PreGE2025 Serikali yatoa Bilioni 5.57 kujenga uzio wa shule zilizopo maeneo hatarishi

PreGE2025 Serikali yatoa Bilioni 5.57 kujenga uzio wa shule zilizopo maeneo hatarishi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

upupu255

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2024
Posts
341
Reaction score
476
Serikali imeendelea kuboresha miundombinu ya elimu nchini ikiwa ni pamoja na kujenga uzio katika shule mbalimbali za msingi kwa kuzipa kipaumbele shule zenye watoto wenye mahitaji maalumu.

Hayo yamesemwa bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Zainab Katimba alipokuwa akijibu swali la mbunge wa viti maalumu, Maimuna Ahmad Pathan aliyetaka kujua ni lini Serikali itajenga uzio kwa shule zilizopo maeneo hatarishi kwa kuwa shule nyingi za Mkoa wa Lindi hazina uzio.

Katimba ameongeza kuwa kwa mwaka 2022/2023 hadi 2023/2024 Serikali imetoa shilingi bilioni 5.57 kwa ajili ya ujenzi wa uzio katika shule 185 za watoto wenye mahitaji maalumu ikiwemo shule ya msingi Namakonde iliyoko Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa.

Aidha, amesema shilingi milioni 105.57 zimetumika kujenga uzio katika shule za sekondari Lindi Wasichana na Nachingwea Wasichana ambapo Serikali Kuu na Mamlaka za Serikali za Mitaa zitaendelea kutenga fedha za ujenzi wa uzio kwa ajili ya usalama wa wanafunzi na mali za shule kadiri ya upatikanaji wa fedha.

pia soma Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze
 
Pongezi kwa serikali.... Lakini shule na jamii ijikite zaid kwenye malezi bora.... Ukuta mtu anaweza ruka
 
ukitaka kuelewa kwamba tanzagiza inaongozwa na ma low iq angalia priorities zao, hivi kwa nini hiyo fedha wasiiwekeze kwenye mambo muhimu kwa wanafunzi kama maabara, madaftari, kalamu, vitendea kazi kwa walimu kama tu kuwa na printers na karatasi, umeme, maji au hata chakula kwa wanafunzi? mabilioni kwa uzio wa shule, really huku wanafunzi wanakaa chini hata vitabu hawana ?

siku tanzagiza itaamua kufwata meritocracy ndiyo labda tutatoka hapa kwenye huu mkwamo wa kuongozwa na incompetents …
 
Back
Top Bottom