The Boss
JF-Expert Member
- Aug 18, 2009
- 49,229
- 116,840
ITV saa nne asubuhi hii wametoa hii habari kwa ufupi.
Maafisa wa Wilaya ya Kyela wamesimamisha kampuni ya Kigeni iliyokuwa inachimba makaa ya mawe toka mwaka 2013.
Huku Serikali ikisema 'ilikuwa haina taarifa'
Kampuni hiyo imechimba na kuuza nje makaa ya mawe.
Nimeona ofisa wake Mzungu anaongea accent kama ya Marekani hivi.
Kampuni ina mashine zote na inachimba waziwazi kwa miaka mitatu vila vibali na serikali inakuja kusema walikuwa hawana taarifa.
Only in Tanzania....
Maafisa wa Wilaya ya Kyela wamesimamisha kampuni ya Kigeni iliyokuwa inachimba makaa ya mawe toka mwaka 2013.
Huku Serikali ikisema 'ilikuwa haina taarifa'
Kampuni hiyo imechimba na kuuza nje makaa ya mawe.
Nimeona ofisa wake Mzungu anaongea accent kama ya Marekani hivi.
Kampuni ina mashine zote na inachimba waziwazi kwa miaka mitatu vila vibali na serikali inakuja kusema walikuwa hawana taarifa.
Only in Tanzania....
PROF. MUHONGO ASIMAMISHA SHUGHULI ZA KAMPUNI YA OFF - ROUTE TECHNOLOGY ILIYOPO KYELA
Serikali imesimamisha shughuli za uchimbaji wa Makaa ya Mawe ya Kampuni ya Off Route Technology iliyopo Kyela ikiwemo kukamata vifaa vya uchimbaji na kuhakikisha kuwa vinakuwa chini ya uangalizi wa Mkoa wa Mbeya hadi hapo uchunguzi dhidi ya uhalali wa kampuni hiyo kuchimba makaa utakapokamilika.Hatua hiyo inafuatia ziara ya Waziri wa Nishati na Madini, Prof Sospeter Muhongo kutembelea mgodini hapo na kubaini kuwa, kampuni hiyo inachimba makaa bila kuwa na leseni halali ya uchimbaji madini.
Aidha, Prof. Muhongo ameitaka kampuni hiyo kulipa kodi zote za Serikali ikiwemo inazodaiwa na Halmashuri tangu ianze kufanya shughuli za kuchimba.Aidha, ili kujua undani wa suala hilo, Prof. Muhongo ameitisha kikao kifanyike kati ya mgodi huo , Wizara ya Nishati na Madini, Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania ( TMAA), Ofisi ya Madini Kanda ya Kusini Magharibi, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kyela, tarehe 18 Januari, 2016 chini ya uenyekiti wa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini.
"Hawa watu wamechimba makaa, wameuza bila kuwa na Leseni na tunawadai kodi zetu. Uongozi hakikisheni katika kikao hicho mnakuja na madai yenu,TMAA pia mje na madai yenu", ameongeza Prof. Muhongo.
Prof. Muhongo pia amezitaka pande zote kuwasilisha nyaraka muhimu kuhusu suala hilo, ili iamuliwe kwa kufuata sheria na taratibu stahili, "hakuna mtu atakayeonewa, kila upande uje na nyaraka zote na sisi wizarani huko ndani kwetu tutaulizana wenyewe kuhusu jambo hili halafu tutalitolea taarifa" ,amesema. Prof. Muhongo.
Akifafanua kuhusu suala hilo , Afisa Mfawidhi wa TMAA ,Mhandisi Jumanne Mohamed amesema kuwa, awali Wakala huo ilifanya ukaguzi na kubaini kuwa kampuni hiyo hailipi kodi na kuwa yapo malimbikizo ya madai ambayo yalipaswa kulipwa na kuongeza kuwa baada ya mawasiliano juu ya suala hilo, kampuni iliahidi kulipa kwa awamu jambo ambalo halijafanywa hadi sasa.Kampuni ya Off Route Technology, ipo katika Kijiji cha Ngana Wilaya ya Kyela mkoa wa Mbeya.
Habari ni kwa Msaada wa Mitandao ya Kijamii
Last edited by a moderator: