Mbepo yamba
JF-Expert Member
- Aug 5, 2012
- 1,262
- 1,773
Wana bodies,
Serikali mwezi December 2023 ilitangaza bei elekezi ya pembejeo zote ambapo bei hizo zilikuwa na ruzuku .
Wakulima wa zao la tumbaku walikuwa miongoni mwa wanufaika wa ruzuku hiyo na bei ingeshuka kwa kiwango cha kuridhisha
Hata hivyo ulipofika wakati wa kulipa mikopo ya pembejeo kwa msimu huo ulioisha, wakulima walikatwa bei ya pembejeo isiyokuwa na ruzuku ndani yake.
Hussein Bashe akajitokeza hadharani mwezi August akasema fedha zote walizokatwa wakulima serikali kupitia wizara yake itazilipa kwa mkulima mmoja mmoja, ila tuu aletewe 'pdf' ya majina, akaunti na idadi ya mifuko ya wakulima ili alipe kwa haraka.
Kukawa kimya.
Mwezi Oktoba tena, akarudia tena kuwa fedha ziko kwake ila bado hajalipa tuu anasubiri hayo majina ya wakulima na akaunti zao na idadi ya mifuko.
Mpaka sasa kuko kimya mwaka unaisha na hatujui kama amefikia wapi.
Swali langu kwake ni ikiwa ameamua kuwazuga wakulima na halipi hizo hela au namna gani.
Bashe, tafadhali sana.
Kuna watu wamepoteza nyumba zao na mashamba. Wameshindwa kusomesha watoto au kugharamia matibabu kwa sababu wewe umeishikilia hiyo 13.5 bilioni yao
Tafadhali sana, Lisa hiyo hela mapema hii ya kuchelewa ili isaidia maeneo mengi ya ustawi wa jamii