Serikali yatishia kuwatimua Tanzanite one | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yatishia kuwatimua Tanzanite one

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by armanisankara, Aug 23, 2012.

 1. a

  armanisankara JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Serikali imetishia kuwatimua wawekezaji wa kampuni ya madini ya Tanzanite one iliyopo Mererani wilayani Simanjiro iwapo watashindwa kulipa deni la zaidi ya Dola za kimarekani milioni 2.2 zilizotokana na ukwepaji kodi.

  Katibu mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, alitangaza msimamo wa serikali wa kupitia upya mikataba ya makampuni ya madini hapa nchini baada ya kugundulika kuwa yapo makampuni kadhaa yamekuwa yakiendesha shughuli zake za madini bila kulipa ushuru wa serikali kinyume cha sheria.

  Akizungumza na Chama cha Wanunuzi na Wauzaji wa Madini nchini (Tamida), jijini Arusha jana, Maswi alisema kuwa kampuni ya Tanzanite one imekuwa ikikwepa kulipa kodi ya mrahaba wa madini tangu mwaka 2004 hadi 2008 na kufikia kiasi cha Sh. bilioni 3.4.

  Alisema kuwa kampuni hiyo ilikuwa ikitumia ujanja wa kukwepa kulipa mrabaha wa mauzo pale inapokuta soko la madini nje ya nchi limeongezeka na kwamba serikali kupitia kitengo cha ukaguzi wa madini ilibaini ukwepaji huo wa kodi na kuiamuru kampuni hiyo kulipa kiasi hicho cha fedha au ifungashe virago.

  ''Tulibaini ukwepaji wa ulipaji kodi kwa kampuni ya Tanzanite one baada ya kuanzisha kitengo maalumu cha ukaguzi wa migodi hapa nchini na tulipoifikia kampuni hiyo ndipo tulipobaini imekwepa kulipa kodi kiasi hicho, na hivi sasa tunaanza kupitia upya mikataba ya makampuni ya madini,'' alisema Maswi.

  Alifafanua kuwa kampuni hiyo iligoma kulipa deni hilo ikidai ni kubwa sana, ndipo serikali ilipotaka kufanya ukaguzi upya lakini kampuni hiyo iligoma na kudai kuwa ipo tayari kulipa deni hilo.

  Aliongeza kuwa iwapo kampuni hiyo ingegoma kulipa deni hilo serikali ilikuwa tayari kuwatimua na kuwamilikisha wazawa mgodi huo.

  Kwa mujibu wa Kamishina wa madini kanda ya kaskazini, Benjamin Mchwampaka, alisema kuwa tayari kampuni hiyo imeshaanza kulipa deni hilo na kwamba hadi sasa imeshatoa malipo ya dola 200,000 zaidi ya fedha za kitanzania milioni 310, huku serikali ikiitaka kuhakikisha inamaliza kulipa deni hilo hadi kufikia jamuari mwaka 2013.


  CHANZO: NIPASHE


  mimi naona kama serikali inadai fedha ndogo sana [deni la dola mil. 2] kampuni kama tanzania one inaingiza millions. sasa why serikali inadai kiasi kidogo?
   
 2. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2012
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Serikali hii haina ubavu huo.
   
 3. Davie S.M

  Davie S.M JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 720
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Ina maaana pamoja na Uhuni wote huo Hakuna kesi/fine au Penalty ...wanalipa iyo Laki2 maisha yanaendelea

  Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,661
  Trophy Points: 280
  Hata mie nashangaa kuona hawakuchajiwa penalty for late payment plus interest....pia kugomea ukaguzi inaonyesha walijua madudu zaidi yangegunduliwa.
   
 5. MARCKO

  MARCKO JF-Expert Member

  #5
  Aug 23, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 2,265
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Where has the govt been?
   
 6. k

  kijereshi JF-Expert Member

  #6
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 257
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Aise hii inasikitisha sana coy inagoma kufanyiwa ukaguzi ambacho ni 'statutory requirement' halafu worse still inalipa deni bila ya penalty na interest au ndo kuwalinda wawekezaji na kale ka mchezo kao ka 10% kama ilivyo ada cc waganga njaa ukifanya late payment ya tax maafisa wa ushuru wanavyokukomalia hizo penalty na interest utatamani ufunge kabiashara kako au kwenye hili kuna double standards?

  Sishangai huku ni kwenye tanzanite tu vipi kwenye madini mengine inawezekana hali ni mbaya zaidi kuliko tunavyoweza kufikiria halafu kibaya zaidi waongozaji wa hayo madudu siajabu ni watanzania wenzetu wenye roho za kujifaidisha wao na familia zao bila kuangalia maslahi ya umma.

  Tuko na safari ndefu sana ili tuweze kufika nchi ya ahadi kwa kizazi hiki cha chama chetu cha kijani sidhani kama tutatoka katika tope hili ndio maana nashangaa kila iliyeko kwenye hiki chama chetu tumbo lazima liwe limemchomoza hata kama alikuwa mwembamba vipi inasikitisha kwakweli.
   
 7. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #7
  Aug 23, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  wakiwatimua hasara itakua kwa nani????maana deni hawatolilipa tena,,,na kwanin hadi sasa wanaendelea kuchimba???wadaiwa wa heslb wameshaanza kuona machungu vp wadaiwa hawa???
   
 8. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #8
  Aug 23, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  kiasi kikubwa kinapelekwa USWIZI
   
 9. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #9
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Niliwahi kuandika humu jamvini kuwa mwaka wa 2010 hawa Tanzanite One walidai kupata carats 2.5mil na wakalipa mrahaba wa $400,000 lakini ukweli hicho walicholipa ni kama hakuna, nikatoa mfano kwenye mauzo huwa kuna grade kuanzia aaa, aa, a, b na c na kama wangeuza hayo madini kwa bei ya soko la ndani na yawe grade a na b tu serikali ingekusanya si chini ya $10mil. kwa mchanganuo ufuatao:
  Grade a ni sh 300,000 - 380,000 ($190 - $240)
  Grade b ni sh 200,000 - 300,000 ($126 - $190)
  Kwahiyo kwa wastani wa $190 wangeuza $475mil ambazo serikali ingepata $14mil, pia ikumbukwe kwamba nimekadiria ubora wa madini kwa viwango vya chini maana ukizungumzia grade aaa sio chini ya $500 kwa carat!

  Sasa wadau mjiulize hivi hata hao kitengo cha ukaguzi wamefanya kazi yao kweli ipasavyo maana ukaguzi wao umeibua $2mil kwa miaka 4/5 iliyopita hata ukizingatia uzalishaji ulikuwa pungufu ukilinganishwa na mwaka 2010? Au ndio uzalendo pembeni na wao hu'chukua chao mapema'?

  Taarifa za mapato na matumizi ya kampuni hii zinapatikana kwenye tovuti yao na yeyote anaweza kuzipata na kuzisoma.
   
 10. k

  kabombe JF-Expert Member

  #10
  Aug 23, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 15,575
  Likes Received: 8,517
  Trophy Points: 280
  Kiongozi unamjua fisadi Ami Mpungwe?ndio kampuni yake hiyo
   
 11. peri

  peri JF-Expert Member

  #11
  Aug 23, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  kwanini hawachukui hatua wanatishia tu?
  Wamechelewa kulipa hawapigwi fain?
   
 12. vipik2

  vipik2 JF-Expert Member

  #12
  Aug 23, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,175
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Hapa naona pana kitu kimejificha, Bungeni tulisikia kwa masikio yetu kuwa mkataba wa Tanzanite One utakapoisha basi hawataruhusiwa kupata mkataba mwingine na watapewa wazawa tu, leo vipi iwe wakilipa pesa hiyo basi wataachwa waendelee? kama sikosei jambo hilo Ole Sendeka alisimamia kidedea sana kuwa wasiongezewe mkataba lakini naye naona kama kawaida yake kisha lamba na hatatia neno tena la wazawa or kuachana na Tanzanite One.

  Hili ndio litanzania letu lilivyo, mchwa kila kona ya nyumba kuanzia kwenye bati mpaka ndani ya sakafu lakini na sie bado tunatinga ndani ya nyumba kama vile hakuna kibaya
   
 13. L

  Lekakui JF-Expert Member

  #13
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,411
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  This is not even a topic for discussion,serikali hii iliyoko madarakani hawawezi hata kujaribu kufanya hivyo,kwani wenye hiyo kampuni ndo walioko madarakani,pili hiyo hela ni ndogo sana kwa tanzanite one
  Gud day
   
 14. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #14
  Aug 23, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,652
  Trophy Points: 280
  Jamani leseni yao si ishaisha? Hawajaondoka tu?
   
 15. Philipo Kidwanga

  Philipo Kidwanga Verified User

  #15
  Aug 23, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 2,063
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  viongozi pumbavu serikali pumbavu wananchi pumbavu wanaume pumbavu wanawake pumbavu vijana pumbavu wasichana pumbavu watoto pumbavu kila kitu kwenye nchi hii cha kipumbavu. na mimi kwa sababu nimezungukwa na ninaishi kwenye nchi ya kipumabavu ni mpumbavu,na mimi upumbavu wangu na wa watanzania wenzangu unasababisha tuishi kipumbavu kama kondoo upumbavu wetu utatusababishia umauti siku moja eeeh mungu usitunusuru maana sisi ni wapumbavu tusiotaka kutumia akili ulizotujalia tuache upumbavu wetu uzidi kutuangamiza taratibu.pumbavu sana sisi watanzania.
   
 16. Philipo Kidwanga

  Philipo Kidwanga Verified User

  #16
  Aug 23, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 2,063
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  eti wanatishia kuwafukuza huku kwa upande mwingine wanabembelezea fungu la kumi masaburi wakubwa.
   
 17. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #17
  Aug 23, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Mnawabembeleza hawa wanaoiba kwasababu ni wakubwa. Wadogo wanagaragazwa chini bila huruma kwa kupigwa kodi za kufa mtu.
   
 18. Philipo Kidwanga

  Philipo Kidwanga Verified User

  #18
  Aug 23, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 2,063
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ungekuwa wewe ungeondoka kwenye neema usiyogharamia kwa chochote sisi ni kama marehemu.
   
 19. LE GAGNANT

  LE GAGNANT JF-Expert Member

  #19
  Aug 23, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 1,247
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Balozi amy mpungwe kumbe naye fisadi? Yeye ndio kiongozi wa hiyo kampuni na anakwepa kodi!
   
 20. a

  armanisankara JF-Expert Member

  #20
  Aug 23, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  asante kaka
   
Loading...