Serikali yatangaza bei mpya ya unga Dar

Serikali yatangaza bei mpya ya unga Dar

Bagamoyo

Platinum Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
29,878
Reaction score
34,037
Bei ya Unga wa Mahindi kupungua kutoka Sh1,500 hadi 900 kwa kilo

January 23, 2013 | Na Nora Damian wa gazeti la Mwananchi

BEI ya unga wa sembe mkoani Dar es Salaam inatarajia kupungua kutoka Sh1,500 hadi 900 kwa kilo kuanzia wiki hii baada ya tani 3056 za mahindi kuanza kukobolewa.

Serikali ilitoa vibali kwa wenye vinu vya usagishaji kuchukua mahindi kwenye maghala ya kitaifa kwa ajili ya kupunguza makali ya bei za vyakula kupanda.

Mkoa wa Dar es Salaam ulipata mgao wa tani 6,400 kutoka wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika na hadi sasa tani 3056 za mahindi zimetolewa kwa wafanyabiashara hao walioingia mkataba na Serikali kuuza unga bei ya rejareja Sh900.

Akizungumza na gazeti hili jana, Ofisa Kilimo Mwandamizi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Denis Nyakisinda alisema tani hizo zimegawanywa katika wilaya tatu za mkoa huo ambapo Kinondoni imepata tani 3,600 wakati Temeke na Ilala zimepata tani 1,400 kila moja.

Alisema Wilaya ya Kinondoni imepewa tani nyingi kwa sababu kuna mashine nyingi na kwamba Tandale na Manzese ndiyo inayolisha Dar es Salaam.

"Kila aliyepewa mahindi amepewa mkataba wenye maelekezo kwamba auze unga kwa bei ya Sh900 kwa kilo na tutafuatilia ili kuona bei ya unga inashuka," alisema Nyakisinda na kuongeza kuwa:

"Kuna baadhi ya maeneo kama ya Mbagala ambako kuna wafanyabiashara walishachukua mahindi hivyo tunategemea bei ya unga itapungua baada ya mahindi kuingia sokoni na kukobolewa," alisema.

Alisema hadi sasa kuna wafanyabiashara 48 ambao wamepewa vibali kwa ajili ya kwenda kununua mahindi hayo katika maeneo ya Songea, Makambako na Mbozi na kwamba wafanyabishara hao ni wale wa kati, wadogo na baadhi ya makampuni makubwa.

Alisema mchakato wa kuwapata wafanyabiashara hao ulifanyika kwenye wilaya kwa kupitia kwa watendaji wa mitaa ambako mashine zipo na kwamba baada ya hapo mkoa ulipokea majina na kuyatuma Wakala wa Chakula (NFRA) kwa ajili ya kupewa vibali.

Kwa mujibu wa ofisa huyo, Songea zimetengwa tani 4200 ambapo wafanyabiashara watakaokwenda kuchukua huko watauziwa kwa bei ya Sh460 kwa kilo wakati Mbozi zimetengwa tani 1800 na wafanyabiashara watauziwa Sh490 kwa kilo na Makambako ziko tani 400 ambazo wafanyabiashara watauziwa Sh500 kwa kilo.

Alisema mfanyabiashara atakayekiuka mkataba atachukuliwa hatua za kisheria kwani wamejipanga kufuatilia kwa kila mfanyabiashara aliyepewa kibali na kwamba kila wanaposhusha mzigo lazima wapige simu kwa maofisa kilimo wa maeneo husika.

My Take:
Je, ni dalili za soko holela kufeli au ni propaganda za kisiasa ambapo serikali inajaribu kuonesha kufahamu wananchi wake wana maisha magumu na hivyo kurejelea sera na siasa za Mwalimu Nyerere?
 
walitakiwa waje na mpango endelevu. hizo tani walizotoa ni za kuliwa na kuisha siku mbili. baada ya hapo nini kitafuata?? bei si itarudi palepale?? wakajipange upya aisee
 
an empty skull normally comes out with a solution full of foolish grin!!!!!!

How long will the government keep on supplying this service to its people?

Or are they doing this just b'se of getting rid of a number of rotten maize bags from their stores?

Is this what a state interventions account for in improving people
's life standards?

Oooops!!! very sorry, I'm temporarily out of reach due to some compromised technical errors in terms of state regime in our country.

Hope to meet you in the soonest time after state economic reform is done!!!!
 
Ni vigumu kwa serikali ku-control hiyo bei elekezi. Binafsi nafanya biashara hiyo ingawa sikufanikiwa kupat hayo mahindi. Lakini watu wengi wenye mashine wanauza huo unga kwa sh. 30,000/= kwa mfuko wenye ujazo wa kilo 25kg- wastani wa sh.1200/= kwa kilo. Akisha saga anasambaza kwa wateja wake madukani.

Kwa hiyo ni vigumu kwa mlaji wa kawaida kumwambia muuzaji kuwa niuzie kwa bei elekezi kwa sababu hakuna control mechanism inayomlazimisha muuzaji wa rejareja kuuza kwa bei elekezi zaidi ya matamko ya kwenye magezeti. Sina hakika kama lengo la serikali litatimia zaidi ya kuwanufainya wafanya biashara.
 
Hivi bado tume ya BEI ipo katika nchi hii?

Mimi nilikuwa nafikiri tuko kwenye mfumo wa soko HURIA na Market forces ndizo zinafanya kazi.

Hao wachumi first class akina Mwingulu Nchemba wako wapi kuishauri serikali ya CCM? Bado CCM wanafikiri ki Eastern europe europe ila ya 70s
 
Hii haina tofauti na lile tamko la serikali kuhusu bei ya sukari ambalo lilipuuzwa na wafanyabiashara...wananchi wameendelea kuumia hadi sasa.
 
biashara zingine hizi hata hazieleweki, kwa nini wasingeacha bei iji regulate yenyewe kutokana na production/supply? supply ikiwa kubwa demand itapungua na bei itapungua tu.
 
Ule uchumi wa soko umeshindwa; si waliache soko liamue bei?

wanataka kuwanufaisha mafisadi kwa mahindi yetu. Hata sukari si walisema hivi hivi? Wakatoa na vibali vya kwenda kubeba sukari pakistani ili kupitishia bongo kwenda china? We toka lini pakistani wakawa exporters wa sukari!
 
walitakiwa waje na mpango endelevu. hizo tani walizotoa ni za kuliwa na kuisha siku mbili. baada ya hapo nini kitafuata?? bei si itarudi palepale?? wakajipange upya aisee
Mdogo wangu una akili sana wewe. Kauli za kisiasa za wanasiasa waliofilisika uwezo wao wa kufikiri.
 
an empty skull normally comes out with a solution full of foolish grin!!!!!!

How long will the government keep on supplying this service to its people?

Or are they doing this just b'se of getting rid of a number of rotten maize bags from their stores?

Is this what a state interventions account for in improving people
's life standards?

Oooops!!! very sorry, I'm temporarily out of reach due to some compromised technical errors in terms of state regime in our country.

Hope to meet you in the soonest time after state economic reform is done!!!!

We are not even sure when exactly the state economic reform will be done! You better come back home soonest possible (though how soon is soon may be a question)!
 
Afadhali kidogo wengine tutaweza pata milo 3 kwa siku.

Sent via EyePhone
 
Bei ya Unga wa Mahindi kupungua kutoka Sh1,500 hadi 900 kwa kilo

January 23, 2013 | Na Nora Damian wa gazeti la Mwananchi

BEI ya unga wa sembe mkoani Dar es Salaam inatarajia kupungua kutoka Sh1,500 hadi 900 kwa kilo kuanzia wiki hii baada ya tani 3056 za mahindi kuanza kukobolewa.

Serikali ilitoa vibali kwa wenye vinu vya usagishaji kuchukua mahindi kwenye maghala ya kitaifa kwa ajili ya kupunguza makali ya bei za vyakula kupanda.

Mkoa wa Dar es Salaam ulipata mgao wa tani 6,400 kutoka wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika na hadi sasa tani 3056 za mahindi zimetolewa kwa wafanyabiashara hao walioingia mkataba na Serikali kuuza unga bei ya rejareja Sh900.

Akizungumza na gazeti hili jana, Ofisa Kilimo Mwandamizi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Denis Nyakisinda alisema tani hizo zimegawanywa katika wilaya tatu za mkoa huo ambapo Kinondoni imepata tani 3,600 wakati Temeke na Ilala zimepata tani 1,400 kila moja.

Alisema Wilaya ya Kinondoni imepewa tani nyingi kwa sababu kuna mashine nyingi na kwamba Tandale na Manzese ndiyo inayolisha Dar es Salaam.

"Kila aliyepewa mahindi amepewa mkataba wenye maelekezo kwamba auze unga kwa bei ya Sh900 kwa kilo na tutafuatilia ili kuona bei ya unga inashuka," alisema Nyakisinda na kuongeza kuwa:

"Kuna baadhi ya maeneo kama ya Mbagala ambako kuna wafanyabiashara walishachukua mahindi hivyo tunategemea bei ya unga itapungua baada ya mahindi kuingia sokoni na kukobolewa," alisema.

Alisema hadi sasa kuna wafanyabiashara 48 ambao wamepewa vibali kwa ajili ya kwenda kununua mahindi hayo katika maeneo ya Songea, Makambako na Mbozi na kwamba wafanyabishara hao ni wale wa kati, wadogo na baadhi ya makampuni makubwa.

Alisema mchakato wa kuwapata wafanyabiashara hao ulifanyika kwenye wilaya kwa kupitia kwa watendaji wa mitaa ambako mashine zipo na kwamba baada ya hapo mkoa ulipokea majina na kuyatuma Wakala wa Chakula (NFRA) kwa ajili ya kupewa vibali.

Kwa mujibu wa ofisa huyo, Songea zimetengwa tani 4200 ambapo wafanyabiashara watakaokwenda kuchukua huko watauziwa kwa bei ya Sh460 kwa kilo wakati Mbozi zimetengwa tani 1800 na wafanyabiashara watauziwa Sh490 kwa kilo na Makambako ziko tani 400 ambazo wafanyabiashara watauziwa Sh500 kwa kilo.

Alisema mfanyabiashara atakayekiuka mkataba atachukuliwa hatua za kisheria kwani wamejipanga kufuatilia kwa kila mfanyabiashara aliyepewa kibali na kwamba kila wanaposhusha mzigo lazima wapige simu kwa maofisa kilimo wa maeneo husika.

My Take:
Je, ni dalili za soko holela kufeli au ni propaganda za kisiasa ambapo serikali inajaribu kuonesha kufahamu wananchi wake wana maisha magumu na hivyo kurejelea sera na siasa za Mwalimu Nyerere?
sioni kipya hapo kama serikali ilishindwa kuwabana wanaouza mafuta ambayo hata wao wenyewe wanaweka kwenye magari yao itawezaje kuwabana wanouza sembe wasiyoila?
 
Hizi ni dalili tosha za serikali ya mheshimiwa dhaifu kufirisika kiuchumi na kifikra.
 
Sijaelewa vizuri, Mna maana shirika letu la umma la NMC limefufuliwa?
 
Back
Top Bottom