Serikali yatafuta mwarobaini wa bidhaa feki

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
Wananchi tutamalizika kwa maradhi kwa kufakamia Bidhaa Fake zikiwemo Vyakula na Madawa yaliokuwa yamesha maliza muda wake na wafanya biashara kuyabadilisha date.

------/

ASILIMIA 20 ya bidhaa zote zinazoingizwa nchini ni bandia, hivyo kuhatarisha maisha ya wananchi, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda amesema.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Dk Kigoda alisema kama hali hiyo itaachwa iendelee itasababisha madhara makubwa kwa wananchi na taifa kwa jumla.

Alisema kuenea kwa soko la bidhaa bandia nchini kunatokana na bei za bidhaa hizo kuwa ndogo, hivyo kuwavutia wateja wengi.

"Watanzania wenye kipato cha chini ndiyo wapenzi zaidi wa bidhaa hizi lakini wanatakiwa kutambua kuwa madhara yake ni makubwa mno," alisema Dk Kigoda na kueleza kuwa Serikali imetangaza vita na wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa hizo.

Dk Kigoda aliwataka wafanyabiashara wanaouza bidhaa hizo kuziondoa sokoni haraka kabla Serikali haijaanza kuziondoa kwa nguvu. Waziri Kigoda alisema uchunguzi umebaini kuwa, kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo mkoani Pwani, kuna bandari bubu 32, ambazo hutumika kupakua bidhaa hizo bandia.

Alizitaja bidhaa hizo kuwa ni matairi ya magari na pikipiki, mafuta ya kupaka, maziwa ya watoto, nyaya za umeme, simu za mkononi na vyakula mbalimbali.

Alisema katika kukabiliana na hali hiyo, wizara yake inashirikiana na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), kuchunguza bidhaa zinazoingia nchini kabla hazijasambazwa katika soko.

Alipoulizwa ni lini operesheni ya kuwakamata wanaouza bidhaa hizo itaanza, Dk Kigoda alimtupia swali hilo Katibu Mkuu wa Wizara yake, Joyce Mapunjo ambaye alisema huenda ikaanza leo, huku akisema wizara inachokifanya kwanza ni kutoa tahadhari. Dk Kigoda akaongeza... "Tukianza (operesheni maalumu) hatutakuwa na mjadala."

"Zipo nyaya bandia za umeme ambazo kwa kiasi fulani zinaweza kuwa chanzo cha kuongezeka kwa matukio ya nyumba kuteketea kwa moto nchini, pia yapo matairi ya magari na pikipiki ambayo nayo kwa kiasi fulani yanachangia kuongezeka kwa ajali."

Akitolea mfano Mkoa wa Dar es Salaam, Dk Kigoda alisema kuanzia Januari mpaka Novemba mwaka huu, kulikuwa na ajali za pikipiki 1997, zilizosababisha vifo vya watu 140.

"Tumejipanga kuhakikisha jambo hili tunalimaliza kabisa, kwanza tumegundua bandari bubu 32 ambazo pamoja na mambo mengine, zinaifanya Serikali kukosa mapato na kuhatarisha usalama wa wananchi" alisema Dk Kigoda.

Alisema kuwa tayari wameshazieleza taasisi zilizo chini ya wizara hiyo kutoa elimu kwa wananchi juu ya madhara ya kutumia bidhaa bandia yakiwamo ya hasara kutokana na kuharibika katika kipindi kifupi.

"Wafanyabishara wanaonunua bidhaa kutoka China wanatakiwa kuwa makini kwa sababu bidhaa zao wanaziuza kulingana na ubora wake, zipo zenye ubora wa juu hadi wa chini," alisema Dk Kigoda na kuongeza: "Sasa wapo Watanzania wanaonunua za ubora wa chini na kuja kuuza nchini kwa sababu wanataka kupata faida zaidi."

Alisema katika kuhakikisha kuwa ajali za barabarani zinapungua, Serikali imetoa pendekezo kwamba kila anayeuza pikipiki ni lazima auze na kofia ngumu (helmet) mbili.

"Hili ni pendekezo ambalo ni kama limeshapita kwa sababu kwa hali ya kawaida kuvaa helmeti ndiyo tahadhari kwa wanaotumia pikipiki," alisema Dk Kigoda. Dk Kigoda alisema wizara hiyo imekuwa ikipokea barua mbalimbali kutoka kwa wananchi, zinazowataja vinara wa kuuza bidhaa hizo, pamoja na maduka au maeneo ambayo bidhaa bandia, huuzwa kwa wingi.... "Hivyo tunawajua wanaofanya hivyo, tunawataka kuziondoa haraka."

Chanzo: Serikali yatafuta mwarobaini wa bidhaa feki - Kitaifa - mwananchi.co.tz
 
Dawa ipo lakini Serekali bado haijaamuwa, hivi kweli kazi ya wakemia ni nini? kula rushwa na kutuingizia maradhi au vipi?.
ikiwa Serekali itahimiza kuwa yoyote mwenyekuingiza bizaa fake atanyaganywa leseni na kupigwa faini na azabu kali basi

Watanzania tunaweza kuwa na matumaini kuwa tunachokula sio sumu na itapunguza mtiririko wa maradhi sugu yasababishwayo na madawa mabovu na vyakula vibovu ambavyo wafanya biashara hutumia utalamu wa kubadilisha date.
 
Back
Top Bottom