Serikali za afrika zamgwaya Rais Bashir | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali za afrika zamgwaya Rais Bashir

Discussion in 'International Forum' started by fiksiman, Jul 15, 2009.

 1. fiksiman

  fiksiman JF-Expert Member

  #1
  Jul 15, 2009
  Joined: May 17, 2008
  Messages: 402
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Ndio hadi sasa serikali kadhaa zikiwemo za Afrika Mashariki (Tanzania na Uganda) pamoja na Afrika Kusini zimeonyesha kumgwaya Rais wa Sudan Omar Ali Bashir ambaye anatuhumiwa na mahakama kuu ya kimataifa kwa uhalifu dhidi ya binadamu nchini mwake. Akijibu swali la Mbunge wa Viti maalum kutoka Chadema, Mhe. Halima Mdee, naibu waziri wa mambo ya nje, aliweka wazi kuwa Serikali ya Tanzania haitamkamata Rais huyo wa sudan endapo atakuja nchini.

  Pia Waziri mmoja pale Uganda aligoma kujibu swali kutoka kwa mwandishi wa BBC swahili alipotaka kujua kama Serikali ya Uganda itamkamata Bashir kama ataingia nchini humo. Waziri huyo alimtupia Mwanasheria Mkuu wa Serikali akidai yeye ndo mwenye wajibu wa kuamua. Hata hivyo baadae aliwaomba waandishi wasubiri mpaka atapofika ndipo itajulikana kama atakamatwa au laa. Uganda ni miongoni mwa mwanachama katika Baraza la Amani la Umoja wa Mataifa.

  Afrika kusini nayo ilionuyesha kumgwaya Rais huyo baada ya kumwalika kwenye shughuli za Kuapishwa kwa Rais Jacob Zuma na baadae kumshauri asihudhurie hafla hiyo ili kuepusha mgongana na jumuya ya kimataifa. Yote tisa, kumi ni pale Umoja wa Afrika ulipotoa tamko la kugoma kushirikiana na Mahakama hiyo katika suala la kumkamata Rais huyo kwa kigezo cha kudai kuwa mara nyingi nchi za Afrika hazipewi kipaumbele katika masuala yao hivyo hawaoni kwanini watoe ushirikiano inapotokea wengine wanawahitaji.

  Pamoja na masuala yote hakuna kiongozi hata mmoja aliyesimama na kukanusha tuhuma alizipewa Rais Bashir ingawa wameonekana kumkingia kifua kama walivyofanya kwa Komredi Mugabe. Je hii inatoa tafsiri gani kwa wachambuzi wa masuala ya siasa za Afrika?
   
 2. B

  Bull JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2009
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hi ni Kanagaroo Court, Blair, Bush, nk, wameuwa watu wengi zaidi ya Bashir na wao watashitakiwa na nani? Hongera African leaders na Tribunal body!!

  Endelea:
  Prosecutors at the International Criminal Court (ICC) have appealed against a decision by the body's tribunal not to charge Omar al-Bashir, Sudan's president, with conducting genocide.

  He said there was insufficient evidence to prove he was also guilty of waging genocide there, "We believe it's a mistake. He told Al Jazeera:

  Leaders of the African Union said on Friday they would no longer co-operate with the ICC and would not arrest and extradite the Sudanese president.

  Source; aljazeera
   
Loading...