Serikali yashindwa kupandisha mishahara

TUMBIRI

JF-Expert Member
May 7, 2011
1,933
1,199
Jamani habari ndio hiyo, ni utaratibu wa Serikali kila mwaka unapoanza Watumishi wake hupandishwa ngazi ya mshahara lakini toka mwaka huu wa fedha uanze na tunakaribia kumaliza nusu ya kwanza bado watumishi hatujapandishwa 'Increment' zetu ambazo ni stahili zate kulingana na waraka wa Utumishi wa Umma. Mi binafsi nalipwa TGSF2 tangu mwaka jana badala ya TGSF3 ya mwaka huu.

Kama wameishiwa waseme tu, sisi tupo tayari kuwasamehe hizo Increment lakini kukaa kimya si dawa ya kutiba ugonjwa - Mficha Uchi hazai.

Mheshimiwa Moderator,
Naomba kutoa hoja.
 
Kwanza mshahara wa mwezi uliopita mmelipwa??? Nasikia wafanyakazi wa umma hamjalipwa mshahara wa November hadi leo wewe unalilia nyongeza hahaha kweli dunia kizungu zungu poleni sana.
 
Mi wangu umeingia jana jioni.
 
Mimi nilisikia kwamba serikali ilipoongeza ile mass increment basi ikafuta annual increment. Sasa sijui huo ni utaratibu maana mie nina miaka miwili kazini lakini sijawahi kupata annual increment na wala sijali. Kazi ninayoifanya ninaipenda hata wasiponipa mshahara nitafanya bure. Mshahara wenyewe nikipata unaisha baada ya siku tano, mshahara gani huo kama si matusi, laki mbili mtu una mke na mtoto?
 
Mimi wa kwangu tayari nimeishakula karibu unaisha, ila niko kwenye SU maana kwenye SU wakati mwingine hutumia fedha zao huku wakisubiri cheque ya hazina ili kureplace fedha iliyotumika kulipa mishahara
 
Mimi nilisikia kwamba serikali ilipoongeza ile mass increment basi ikafuta annual increment. Sasa sijui huo ni utaratibu maana mie nina miaka miwili kazini lakini sijawahi kupata annual increment na wala sijali. Kazi ninayoifanya ninaipenda hata wasiponipa mshahara nitafanya bure. Mshahara wenyewe nikipata unaisha baada ya siku tano, mshahara gani huo kama si matusi, laki mbili mtu una mke na mtoto?
sasa mkuu wewe unaishije? kama mshahara unaisha baada ya siku tano, unafika mwisho wa mwezi na familia yako?
 
...hayo yote tisa,kumi ni kituko cha Watumishi wa Mahakama. Wabunge walipitisha sheria ya uanzishaji wa JUDICIAL SERVICE COMMISSION,kwa misingi kwamba watumishi wa Mahakama watapandishiwa mishahara. Matokeo yake,hakuna cha mshahara mpya na bunge letu lipo kimya. Kweli hii ndo Tanzania ya Kikwete,mambo yote huishia kwenye makaratasi!!
 
Back
Top Bottom