka hapo Hazina Makao Makuu hadi leo yuko hai Kijijini kama EL kule Peninsular; na akasusa kabisa kurudi Hazina.
Aina hii ya watumishi ndiyo wamejaa serikalini na ndiyo watafanya models kama za akina Makonda zisiishe nchi hii, zitakuja na kutoweka na kurudi tena na kutoweka tena na kurudi...
Yaliyopita si ndwele...