Serikali yavunja mkataba na kiwanda cha Mponde Tanga

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,879
6,356
Awali akitangaza kuvunjwa kwa mkataba huo rasmi msajili wa hazina kutoka ofisi ya msajili wa hazina Laurence Mafuru amesema wamevunja rasmi mkataba huo kutokana na kukiukwa kwa makubaliano waliyowekeana na mwekezaji huyo kushindwa kuyatekeleza ipasavyo.

Aidha amesema kwa muda wa miaka mitatu sasa kiwanda hicho kilisimama kufanya shughuli za uzalishaji kutokana na mgogoro uliokuwepo baina ya wakulima na mwekezaji huyo hali iliyopelekea wakulima wa zao hilo kuyumba kimaisha.

Mafuru amesema lengo la serikali ni kuhakikisha inafufua na kuviendeleza viwanda vilivyopo Nchini kwa maslahi ya wananchi wake ikiwa ni pamoja na kukuza pato la mtu mmoja mmoja sambamba na kuinua uchumi wa eneo husika.

Amesema serikali ilifuata taratibu na sheria ya kusitisha mkataba huo hivyo wametengeneza menejimenti ya muda mfupi itakayoendesha na kuboresha kiwanda hicho chini ya usimamizi wa bodi ya chai ili kianze kazi ya uchakataji chai kwa haraka.

Chanzo: EATV
 
Umeelekea mrembo
 
Kama wamevunja mkataba na mwekezaji kwa kukiuka masharti ya mkataba ni sawa.

Swali 1: TEA BOARD ni regulator wa sector ndogo ya Chai Tanzania je manejimenti iliyoundwa ni sawa kuwa chini ya regulator?

Sawali 2
: Working capital inatoka wapi serikalini au watamortage mali za kiwanda wapata mikopo benki?

Swali 3. How competitive is this management team- it should be recalled viwanda vyote hivi viliwahi kuwa chini ya serikali na vikashindwa, je si wakati muafaka wa kutafuta mwekezaji mwingine ambaye ni experienced kwenye sector ili as soon as it is possible achukue management ya kiwanda toka kwa hii management team iliyopo chini ya bodi?

Swali 4. Baada ya kugundua mwekezaji huyu ameisababishia hasara serikali na kuwatia wananchi umaskini wa kipato kuna damage yoyote anatakiwa alipe? au, ndiyo kunyang"anywa tu kiwanda na basi yameisha

Swali 5: serikali lini itachukua similar steps kwa wawekezaji wengine wa aina hii kwa mfano wa mashamba ya mkonge, kahawa, ginneries za pamba, viwanda vya nguo, ngozi etc
 
Mmepiga hatua kwan huko kuna majipu mengi sana awajamaa wamebinafsisha viwanda utafikili Mali zao vibarua wanaburuzwa kama wako ugenini
 
pale mponde na kule lupembe viwanda vyote hivi alinunua kada wa CCM , ndugu Muller na ambaye kwa wakati fulani alikuwa mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mbeya na ambaye kwa sasa mdogo wake ndiye mbunge wa mbarali.
 
Mbona mikataba mibovu ya uwekezaji kwenye madini hawavunji......sekta y madini ndio inabeba uchumi we2 ila wao wamekalia mikataba y chai
 
Ndio hapo Lowasa alisema amechoka kuskia habari za mponde kila siku ,Jakaya alifika hapo ,waziri mkuu kafika kila siku kelele ,sasa hatua zichukuliwe ,
 
Back
Top Bottom