GEITA: Serikali yatenga zaidi ya Sh. Bilioni 6 za kuchimba visima Chato!

TCU haijakosea kabisa, namna michango ya watu humu ilivyo? Yaani hawaulizi hata kutaka kujua huo mpango ulikuwa wa lini, unajumuisha sehemu gani nyingine za nchi, je kuna sehemu au wilaya myingine zina miradi ya maji mikubwa kama hiyo, je Chato kuna shida au uhaba wa maji, wenyewe ni kutaka kuona watu wa Chato hawa enjoy haki zao kama wananchi wengine wa nchi hii kwa vile tu mtoto wao amekuwa Rais wa nchi. Kufikiri kweli kazi lakini kama imekuwa kazi kubwa namna hii hata kwa watu ambao wana nafasi ya kupata taarifa sahihi wakiwa wamekaa mbele ya gadget zao, basi tuna tatizo kubwa zaidi. Tumekuwa watu wa kupenda uzushi, uongo, uzandiki, fitina na uchonganishi utadhani katika hilo kuna la maana tutakalovuna. Haya tuendelee na kuzikiji haja ya hamu na ashki zetu. Wanasema zoea zoea watu utakuja zoea majini. Endekezeni endekezeni ashki zenu mtakuja kupata ashki za ushoga!
Nyie ndio watu mnawafanya watawala wajione wako sahihi muda wote.. Wewe inakuuma nini wananchi kuhoji why always mambo yanaenda huko? Hebu tuanze na wewe Wilaya yako imetengewa bajeti ya sh ngapi kwa ajili ya maji na uwanja wa ndege.
 
Why Chato everyday?Inamaana hao ndio wanahitaji huduma sana kuliko wengine?

Watanzania tuwe wavumilivu. Serikali inajua kuwa maeneo mengi nchini wananchi wana shida kubwa ya maji na baadhi ya maeneo shida inazidi iliyoko wilayani Chato. Jambo la faraja ni kuwa ipo mipango na utaratibu wa kuwafikishia wananchi maji kwenye kaya zao kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu kuyatafuta.

Mpango mkuu ni kuanza na wilaya aliyotoka rais. Zitafuatia wilaya za M/rais, w/mkuu na mawaziri wengine kulingana uwezo wa bajeti. Utekelezaji wa mpango huu ni rais wa jamhuri ya mwuungano wa tanzania.

Ili kuwaletea watanzania matunda ya utawala huu wa serikali ya awamu ya tano, mh ameamua kusimamia vilivyo ukusanyaji na matumizi ya mapato ya serikali. Watanzania ni mashuhuda wa namna rais anavyojitolea kuwaletea maendeleo bila ubaguzi wala upendeleo. Rais ni mkereketwa wa maendeleo na msemakweli. Alisema atawanunulia watanzania ndege zinazoweza kutua popote hata pasipokuwa na uwanja wa ndege ili hata wasio na uwezo wazipande; kanunua. Tumuombee kwa mungu maisha marefu na utumishi uliotukuka awatimizie watanzania ndoto yao ya nchi ya viwanda.

Mawaziri wa nishati na viwanda wakumbuke kuanza na mkoa anaotoka rais ikiwa ni ishara ya kumshukuru kwa juhudi anazofanya. Waziri anayehusika na ujenzi wa barabara na viwanja vya ndege ameonyesha mfano.
 
Hivi wanainchi wa Kahama walipopelekewa maji toka ziwa Victoria kwa gharama ya Tsh billion 200 nako huko Wilaya ya Kahama kuna Rais anatoka au??
 
Wale wazee wa kupongeza watakuja na wimbo "kwani chato sio Tanzani!" ebu orodhesheni miradi mingine inayoendelea chato mi naanza na chato international airport, jengo kubwa la TRA, msd nk

Kura si zilitoka chato zote nyie kajambakoti mtajuju na 2020 wachato watakuwa wamezaana na kura zitamtosha dadadeki
 
nitahamia chato baada ya miradi kadhaa kukamilika...
.
inawezekana huu ni mkakati wa kupunguza idadi ya watu Dsm... maana anayekwambia mpaka mwezi wa 7 ukibaki huku we kidume,halafu wakati huohuo anaendeleza pengine maana yake kwa tafsiri rahisi amekwambia nenda kule ninapoendeleza..sawa. naja!!!
 
maji ni uhai na yakiwa karibu ni bora zai. lakini kukinga vijito ili kupata mabwawa huwa na manufaa zaidi. utafuga samaki, kunywesha mifugo kirahisi na kilimo cha mboga pembeni. visima vina kawaida ya kukauka.
 
Back
Top Bottom