PreGE2025 Serikali yatenga Sh. Bilioni 25 kutekeleza mradi wa SLR

PreGE2025 Serikali yatenga Sh. Bilioni 25 kutekeleza mradi wa SLR

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Wont be the same

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,564
Reaction score
2,483
KATIBU Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kiasi cha Shilingi Bilioni 25 zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Bayoanuai Tanzania (SLR-Tanzania) ulioanza mwaka 2021-2025 katika Mikoa mitano na Halmashauri za Wilaya saba nchini.

Aidha kutokana na mwitikio chanya wa wananchi katika kutekeleza mradi huo, Serikali imekusudia kuongeza maeneo ya utekelezaji, katika Mikoa na Halmashauri nyingine nchini.

Mhandisi Luhemeja amesema hayo jana Jumamosi Machi 15, 2025 Jijini Mbeya wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati tendaji ya kitaifa ya usimamizi wa mradi huo kilichojadili shughuli mbalimbali za utekelezaji wa mradi huo hadi kufikia sasa.
Snapinst.app_484887726_18491959897056691_1856233941772388222_n_1080.jpg


Luhemeja amesema tathimini iliyofanywa na Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais, imeonesha wananchi wamefurahishwa na utekelezaji wa shughuli za mradi na hivyo Serikali imepanga kuhakikisha kuwa inaongeza wigo wa maeneo ya utekelezaji wake ili kuleta manufaa katika masuala ya uhifadhi wa mazingira nchni.

“Mwezi Oktoba mwaka huu tutafanya tathimini ya mradi na ili kuona uwezekano kupata maeneo mengi zaidi ya utekelezaji ili kutunza mazingira na pia kuwanufaisha jamii mbalimbali ambazo zimeweza kubuni miradi ya kijamii inayowaingia kipato kutokana na shughuli mbadala zinazoenda sambamba na uhifadhi endelevu wa mazingira” amesema Lihemeja.
Snapinst.app_484516023_18491959873056691_9091599755843196723_n_1080.jpg


Ameongeza kuwa mradi wa SLR ni mojawapo ya miradi ya mfano ambayo Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais imekusudia kuianzisha katika maeneo mbalimbali nchini, ili kuisaidia jamii kuongeza hamasa ya uhifadhi wa mazingira na hivyo kuweza kutumia vyema fursa ya mabadiliko ya tabianchi kwa ajili ya kuibua miradi ya kijamii.

Amefafanua kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais itaendelea kujenga uwezo kwa jamii zinazotekeleza mradi huo ziweze kuhamasisha katika masuala ya uhifadhi wa mazingira na kutumia fursa zilizopo kuweza kujiongeza kipato kupitia shughuli za uzalishaji mali.
Snapinst.app_484998642_18491959888056691_857914424570670988_n_1080.jpg

Soma pia: Pre GE2025 Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze
 
Back
Top Bottom