RUCCI
JF-Expert Member
- Oct 6, 2011
- 1,701
- 1,714
Baraza la Mitihani la Taifa limetangaza matokeo ya kumaliza elimu ya msingi (PSLE) ambayo yameonyesha ongezeko la ufaulu kwa asilimia 2.
Akitangaza matokeo hayo leo (Alhamisi), Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema jumla wa watahiniwa 555,291 kati ya 789,479 waliofanya mtihani huo wamefaulu.
Amesema idadi hiyo ni sawa na asilimia 70.3 ya ufaulu tofauti na ufaulu wa mwaka jana ambao ulikuwa ni asilimia 67.8
"Hivyo kuna ongezeko la ufaulu kwa asilimia 2.52," amesema Dk Msonde.
Shule iliyoongoza kitaifa ni shule ya Msingi Kwema ya mkoani Shinyanga.
Tembelea Hapa=> Link ya Kwanza
Tembelea Hapa=> Link ya Pili
Habari hii imetumika kwenye Kipindi cha JamiiLeo kinachorushwa kila siku jioni katika Channel ya JamiiForums kwenye mtandao wa YouTube.
Kuona kipindi hicho angalia video ifuatayo, acha maoni yako na kisha Subscribe kwenye Channel ya JamiiForums.