barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,874
Helicopter ya Jeshi la Polisi imetua Mkoani Iringa ili kuwaokoa watu waliozungukwa na maji ya mafuriko yenye vimelea vya Ugonjwa wa kipindupindu katika Tarafa ya Pawaga kwenye vijiji vya Mboliboli,Kimande na Usolanga.
Itakumbukwa hili ni jimbo la Isimani kwa Mbunge na Waziri wa Ardhi ndugu William Lukuvi.
Eneo hili ni maarufu sana kwa ulimaji wa mpunga ktk ukanda wa eneo la Bonde la mto Ruaha.
Serikali ameamuru kufungwa kwa vilabu vya pombe na utengenezaji wa aina yoyote ya Pombe za kienyeji,hali ni mbaya sbb watu wanakunywa maji yenye kinyesi yanayotoka kwenye majaruba ya mpunga.