Serikali yatua rasmi ‘zigo’ la ATCL | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yatua rasmi ‘zigo’ la ATCL

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by fangfangjt, Mar 25, 2011.

 1. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  Serikali yatua rasmi

  Fidelis Butahe
  SERIKALI imesema haiwezi kutoa fedha za kusaidia uendeshaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) na badala yake, inatafuta mwekezaji wa kuliendesha shirika hilo.

  Pia, imesema mkakati ulipo sasa ni kupunguza wafanyakazi 153 wa shirika hilo na kutafuta Dola 700,000 za Kimarekani kwa ajili ya kulipia matengenezo ndege moja iliyopelekwa Afrika Kusini. kwa matengenezo.

  Msimamo huo ulitangazwa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Omary Chambo, baada ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, kumtaka aeleze mikakati ya serikali katika ukusanyaji wa mapato na uboreshaji wa shirika hilo.

  Kamati hiyo ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wake, Zainab Vullu, pamoja na mambo mengine, ilisema moja ya sababu za kuzorota kwa shirika hilo ni Bodi na Menejimenti ya ATCL na kuitaka serikali iivunje bodi hiyo.

  Akijibu hoja hiyo, Chambo alisema kwa sasa hali ya ATCL ni mbaya na kwamba hiyo inatokana na kuwa na ndege tatu, moja ikiwa ya kukodi.Kwa mujibu wa katibu mkuu, ni ndege mbili tu kati hizo ndizo zinazomilikiwa na shirika.
  "Hivi sasa anatafutwa mbia wa kuendesha ATCL, ila serikali haiwezi kutoa tena fedha kwa ATCL, mkakati ulipo ni huo wa kutafuta mbia na kupunguza wafanyakazi," alisema Chambo,


  Alisema serikali pia sasa iko katika mchakato wa kutazama utendaji kazi wa Menejimenti na Bodi ya ATCL na kwamba ikijiridhisha, itachukua hatua stahiki.

  Mbali na ATCL wabunge hao pia walitaka kupata ufafanuzi kuhusu mkataba wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) ambayo serikali ina hisa ya asilimia 49 wakati Kampuni ya Rites ya India, ikiwa na asilimia 51 ya hisa.

  Akitoa ufafanuzi suala hilo, Chambo alisema serikali ipo katika hatua za mwisho za kununua hisa zote za Rites ili kampuni hiyo iongozwe na Watanzania na kwamba nguvu kubwa itawekwa katika uwekezaji ili kuboresha zaidi usafiri wa reli ya kati.

  Pamoja na majibu hayo wajumbe,waliokenaka kutoridhishwa na Mbunge wa Nkasi, Ali Mohammed Kessy (CCM), aliwataka wabunge wenzake wasimbane Chambo kwa kuwa hivi sasa siasa zimeingilia utendaji wa serikali.

  "Hapa makatibu wakuu mnawaonea bure, unajua siasa zimekuwa zikiwekwa mbele zaidi kuliko utendaji, kila kitu siasa tu, siasa tu, umefikia wakati wa kuweka fedha mbele siasa nyuma,” alisema Kessy.
   
 2. TITAN

  TITAN JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 309
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Iyo imetulia !!!
   
 3. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #3
  Mar 25, 2011
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hapo kwa BOLD!
  Ina maana mpaka leo hii Serikali haijajua utendaji MBOVU uliochukulia kuiua ATC (L)? Wasituchezee Akili zetu hawa...
   
 4. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  Badala ya dola laki saba za kimarekani tungetafuta sh. milioni mia tisa za kibongo!!! hivi hayo matengenezo....aaah kumbe ndege hazina insurance....wabongo bwana, keshokutwa utasikia bima ndio walilipia!!
   
 5. Mr. Mwalu

  Mr. Mwalu JF-Expert Member

  #5
  Mar 25, 2011
  Joined: Feb 4, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 60
  Wamasema siasa zimeingilia utendaji wa serikali, 'siasa' ni nini?
   
 6. n

  ngoko JF-Expert Member

  #6
  Mar 25, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 574
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hivi hii serikali imejifunza chochote kwa uwekezaji wa RITES kwenye TRL , tuliahidiwa mengi mazuri lakini tulipo kila mtu anapajua.
   
Loading...