figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,689
- 55,662
Wiki moja baada ya Serikali kutangaza kuchukua hatua za kupunguza riba za mabenki kwa wananchi kwa kuagiza akaunti za mashirika na taasisi zake katika mabenki ya kibiashara zifungwe na kuhamisha fedha zilizopo katika akaunti hizo kwenda Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Sasa imegonga mwamba.
Waziri wa Ofisi ya Rais, TAMISEMI, utumishi na Utawala bora, George Simbachawene amesema huo mpango wa kuhamisha akaunti za mashirika na taasisi za Serikali umetolewa kimakosa.
Hata waziri wa Fedha na Mipango ameshafanyia marekebisho swala hilo kwenye mapendekezo Ya mpango wa maendeleo wa Taifa wa mwaka 2016/17 uliouwasirisha Bungeni.
Agizo hilo lilitolewa na Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru hivi karibuni, akiwataka watendaji wakuu wote wa mashirika na taasisi hizo, kufuata maelekezo matano ya kufunga akaunti zao katika mabenki ya biashara na kuhamishia fedha hizo BoT.
Hatua hiyo iliungwa mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.Charles Kimei ambaye majuzi aliongea na vyombo vya habari na kusema "tunafikiri maamuzi hayo hayana athari zozote kwani nchi mbalimbali zimekuwa zikitumia mfumo huo ikiwemo Uganda, Rwanda na Kenya ila kwa kwetu unaonekana mgeni kutokana na kutotumika kwa muda mrefu" alisema.
Sasa nashangaa leo Serikali kuachana na mpango huo uliokuwa na manufaa kwa Nchi.