Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,253
- 44,595
Tafadhali naomba nielimishwe yafuatayo:Kiev: Wanafunzi bado wapo Ubalozini hawaendi popote na wako tayari kukaa hapo weekend nzima. Kwa mujibu wa Afisa wa ngazi za juu za ubalozi huo niliyezungumza naye, wao hawana matatizo na vijana kuwa hapo kwani wameomba hiyo hifadhi.
Dar-es-Salaam: Ubalozi wa Uingereza Ukraine umekuwa na mawasiliano na Ubalozi wao Tanzania ambao kutwa nzima ya leo wamekuwa wakiwasiliana na viongozi wa serikali ya Tanzania kwani hili la wanafunzi kupiga kambi ubalozini limeishtua serikali.
Michango:
Kuna mtu ameshauri kutumia paypal account ya KLH News, hata hivyo nimecheki na Paypal inahitaji niwe na account nao angalau siku 60 kabla hatujaweza kutoa fedha kwenye account hiyo, na hadi leo tuna siku 51!!
Kwa ushauri wa Afisa huyo njia pekee ya kuwafikishia misaada vijana hao kwa haraka ni kupitia Western Union. Nimezungumza na vijana wote na wao wamekubali kutumia jina la mtu mmoja. Ninachotaka kufanya ni kutumia mtindo wa collective check and balance.
: Jina analotumiwa ni la mmoja
: Swali la usalama (anapewa mwingine)
: Jibu anapewa mwingine
: Wale wanaotaka kutuma wawasiliane na mimi nitawapa jina, swali na jibu. Wakishatuma waconfirm na mimi. Na mimi sitawaambia Kiev zilizotumwa hadi baadaye jioni ya leo au kesho asubuhi (nikijumlisha).
I'm open for any other suggestions, lakini tusipoteze muda kukosoa tu tuje na suluhisho linalowezekana kwani kule ni jioni ni giza linaingia...
Hivyo wanafunzi angalau watatu wanashiriki katika kuzichukua fedha hizo: That is the best I can come up with right now.
Nimekuelewa na ahsante kwa maelezo yako.KNKCU,
a. Lengo la wao kwenda hapo ni kutaka attention ya Taifa lao na viongozi wao. Kwa vile hatuna Ubalozi Ukraine, taratibu zinawataka wajisalimishe kwa nchi ya Jumuiya ya Madola.. na Uingereza ndio mama yao. Hawakwenda kuomba ukimbizi.
b. Ubalozi umekubali kuwasikiliza na kuwaacha wakae hapo kwenye uwanja wa Ubalozi. Hadi hivi sasa ubalozi haujatoa chochote zaidi ya kujaribu kuwasiliana na Tanzania na Ubalozi wa UK Tanzania. Ubalozi ulishatoa ofa kwa serikali ya Tanzania kuwa wawaruhusu wao Ubalozi watoe fedha za matumizi n.k kwa vijana kwa ahadi kwamba serikali ya TZ itairudishia Uingereza pesa hizo, serikali yetu imekataa (haikutoa jibu). So Ubalozi wa Uingereza hauna lolote lile la kufanya.
c. Michango kwa sasa inawalenga wale waliopiga kambi hapo Ubalozini 20 hivi siyo wote 29 wapo hapo wengine wanaangalia vitu huko vyuoni walikowaacha. Hivyo michango hii ya matumizi na kujikimu hadi serikali itakapotatua tatizo hilo ni kwa wale waliopiga kambi hapo. Hawaondoki Ubalozini hapo..! Hivyo ni kuhakikisha wanapata chakula, na mablanketi n.k..
d. Nimeshawaambia wanafunzi wote kwa pamoja (kutumia spika za simu) na kuzungumza nao mmoja mmoja kuwa tunajaribu kuwasaidia na nimewaeleza mpango wazi, so siyo mtu mmoja mwenye ujuzi wa michango hii. Na ndio maana badala ya kutuma mtu mmoja mmoja nataka nijue ni kiasi gani kimetumwa na nitakapowaambia waende kuchukua basi nitawaambia kwa pamoja (na kurekodi naweza kuwarekodi)!
Nahitaji msaada wako naomba uangalie kisanduku chako!No problem