Serikali yashikilia makato ya Bima ya Afya; NHIF wasitisha huduma

Lupweko

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2009
Posts
25,143
Reaction score
27,280
Katika hali ya kushangaza, serikali imeshindwa kuwasilisha makato ya mishahara ya wafanyakazi wa baadhi ya taasisi zake katika Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) kwa miezi mitatu. Hii inatokana na mfumo wa sasa wa mishahara ya watumishi wa serikali na taasisi zake kulipwa moja kwa moja kutoka Hazina. Serikali imetumia mwanya huo kuwasilisha mishahara tu, huku ikiendelea kushikilia makato hayo yaliyotakiwa kupelekwa NHIF.

Hali hiyo imesababisha NHIF kusitisha huduma za kushughulikia jambo lolote kutoka kwa taasisi au Idara ya serikali inayodaiwa na mfuko huo, ikiwa ni pamoja na kutengeneza vitambulisho kwa wanachama wapya, kufanya uhakiki wa wanachama wa zamani na mbaya zaidi, NHIF ina mpango wa kusitisha huduma ya Bima ya Afya kwa wafanyakazi ambao taasisi au Idara zao zinadaiwa.

My take:

Kama wafanyakazi wametimiza wajibu wao wa kukatwa michango yao, kwa nini waadhibiwe hivyo kwa sababu za uzembe au za makusudi ya serikali? Serikali imefilisika kiasi hicho hadi kutumia hela zinazotakiwa kuwasilioshwa kama makato?

Kama serikali imekuwa ikiwakaripia waajiri kushindwa kuwasilisha makato ya wafanyakazi katika mifuko mbalimbali ya hifadhi za jamii, iweje leo yenyewe iache kuwasilisha makato ya Bima ya Afya mahali husika? Kwa nini kama ni ukata wa fedha, serikali isiwasilishe tu hiyo michango halafu iende kukopa NHIF kama inavyokopa PPF na NSSF?

ninaongea hapa kwa ushahidi kamili, kwani NHIF wameniambia serikali haijawasilisha makato ya taasisi yako, so siwezi kuprocess chchote!
 
May be.serikali nao waseme juu ya hili, ili tuweze kujaji
 
Kule PSPF Serikali ilichota fedha za kuendeshea shughuli zake kwa ahadi kwamba watazirejesha. Deni lililopo sasa kule linasoma Trilioni, sio bilioni tena. Fedha hizo zinalipwa na Serikali kidogo kidogo kila mwezi ingawa sijui watamaliza deni hilo au wanazidi kuliongeza tu.
 
Juzi MSD walisitisha huduma hospitalini, leo NHIF wanasitisha huduma kwa wagonjwa wa bima ya afya kisa serikali haiwasilishi makato, je hatma ya maisha ya wanannchi wa Tanzania tunaiweka wapi?
 
Sitashangaa maana TD amejifunza urubani huku akikwangua hazina bila huruma na kuruhusu wanaomwangalia kisogo kujichotea. 2005 alikuta hazina imenona, hadi kugawa pesa kupitia mamilioni ya TD, leo anaondoka hazina iko dhofu mithili ya mtoto mwenye unyafuzi!
 
Mfano wa taasisi hizo la serikali tafadhali
 
Sitashangaa maana TD amejifunza urubani huku akikwangua hazina bila huruma na kuruhusu wanaomwangalia kisogo kujichotea. 2005 alikuta hazina imenona, hadi kugawa pesa kupitia mamilioni ya TD, leo anaondoka hazina iko dhofu mithili ya mtoto mwenye unyafuzi!
TD ndiyo nani?
 
Juzi MSD walisitisha huduma hospitalini, leo NHIF wanasitisha huduma kwa wagonjwa wa bima ya afya kisa serikali haiwasilishi makato, je hatma ya maisha ya wanannchi wa Tanzania tunaiweka wapi?
Ushahid jamani, mbona mimi teacher lakini kama kawaida natibiwa kwa bima, tena jana nilikuwa Regency medical Center Sar es Salaam?
 
May be.serikali nao waseme juu ya hili, ili tuweze kujaji
Kweli kabisa kwa sababu bwana, JF hivi sasa tumepoteza mwelekeo kabisaa, utakuta tunashabikia uzushi tu , mtu kajisikia kumnanga kiongozi au taasisi fulani basi tunajikuta tunashobokea tu kabla hatujapata ukweli kuhusu jambo lenyewe
 
Katika hali ya kushangaza, serikali imeshindwa kuwasilisha makato ya mishahara ya wafanyakazi wa baadhi ya taasisi zake katika Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) kwa miezi mitatu. Hii inatokana na mfumo wa sasa wa mishahara ya watumishi wa serikali na taasisi zake kulipwa moja kwa moja kutoka Hazina. Serikali imetumia mwanya huo kuwasilisha mishahara tu, huku ikiendelea kushikilia makato hayo yaliyotakiwa kupelekwa NHIF.

Hali hiyo imesababisha NHIF kusitisha huduma za kushughulikia jambo lolote kutoka kwa taasisi au Idara ya serikali inayodaiwa na mfuko huo, ikiwa ni pamoja na kutengeneza vitambulisho kwa wanachama wapya, kufanya uhakiki wa wanachama wa zamani na mbaya zaidi, NHIF ina mpango wa kusitisha huduma ya Bima ya Afya kwa wafanyakazi ambao taasisi au Idara zao zinadaiwa.

My take:

Kama wafanyakazi wametimiza wajibu wao wa kukatwa michango yao, kwa nini waadhibiwe hivyo kwa sababu za uzembe au za makusudi ya serikali? Serikali imefilisika kiasi hicho hadi kutumia hela zinazotakiwa kuwasilioshwa kama makato?

Kama serikali imekuwa ikiwakaripia waajiri kushindwa kuwasilisha makato ya wafanyakazi katika mifuko mbalimbali ya hifadhi za jamii, iweje leo yenyewe iache kuwasilisha makato ya Bima ya Afya mahali husika? Kwa nini kama ni ukata wa fedha, serikali isiwasilishe tu hiyo michango halafu iende kukopa NHIF kama inavyokopa PPF na NSSF?

ninaongea hapa kwa ushahidi kamili, kwani NHIF wameniambia serikali haijawasilisha makato ya taasisi yako, so
siwezi kuprocess chchote!

Labda taasisi yako tu ndo haijalipa huo mchango, nipo hapa kwenye system na michango ya wanachama inasomeka kabisa ,acha uzushi please
 
Back
Top Bottom