Serikali yawasimamisha viongozi 5 waandamizi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)

Waungwana
Safisha safisha NHC imeendelea ili kuliwezesha kuanza upya...

Baada ya MD Mr Mchechu kusimamishwa, Serikali kupitia Bodi ya Shirika imewasimamisha Viongozi 5 waandamizi wa Shirika hilo....

Vyombo vya Dola vinaendelea na kazi zao...

Taarifa zaidi zinafuata.....

cc: BAK barafu
Hata wakati muhongo anatimuliwa tulishangilia hivi hivi, lakini linalotufika leo kila mmoja analia kivyake. Tusiingize siasa kwenye utaalamu
 
Funga majizi hayo, hakuna kuangalia usoni.
Kwenye Hilo lidubwana RUSHWA imeanzia kwa MKURUGENZI mkuu mpaka mfyagiaji, kama vp timua wote vijana wetu wa vyuo wapo mitaani wanataka hivyo vibarua.
 
Yetu macho na tunaomba Mungu atupe maisha marefu tuone uongozi mpya wa NHC utakavyoanza kudidimiza kila kitu alichobuni na kukifanya Mchechu. Leo Mchechu ametolewa kwa sababu ameteuliwa ila angekuwa dokta bingwa mfano wa moyo, figo etc. asingewezwa kutolewa kwa sababu professional yake ndo inamfanya bingwa na sio uteuzi. Akina Professor Janabi kama siyo kuwa pale kwa professional yake pia naye angetolewa kisiasa ikibainika tu hapokei kila kitu kinachosemwa na wanaojiona wakubwa. Naishauri serikali iangalie athari za maamuzi kabla ya kumtoa mtu kwenye nafasi
Tatizo Wabongo mna mahaba ya kipuuzi sana.

Mimi sina tatizo wala chuki na Mchechu ila karma is really, huyo Mchechu yupo kwenye bodi ya Dawasco kuna dogo alimuonea akamfukuza kazi sasa na yeye afeel the same pain siyo kuja kutetea ujinga ujinga hapa au kwa sababu wengine hawana sauti za kusikika? Kwanza wewe unajuwa Mchechu yupo kwenye bodi ngapi?
 
Tatizo Wabongo mna mahaba ya kipuuzi sana.

Mimi sina tatizo wala chuki na Mchechu ila karma is really, huyo Mchechu yupo kwenye bodi ya Dawasco kuna dogo alimuonea akamfukuza kazi sasa na yeye afeel the same pain siyo kuja kutetea ujinga ujinga hapa au kwa sababu wengine hawana sauti za kusikika? Kwanza wewe unajuwa Mchechu yupo kwenye bodi ngapi?
Nakuunga mkono...[HASHTAG]#matola[/HASHTAG]


OvA
 
Felcechemi Mramba alitolewa TANESCO kwa sababu ya kumweka mtu smart zaidi; je kumwondoa kumeleta tofauti yoyote chini ya uongozi mpya. Ifike mahali tufanye tahmini ya mabadiliko tuangalie mabadiliko versus improvement baada ya kumbadili mtu.
Tupo Watanzania millioni 50, watangaze nafasi na sifa za mkurugenzi uone kama hakuna Watanzania wenye sifa hiyo.

Msilete mambo ya kijinga kisa mnanunuliwa bia mitaani huko, kama una huruma naye andaa makarasi ya dhamana ukajaribu bahati yako kumuombea dhamana, lakini dalili zote zinaonesha huyu lazima akunje nondo hakuna dhamana.
 
kwa Docta Ramadhan Dau mbona haya hamkuyasema!?
acha unafiki
Yapi?tafsiri yako ya unafiki ni ipi?Unaweza kutafuta maandishi yangu humu JF na ukani-quote kuona nilisema nini kwa mjadala wa Dr Dau?Jf hutunza kumbukumbu
 
walikuwepo tena vikao DUBAI!! Na jaribu kutafiti inawezekana kila zilipojengwa nyumba nao wana nyumba hapo!! TZ yetu ya vi wonder.
Hujakosea. Wanazo Apartments na frem za biashara. Ndo chanzo cha kodi kupanda kwa 300% kitu kilichopelekea mfumuko wa bei ya sukari na vitu vingine. Ijulikane kuwa washika biashara wetu ni wapangaji wa makazi, maofisi na maduka wa Nhc. Huku mchechu akishauriwa na Hamad kushinikiza wapangaji kulipia huduma za maji, umeme, walinzi na wafanya usafi kwa US Dollar, kwa wasimamizi wa majengo ambao ni watanzani wenye asili ya asia. Huku wakiwatishia wapangaji kufukuzwa iwapo wangelikataa
 
Tupo Watanzania millioni 50, watangaze nafasi na sifa za mkurugenzi uone kama hakuna Watanzania wenye sifa hiyo.

Msilete mambo ya kijinga kisa mnanunuliwa bia mitaani huko, kama una huruma naye andaa makarasi ya dhamana ukajaribu bahati yako kumuombea dhamana, lakini dalili zote zinaonesha huyu lazima akunje nondo hakuna dhamana.
Umemjibu vizuri. Utendaji kazi mzuri usiendane na wizi. Akatumie pesa aliyopewa. Magufuli fanya kazi.
 
Tupo Watanzania millioni 50, watangaze nafasi na sifa za mkurugenzi uone kama hakuna Watanzania wenye sifa hiyo.

Msilete mambo ya kijinga kisa mnanunuliwa bia mitaani huko, kama una huruma naye andaa makarasi ya dhamana ukajaribu bahati yako kumuombea dhamana, lakini dalili zote zinaonesha huyu lazima akunje nondo hakuna dhamana.
Watanzania ndomana viongozi wanatuitaga Wapumbav na malofa,utawaskia oh jamaa his smart sjui intelligent Sijui Mara kichwa,kumbe mwisho wa siku hao hao wanatupiga
Kuna mijitu ya hivyo kabisa,nimeamini usemi wako hao jamaa huwa wanawanunulia bia ndomana kuna watu wanaishia kuwasifia tu

Ova
 
Ila tuacheni majungu Mchechu na timu yake wameitoa NHC ICU... Shirika lilikuwa na majengo mazee yaliyorithiwa enzi za mkoloni mpaka leo shirika linamiliki maghorofa ambayo hata kwenye baadhi ya nchi za Ulaya hawana, hiyo ni hatua kubwa sana. Mengine hayo ni human elements tu...
So far shirika la NHC now liko katika peak in terms of operations and total assets than at any other time in its histrory... Serikali iache kufrustrate watendaji wake kitu kinachochangia kushusha morale ya kazi na kudumaza ubunifu katika taasisi za uma. Kama wamemchoka Mchechu wamwamishie kwingine sio kumzushia makesi ya uongo uongo.
NHC ilikuwa haiwezi hata kununua kopo la rangi na kupaka majengo yake. Hivi sasa huwezi kuta jengo la NHC lina rangi za mwaka sabini. Majengo yake yote yako painted huku shirika likiendelea na ujenzi wa miradi mipya kadhaa. Haya mambo hayajawahi kufanywa na kiongozi yeyote wa NHC tangu nchi hii ipate uhuru. Hawa wanaothubutu leo hii ndio wanakuwa frustrated na kuchafuliwa kwa mambo yasiyo na tija. Mtu anapokuja na shutuma kuwa Mchechu kaipa tenda kampuni yake, Je mchechu ana hisa kwenye kampuni ya Estim au CRJE ambazo ndizo kampuni zinazotekeleza miradi mikubwa ya NHC?
Mimi naamini kwenye rizki siku zote hakukosi fitina na majungu. Na hii ni sehemu ya watu wenye njaa ambao wanatolea macho nafasi za hilo shirika ili nao wakachume na mwisho wa siku kuliua kabisa shirika au kulirudisha ICU... Otherwise tuhuma hizi ni majungu kama majungu menginewe yasio ya tija kwa shirika la NHC.
Waafrika ndiyo tulivyo ........... hatupendi mafanikio ya watu!! Kila siku lazima atafutwe mchawi tu kwa matatizo au mafanikio ya mtu!!

Nakumbuka enzi tukiwa wadogo, nilikuwa nasikia story za matajiri wengi hasa wa mabasi na maroli kuwa wamepata utajiri kwa sababu za uchawi. Mtu akifa around utasikia lazima kifo kihusishwe na uchawi.

Sasa huyu Mchechu pamoja na aliyoyafanya bado anatafutiwa mchawi ili wamuangushe. Kwangu haiingii akilini kusikia kuwa anasimamishwa eti kupitisha uchunguzi ............ yaani hayo makosa yalikuwepo lakini yalikuwa yanasubiria Rais aalikwe kwenye ufunguzi wa mradi ndiyo aseme!!

Nafikiri huko mbeleni maCEOs wataanza kuepuka kumuita Rais kufungua miradi yao ..........!!

Anyway, tusubiri uchunguzi ..... ila hili la kwamba uanapika maandazi lakini hurusiwi kuyaonja mimi sioni kama linawezekana!!
 
Hiyo bodi si ndio wanafanyia vikao DUBAI?
uwanja wa kawe ulibinafsishwa kwa waarabu miaka 10 iliyopita, kupitia urais wa kikwete , walikubaliana kutengeneza kampuni tanzu ya kupaendeleza na NHC ndiyo waanze kujenga, wakati upande wa waarabu waliona wasubiri upepo wa raisi mpya( waliona mbali) kwa hiyo kwenda kufanya mkutano dubai ni kwa ajili ya mradi wa kawe na ni makao makuu ya mbia wao wa kawe project. acheni unafiki watanzania mmejaa umasikini wa mawazo
 
uwanja wa kawe ulibinafsishwa kwa waarabu miaka 10 iliyopita, kupitia urais wa kikwete , walikubaliana kutengeneza kampuni tanzu ya kupaendeleza na NHC ndiyo waanze kujenga, wakati upande wa waarabu waliona wasubiri upepo wa raisi mpya( waliona mbali) kwa hiyo kwenda kufanya mkutano dubai ni kwa ajili ya mradi wa kawe na ni makao makuu ya mbia wao wa kawe project. acheni unafiki watanzania mmejaa umasikini wa mawazo
We ndio maskini wa mawazo. Mtu anakuja kuwekeza kwako halafu anakupa masharti mpaka umfuate kwake, hiyo ni dalili mbaya.
 
Hii ni clear msg kwako pia kama umekabidhiwa dhamana ya kuutumikia umma basi simama na umma, hatuna sababu yoyote ya kumchukia mtu aliyesimama na umma kwenye sera zake.

Kuna kitu kinaitwa legacy, hii ni kitu muhimu kwa kila kiongozi, ukifika katika mji wa Cape town katika location za Langa, Gugulethu na Khayelisha utaona maelfu ya nyumba ambazo zilijengwa na Mandela na kuzigawa bure kwa raia wasiokuwa na uwezo.

Sasa kosa kubwa la kina Mchechu hawakuwa NHC kutatuwa shida ya makazi kwa Watanzania bali kufanya ubunifu ambao mwisho wa siku wao ndio wanaopiga pesa na malengo ya shirika yanawekwa pembeni, kumbuka hata Lukuvi mara nyingi amewalalamikia bei zao za nyumba lakini hawaelewi, eti leo unakuja na mradi wa apartments uziuze kwa shilling millioni 200 mpaka million 400 utasema wewe kichwani ni mzima kweli?

Tanzania bado kuna shida ya makazi tunahitaji watu serious wa kuiongoza NHC na siyo hawa wapigaji kama Mchechu.

Na kupiga siyo dhambi kama kazi unayofanya wengi wananufaika hakuna wa kukufuatilia. Hivyo tu.

Mkuu unawaangushia Nyumba mbovu
NHC Management ya NHC kumbuka lile ni Shirika la Serikali na kama hizo mnaita Nyumba za Bei nafuu ingawa hamsemi nafuu inaanzia Kiasi gani ...Serikali ndio yenye jukumu la kuiSUPPORT

NHC ikiwa pamoja nakuwaondolea KODI kwenye Vifaa vya Ujenzi au kuwapa RUZUKU nk tangu waanze Kujenga sijasikia Support ya Serikali kwenye maeneo hayo... Kama Vifaa wananunua na KODI kama mimi nawewe nahawana Ruzuku huo ubei Rahisi wa Nyumba watautoa wapi?

Halafu watu wengi wameanza kuitolea Macho NHC baada yakuingia huyo Jamaa nahasa iliposikika anapewa Mshahara Mkubwa kibongobongo iliumiza wengi...Maana tangu zamani hayo Majengo wakaaji wake ni Wahindi wanalithishana Baba mpaka Kitukuu...ni
Nyumba chache sana utakuta maGOLO

lkn asilimia kubwa wadosi... Sasa hizi Povu zinazomwagika sasa hivi kuhusu hao Jamaa wengine tunabaki na mshangao tu!

Huenda kuna ukweli kwenye tuhuma walizonazo chamuhimu nikusubiri ila mpaka Sasa hawana Kazi hata Tuhuma zao zisipothibitishwa tayari watakuwa wameondolewa!
 
Back
Top Bottom