Serikali yavunja mkataba na mbia TTCL | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yavunja mkataba na mbia TTCL

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MziziMkavu, Jul 11, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  SERIKALI imevunja mkataba na menejimenti ya kigeni ya Kampuni ya Simu (TTCL) iliyopewa mkataba wa miaka mitatu kuiongoza kampuni hiyo kubwa ya simu nchini. Habari za uhakika ambazo gazeti hili limezipata, zinaeleza kuwa, kutokana na serikali kuvunja mkataba huo, tayari Bodi ya Wakurugenzi ya TTCL imeshateua Watanzania wa kujaza nafasi zilizokuwa zinashikiliwa na menejimenti hiyo ya Saskatel International ya Canada.

  Serikali kupitia iliyokuwa Tume ya Rais ya Kurekebisha Mashirika ya Umma (PSRC), ndio iliingia mkataba wa miaka mitatu na Saskatel, lakini haikumaliza miaka hiyo mitatu badala yake imefanya kazi miaka miwili tu na kuamua kufungasha virago na kuiacha TTCL chini ya wazalendo ambao wamekuwa wanalilia kuongoza kampuni hiyo.

  Jana Bodi ya Wakurugenzi ilifanya kikao maalumu chini ya uenyekiti wa Profesa Mathew Luhanga na kuteua menejimenti ya wazalendo baada ya Saskatel kukubaliana na serikali kuvunja mkataba wake. Profesa Luhanga hakupatikana jana kuzungumzia suala hilo kwa kina kutokana na simu yake kuzimwa.

  “Wamekubaliana na serikali kuvunja mkataba bila masharti, hakuna kushitakiana,” alisema Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa TTCL, Amin Mbaga. Hata hivyo, hakutaka kuingia kwa undani suala hilo “Tutatoa taarifa zaidi hapo baadaye,” alisema. Leo menejimenti hiyo ya kigeni itakabidhi ofisi kwa menejimenti mpya ambayo imeteuliwa jana na Bodi. Menejimenti ya kigeni ilikuwa na maofisa wanne ambao kutokana na kuondoka kwao, Bodi imeteua watu wa kujaza nafasi hizo. Walioteuliwa kukaimu nafasi kadhaa ni Said A.

  Said ambaye anakuwa Kaimu Mtendaji Mkuu. Kabla ya hapo, Said alikuwa Mkuu wa Biashara wa TTCL Nyanda za Juu Kusini. Bodi hiyo pia ilimteua Kaimu Mkuu wa Fedha ambaye anakuwa Shaban Mrisho. Wengine ni Kaimu Mkuu wa Mtandao, Priscila Chilikweli na atakayekaimu ukuu wa mauzo na masoko ni Ernest Nangi.

  Uamuzi wa kuajiri menejimenti ya kigeni ulifanywa na kikao cha Baraza la Mawaziri na kutangazwa mbele ya waandishi wa habari na aliyekuwa Waziri wa Miundombinu wakati huo, Andrew Chenge mjini Dodoma licha ya kupata upinzani kutoka kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo.

  TTCL ilibinafsishwa Februari 23, 2001, Kampuni ya Consortium of MSI (ambayo sasa inajulikana kama Celtel International) ya Uholanzi na Detecon ya Ujerumani inamiliki asilimia 35 ya kampuni hiyo. Baada ya kubinafsishwa wawekezaji hao wakapewa jukumu la kuendesha menejimenti ya TTCL.


  Chanzo: HabariLeo
   
Loading...