Serikali yawaonya wanaowanyanyasa watalii

BimaYaAfya

Member
Nov 10, 2018
69
125
Serikali ya Zanzibar imewaonya watu ili waache tabia ya kuwabugudhi na kuwanyanyasa watalii wanaotetembelea visiwa hivyo.

Onyo hilo limetolewa na Seif Idd, Makamu wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati wa kuahirisha kikao cha Baraza la Mwakilishi, ambapo alisema "Unyanyasaji wa watalii wanaotembelea fukwe unaharibu picha nzuri ya serikali ya Zanzibar ulimwenguni kote,"

Aidha,Tume ya Utalii Zanzibar (ZCT) imepanga kuimarisha sekta ya utalii kwa kuvutia watalii zaidi kutoka bara la Asia ambalo lina idadi kubwa ya watu. Hata hivyo Serikali ya Zanzibar inalenga kupokea watalii 500,000 kutembelea Visiwa hivyo kila mwaka hadi kufikia mwaka 2020.
 

pepsin

JF-Expert Member
Apr 23, 2015
3,341
2,000
SMZ haina makamu wa kwanza wa rais, Seif Idd ni makamu wa pili.

Kwani ni lini serikali iliruhusu watalii wabughudhiwe
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom