Serikali yatoa kibali cha ajira kuziba nafasi zilizoachwa na waliokutwa na vyeti feki

Uongo halmashauri bado hazijapokea vibari hii serikali inawalaghai wananchi kwa nini?
Tulia wewe mambo ya kiserikali hayawahi haraka kama unamgegeda mke wa mtu huku unaogopa jemba yake itakukuta, govt ikisema itatenda
 
Madaraja na vyeo ni msamiati awamu hii
Sembuse ajira?
Unajua mtu akisikia mwezi wa saba anaona mbali na anaweza danganya atakavyo kumbe just near the corner ngoja tuone
 
Huu ni uongo mtupu. Asilimia 200?
Ninavyojua asilimia ni mwisho 100% tu.
Teh teh teh
Ndiyo haya haya ya madini, serikali ya ccm ni ya wezi na ni chanzo cha umasikini
Asilimia mwisho sio 100 inaweza kuwa hata 10000% kulingana na by how much kitu kimeongezeka, kama kitu kilikuwa 1000 mwanzoni kikaongozeka mpaka 4000 hapo ni kama 300% increase.. So wapo sawa kusema 200%

Ila tu ukweli ni kwamba vijana wanazidi kusoma namba vema
 
Sawa kwann huwahawajiamin kwa kusema ni lini wanazitoa??
Hii ni kama kauli ya NNE wanazungumzia ajira..na kuhusu hiyo mishahara ya 200% ..mhhhhhh
 
Waziri Angela Kairuki amesema kwamba serikali itaanza kuajiri watumishi wa serikali kwa kada mbalimbalk hususani katika sekta ya Afya na Elimu kutokana na upungufu wa asilimia 70% waliokumbwa na sakata la vyeti vyeki.

Pia ameongeza kwa kusema mishahara itapanda kutokana na agizo la Rais Pombe Magufuli na kwamba mishahara itapanda kutokana na ukuaji wa uchumi na mfumuko wa bei pamoja na kima cha chini cha mshahara kupanda kwa asilimia mia mbili 200% na kwamba mshahara umetoka kuanzia 100,000/= mpaka kima cha chini kuwa 300,000/=

Akijibu swali la Mbunge Lucy Mollel kwamba mafunzo kwa watumishi bado yanaendela na kwamba serikali haijafuta mafunzo kwa watumishi wa umma.

Waziri Kairuki amesema kwamba kwa sasa wanasubiri taarifa toka Tamisemi ili waweze kujua idadi ya watumishi wanaohitajika katika kila idara katika halimashauri mbalimbali nchini.



------
Waziri wa nchi,Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora Mh.Angela Kairuki amesema tayari serikali imeshatoa kibali cha ajira 15000 kwa ajili ya kujaza nafasi zilizoachwa wazi na watumishi waliobainika kuwa na vyeti feki katika zoezi lililofanyika nchi nzima la kuwabaini na muda si mrefu nafasi hizo zitajazwa.

Mh.Kairuki amesema hayo Bungeni mjini Dodoma wakati aijibu swali la nyongeza la mbunge wa viti maalum iringa mh.Rita Kabati aliyetaka kufahamu juu ya ujazwaji wa nafasihizo ambaye amekiri upungufu huo kusababisha usumbufu mkubwa katika taasisi mbalimbali za umma hivyo kuwahakikishia wananchi na kuwa tatizo hilo litakwisha hivi karibuni.

Katika hatua nyingine akijibu swali la Mbunge wa Mtwara mjini Mh.Maftaha Abdallah Nachuma aliyetaka uboreshwaji wa bandari ya Mtwara kwa kudai kuwa imesahaulika licha ya kuwa na kina kirefu katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati,Naibu waziri wa ujenzi,uchukuzi na Mawasiliano Mh.Edwin Ngonyaniamesema serikali inampango wa kuboresha na kuendeleza bandari zote nchini ikiwemo bandari ya Mtwara ili kuipunguzia mzigo bandari ya Dar es Salaam.

Mh.Ngonyani amesema kwani tayari imeshatenga fedha kwaajili ya ujenzi wa gati katika bandari ya Mtwara yenye urefu wa meta 350 itakayogharimu zaidi ya shiling bilioni137 inayotarajiwa kukamilika ndani ya miezi 21.

Chanzo: ITV

Du
 
Mwanasiasa ni mbaya bora wez wa makinikia yetu, waongo waongo tu, huyu mama nae kazd na mwenzake wa ufundi na sayansi! MATAMKOOOOOOOOO!

Walete report ya UHAKIKI vyeti fake part 2 maana wamekaa kimya as if ndo wameanza UHAKIKI wakati wamehakiki mwaka mzma!
 
Back
Top Bottom