Serikali yawajibu Umoja wa Ulaya(EU) na Marekani kuhusu kutokuwepo usalama na haki za binadamu Tanzania

Siyo kweli kivipi?

Hivi Tundu Lissu hajamiminiwa risasi mchana kweupe na Leo hii ni zaidi ya miezi 5 hakuna hata mtuhumiwa mmoja aliyekamatwa kwa mahojiano?

Hivi akina Akwilina, yule diwani wa Kilombero na huyu Katibu wa Hananasif hawajauawa kwa sababu za kisiasa??
 
Wizara imehoji kuwa ni hivi sasa tu ndio EU inataja juu juu shambulizi la silaha lililotokea Mkoa wa Pwani katika kipindi cha miaka miwili.” Kuchelewa kutolewa kwa matamko hayo baada ya muda mrefu na wakati mgumu unastaajabisha.

Moja ya matamko yaliyotolewa na mabalozi wizara imesema ni jambo zuri kwa mabalozi wametambua wito wa Rais Magufuli akitaka uchunguzi ufanyike wa matukio mengine ya uvunjifu wa amani katika wimbi la operesheni ya Kibiti, Mkuranga na Rufiji.



Kitu najiuliza, hivi kosa huwa linafutwa kwa kosa.. kwa kuwa kulikua na mauaji kibiti na walichelewa kutoa tamko, hata sasa wakati raia wanaendelea kutekwa na kuuwawa na watu wasiojulikana, huku demokrasia ikiendelea kudorora kwa kubana uhuru wakutoa maoni kwa raia hasa wale wanaoikosoa serikali, basi jamaa walipaswa kuendelea kukaa kimya tu..

Serikali yangu hii ya safari hii ni kiboko aisee
 
Hoja za msingi hazijajibiwa badala yake wemekimbilia kuzungumzia ya Rufiji na wanachoita mapambano dhidi ya rushwa. Kusema ukweli wamekwepa kabisa kujibu haja wanazolaumiwa nazo
 
No. Two wrongs do not make a right. If the mentioned embassies kept silent about the Mkuranga-Kibiti-Rufiji incidents, it does not imply they should also keep silent about the atrocities that followed. Besides, the state responded and instituted heavy measures to address the Mkuranga-Kibiti-Rufiji issue, so obviously no statement of condemnation was warranted except probably about appropriateness of those measures. The state has not instituted measures to curb what appears to be systematic persecution of opposition politicians including murders, tortures, disappearances, assassination attempts (by 'unknown assailants'). There have also been multitudes of wacky arrests and imprisonments of anyone who dares to criticize the government. The inaction and peculiar reactions send a very different message, and I believe the statements by the EU and US are made against this foundation.
 
Utofauti ni upi exactly, kwamba hao more than 30 wa kibiti ambao wengi waliouliwa ni wa ccm are lowlifes, compared to these few of chadema and a journalist. Shame on you guys
Tatizo lako unachukulia watu wote wanaccm na wanachadema. Kumbuka kuna Watanzania wasio na vyama nao wanaumizwa, haki zao zinakiukwa kwa hiyo kama bindamu mwenye utu ni lazima uguswe na haya yanayotokea ndani ya taifa letu bila kujali itikadi zetu. Ni vema Mungu atupe roho ya kujali utu wa Mtanzania.
 
Back
Top Bottom