Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 4,783
- 14,975
Tukio hilo limefanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Tunduma, Machi 20, 2025 ambapo mradi huo kutoka Chanzo cha Maji ya Mto Momba, uliopo Wilaya ya Momba, mkoani Songwe utagharimu shilingi bilioni 119.9 za Tanzania.
Akizungumza Chongolo amesema Mradi huo utahusisha ujenzi wa chanzo cha maji (Intake) chenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni 21.5, ujenzi wa Kituo cha kuchakata na kutibu maji chenye uwezo wa kuzalisha lita 20m kwa siku.
Pia soma: Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze
Ujenzi wa mtandao wa mabomba ya kusafirisha maji yenye kipenyo cha 100mm yenye urefu wa kilometa 96, ujenzi wa matenki ya maji yenye uwezo wa kuhifadhi ujazo wa lita 5m litakalojengwa katika Mtaa wa Uwanjani/Uhuru, Halmashauri ya Mji-Tunduma, tenki la lita 3m litakalojengwa katika Kijiji cha Ikana na tenki lenye ujazo wa lita 2m litakalojengwa katika Kijiji cha Nkangamo, Ununuzi wa pampu, Ujenzi wa Ofisi na Vitendeakazi vingine.
Akihutubia mamia ya wakazi wa Mkoa wa Songwe waliojitokeza kushuhudia tukio hilo katika Viwanja vya Uwanjani, mjini Tunduma, Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, aliwahakikishia wananchi hao kuwa Serikali itatoa fedha zote za kutekeleza mradi huo ambao ni ahadi ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kumtua mama ndoo kichwani.
Kwa upande wake, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, alimpongeza Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa kiasi hicho cha fedha takriban sh. bilioni 120, ambazo ni fedha za ndani, kwa ajili ya kuwaondolea adha ya maji wananchi wa Tunduma, Vwawa na Mlowo, watakaofikiwa na mradi huo.
Mradi huo unatarajia kuwanufaisha wakazi 219,309 katika miji hiyo ya Tunduma, Vwawa na Mlowo, ambapo ujenzi wake utachukua miezi 18 kukamilika na kuanza kutoa maji safi na salama.