Serikali yatoa ubani kwa marehemu Arusha

Serikali yatoa ubani kwa marehemu Arusha

Kwa hivyo thamani ya kila Mtanzania anapouaua ni Tsh milioni 5 siku hizi????????????????
 
Tunamsubiri Mh Pinda tuone anatoka vipi manake kila mmoja anajiuliza atoke na single gani???
 
mbona hajasema nani anawajibika, au siyo kazi yake?
 
Yani kaaazi kweli kweli!Hiyo mil. 5 ndo wameona ni kitu?
 
Bila wauaji hao (polisi) kushtakiwa Ubani na porojo hazitaleta haki. Tumeambiwa kuwa pia walikuwa wanapora simu za raia waliowakamata.Uhuni uliozidi kipimo kwa chombo cha dola.
 
Serikali inatakiwa kutimiza madai ya Chadema kuhusu wafiwa. Tamko linahitaji serikali iwalipe fidia wanafamilia za wafiwa. Ubani ni suala la pole. Sasa kinachofuata watimize sheria kwa kuwalipa fidia halali kisheria wanafamilia hao.
 
Hapa hakuna cha kujikosa. Kama watamudu kupindisha sheria za tanzania(kama kawaida yao eg zombe) bado watakutana na mkono wa Ocamp.
 
hivi Sabodo ametoa kiasi gani? au Sabodo ndiyo serikali
 
Hivi katika vurugu waliofariki ni wawili tu?

Hivi kuna kuna anayejua kuhusu wale waliouawa Pemba na Mwembechai kama nao walipewa ubani na kiasi gani, au kwa kuwa hili limepigiwa kelele sana ndio wanatoa huo ubani?
 
Serikali bado inajichanganya na ni aibu kubwa sana.
Unawapa wafiwa ubani wa milion 10!!...je walio mahospitalini na mlio waweka rumande mbona hamjatoa maamuzi kua mnataka kuwasaidiaje??
Roho na Utu za watu haziwezi kubadilishwa kwa hela milele.....yale yaleeee
Wao wana hela sisi tuna mungu..
 
Hapa sijaelewa,
polisi ktk tamko lao inaonesha hawa marehemu walivunja sheria. Sasa siri kali inatoa rambirambi kwa wavunja sheria. Yaani sasa majambazi wakiuawa na polisi, serikali itatoa rambirambi?

This is stupid and crazy!
 
Back
Top Bottom