Serikali yarejesha asilimia 49 za UDA, Simon Group yalipa sh bilioni 5.8

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
SERIKALI imerejesha asilimia 49 ilizokuwa inazimiliki kwenye Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), ambazo baada ya shirika hilo kubinafsishwa kwa kampuni binafsi ya Simon Group kulizuka utata zilipo hisa hizo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene alimweleza Rais John Magufuli kuwa baada ya kuwa amewaagiza kufuatilia uuzwaji wa UDA, walifanya kazi hiyo kikamilifu na kufanikiwa kurejesha asilimia 49 za serikali.

“Tulifanya kazi chini ya uongozi wa Waziri Mkuu, tukafanikiwa kurejesha asilimia 49 ambazo kwa kweli zilikuwa hazijulikani ziliko, lakini hisa asilimia 51 za jiji hizi tayari tulibaini zilishauzwa kwa Kampuni ya Simon Group,” alisema Simbachawene.

Alisema walibaini pia kuwa baada ya kuuziana, baadaye walishitakiana wenyewe kwa wenyewe, hivyo wakafanikiwa kuhakikisha serikali inabaki na asilimia zake 49 kwenye UDA ambayo sasa inafahamika kama UDA RT, ambayo ndio wanaoendesha Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka.

Aliongeza kuwa baada ya kuuza hisa hizo, Halmashauri ya Jiji hatimaye ililipwa Sh bilioni 5.8 na mwekezaji huyo, lakini halmashauri ya jiji na manispaa, wanavutana juu ya matumizi ya fedha hizo.

“Wanabishana wengine wataka kila manispaa ipewe mgawo, wengine wanataka wajenge vituo vitatu ya mabasi ya mikoani, lakini hawajapata muafaka wanaendelea kubishana...haya ni majungu tu nimeamua kuyasema hapa, lakini wakishindwa tutaomba mheshimiwa Rais utoe maelekezo mengine juu ya namna ya kutumia fedha hizo,” alisema Simbachawene.

Aliongeza kuwa iwapo halmashauri ya jiji, itakubaliana na mawazo ya kujenga stendi tatu kwa ajili ya mabasi ya mikoani ya Kongowe, Mbezi na nyingine kwa ajili ya mabasi yanayotoka mikoa ya kaskazini ni wazi kuwa watakuwa wamebuni miradi mizuri yenye manufaa kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam.

Pia Simbachawene alisema DART wamekuja na mpango wa kujenga jengo lao, jambo ambalo yeye amewakatalia, kwa kuwa kufanya hivyo kuvunja fedha za mradi. Alisema amewakatalia kwa sababu serikali inahamia Dodoma na wao wanaweza kupata jengo moja kwa ajili ya kuendeshea shughuli zao.

Akizungumzia kuhusu hoja hiyo, Rais Magufuli ametoa siku tano kwa viongozi wa jiji hilo, wawe wameamua watazitumia fedha hizo kwa miradi gani.

“Nataka waje waniambie watazitumia fedha hizo kwa jambo lipi, wakishindwa sisi tutawasaidia kuwapangia. Ila nataka wasigawane, badala yake wazielekeze kwenye miradi yenye manufaa kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam,” alisema Rais Magufuli.

Akizungumzia Kampuni ya Simon Group, Rais Magufuli alisema kwamba alipanga kuitumbua kampuni hiyo, lakini bahati nzuri imelipa deni hilo.

Alisema deni hilo ndio ulikuwa mtego wake aliokuwa ameutega, kama ingeshindwa kulipa deni lake la ununuzi wa hisa za Jiji la Dar es Salaam. Alisema kwa kweli Simon Group wameonesha uwezo wa kuendesha mradi huo, na hivyo mpango wake wa kuitumbua ameufuta.

Chanzo: Habarileo.
 
Ahadi kuu ya UKAWA ilikuwa kuhakikisha asilimia 51 za UDA zilizochukuliwa na Simon Group zinarudishwa katika Jiji.

Saed Kubenea alituahidi hili suala la UDA atalipeleka Bungeni na Mahakamani kama tukimchagua kuwa Mbunge wa Ubungo.

Baada ya kumchagua Kubenea na kuichagua UKAWA kuongoza Jiji, suala la UDA hatukulisikia tena.

Baada ya Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Charles Mwita kugundua umuhimu wa kufanya kazi na serikali, ameacha kufuata mawazo ya Kubenea ambaye alisema hawawezi kushirikiana na Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Niliwahi kuandika kuhusu hili suala katika Thread hii;

Jiji la Dar es Saalaam na Ahadi Hewa za Madiwani na Wabunge wa Ukawa
 
Ukistaajabu ya Musa! ... nimeamini penye uzia penyeza rupia! , yaani hiyo asilimia 51 ya Jiji ndio imeuzwa kwa Simon Group kwa peanuts halafu Ngosha ameukubali. Pesa hiyo hata kununua tuu ile ardhi ya depot ya Kurasini hazitoshi achilia majengo, achilia assets nyingine za UDA! . Kabla ya kuuzwa kwa hizo hisa za Jiji, jee ilifanyika valuation kuitathmini thamani halisi ya UDA ndipo ikapatikana hiyo value ya 51% ?!.

Something fishy ila damu ni mzito kuliko maji au kwa vile jamaa ni home boy?!.

Paskali
 
Ama kweli damu ni nzito kuliko maji....Huyu Simon angekuwa anatoka kwenye ile Kanda mukulu anayoichukia na anatamani wakazi wake waishi kama mashetani hakika asingepona...ila kwa vile anatoka Kanda pendwa amezawadiwa UDA kwa bei ya kibaba cha Unga..
 
Kumbe inawezekana kurudisha kitu ambacho hujui kimeenda au kimepotelea wapi?

Kwani hujaona kama imewezekana mkuu...nashangaa kwa nn zile pesa zilizosombwa kwa sandarusi hazirudishwi wakati bado Tanesco inadaiwa na pesa walimzawadia kalasinga...mh lifanyie Kazi hili suala tafadhali.
 
Kampuni inauzwa, inabadilishwa jina, hisa hazionekani? Kweli mafisadi wanavipaji haswa! Ni jambo la heri kwakweli kwa hisa hizo hatimaye kurejshwa!
 
Kitu hawajui kilipo...kimerudije sasa...
Hapa naona kuna ule mchezo wa kupanga data chumbani alafu taarifa inatolewaa kuwa uchumi umekua...
Hapa naona kuna funika kombe mwana mshenzi apite
 
Inawezekana sijafanya vizuri somo la hesabu darasani Lakini huyu waziri naweza kumzidi mbali tu, yaani kwa hali ya sasa na thamani ya fedha yetu ujenge stand 3 kwa 5.8 b Tshs? Labda stand za daladala tena 2 tu, stand sio nyumba ya kuishi upate sqm 400, hapa sioni faida ya kuuza hizo hisa
 
Kila siku tunalia hatuna pesa.

Tukipata pesa, tunaanza kulumbana namna ya kuzitumia.

Huo mpango wa kila manispaa kupata mgao wake utakuwa aina ya wizi mwingine. Zitaishia kwenye kulipana posho au tendder za madiwani. Ni vyema wajenge vituo vya ma-bus
 
Hii ni vichekesho tu....ati hisa hazijulikani zipo wapi ? Hii kali ya mwaka . Hivi brella wanasajili kampuni bila ya wanahisa kujulikana.
Mradi huu viwanja na parking hizi ..mali za uda zikiwamo nyumba workshop ndio thamani yake ni 5billiin ?
Huu ni ufisadi mkubwa sana. Imeundwa simon group wakubwa wale kwa mgongo wa serikali.
Kwa nn huu mradi wote usimilikiwe na jiji? Mradi huu una involve ujenzi wa miundo mbinu kwa mkopo kwa serikali kwa zaid ya $ 350 million
Vipi tumpe mtu binafsi share hizi ?
Hapa inataka uchunguzi wa kina otherwise something is wrong
 
Ukistaajabu ya Musa! ... nimeamini penye uzia penyeza rupia! , yaani hiyo asilimia 51 ya Jiji ndio imeuzwa kwa Simon Group kwa peanuts halafu Ngosha ameukubali. Pesa hiyo hata kununua tuu ile ardhi ya depot ya Kurasini hazitoshi achilia majengo, achilia assets nyingine za UDA! . Kabla ya kuuzwa kwa hizo hisa za Jiji, jee ilifanyika valuation kuitathmini thamani halisi ya UDA ndipo ikapatikana hiyo value ya 51% ?!.

Something fishy ila damu ni mzito kuliko maji au kwa vile jamaa ni home boy?!.

Paskali

Ni aibu tupu haya mambo inatosha kusema hivyo!
 
SERIKALI imerejesha asilimia 49 ilizokuwa inazimiliki kwenye Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), ambazo baada ya shirika hilo kubinafsishwa kwa kampuni binafsi ya Simon Group kulizuka utata zilipo hisa hizo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene alimweleza Rais John Magufuli kuwa baada ya kuwa amewaagiza kufuatilia uuzwaji wa UDA, walifanya kazi hiyo kikamilifu na kufanikiwa kurejesha asilimia 49 za serikali.

“Tulifanya kazi chini ya uongozi wa Waziri Mkuu, tukafanikiwa kurejesha asilimia 49 ambazo kwa kweli zilikuwa hazijulikani ziliko, lakini hisa asilimia 51 za jiji hizi tayari tulibaini zilishauzwa kwa Kampuni ya Simon Group,” alisema Simbachawene.

Alisema walibaini pia kuwa baada ya kuuziana, baadaye walishitakiana wenyewe kwa wenyewe, hivyo wakafanikiwa kuhakikisha serikali inabaki na asilimia zake 49 kwenye UDA ambayo sasa inafahamika kama UDA RT, ambayo ndio wanaoendesha Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka.

Aliongeza kuwa baada ya kuuza hisa hizo, Halmashauri ya Jiji hatimaye ililipwa Sh bilioni 5.8 na mwekezaji huyo, lakini halmashauri ya jiji na manispaa, wanavutana juu ya matumizi ya fedha hizo.

“Wanabishana wengine wataka kila manispaa ipewe mgawo, wengine wanataka wajenge vituo vitatu ya mabasi ya mikoani, lakini hawajapata muafaka wanaendelea kubishana...haya ni majungu tu nimeamua kuyasema hapa, lakini wakishindwa tutaomba mheshimiwa Rais utoe maelekezo mengine juu ya namna ya kutumia fedha hizo,” alisema Simbachawene.

Aliongeza kuwa iwapo halmashauri ya jiji, itakubaliana na mawazo ya kujenga stendi tatu kwa ajili ya mabasi ya mikoani ya Kongowe, Mbezi na nyingine kwa ajili ya mabasi yanayotoka mikoa ya kaskazini ni wazi kuwa watakuwa wamebuni miradi mizuri yenye manufaa kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam.

Pia Simbachawene alisema DART wamekuja na mpango wa kujenga jengo lao, jambo ambalo yeye amewakatalia, kwa kuwa kufanya hivyo kuvunja fedha za mradi. Alisema amewakatalia kwa sababu serikali inahamia Dodoma na wao wanaweza kupata jengo moja kwa ajili ya kuendeshea shughuli zao.

Akizungumzia kuhusu hoja hiyo, Rais Magufuli ametoa siku tano kwa viongozi wa jiji hilo, wawe wameamua watazitumia fedha hizo kwa miradi gani.

“Nataka waje waniambie watazitumia fedha hizo kwa jambo lipi, wakishindwa sisi tutawasaidia kuwapangia. Ila nataka wasigawane, badala yake wazielekeze kwenye miradi yenye manufaa kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam,” alisema Rais Magufuli.

Akizungumzia Kampuni ya Simon Group, Rais Magufuli alisema kwamba alipanga kuitumbua kampuni hiyo, lakini bahati nzuri imelipa deni hilo.

Alisema deni hilo ndio ulikuwa mtego wake aliokuwa ameutega, kama ingeshindwa kulipa deni lake la ununuzi wa hisa za Jiji la Dar es Salaam. Alisema kwa kweli Simon Group wameonesha uwezo wa kuendesha mradi huo, na hivyo mpango wake wa kuitumbua ameufuta.

Chanzo: Habarileo.
Sasa hivi halmashauri zikijenga stand yoyote ile wajenge itakayo dumu na kuangalia mahitaji hata ya miaka 50 ijayo sio baada ya miaka 5 tu au 10 wanaanza kufikiria kuzitanua au kuzihamisha
Hatusajahau yaliyotokea kwenye zilizo kuwa stand za daladala za Mwenge na Ubungo (pale karibu na jengo la TANESCO)
Na stand nyingine ndo zimedoda kabisa kama stand ya Temeke ambayo daladala zimegoma kwenda badala yake zinaenda Tandika Sokoni
 
Ukistaajabu ya Musa! ... nimeamini penye uzia penyeza rupia! , yaani hiyo asilimia 51 ya Jiji ndio imeuzwa kwa Simon Group kwa peanuts halafu Ngosha ameukubali. Pesa hiyo hata kununua tuu ile ardhi ya depot ya Kurasini hazitoshi achilia majengo, achilia assets nyingine za UDA! . Kabla ya kuuzwa kwa hizo hisa za Jiji, jee ilifanyika valuation kuitathmini thamani halisi ya UDA ndipo ikapatikana hiyo value ya 51% ?!.

Something fishy ila damu ni mzito kuliko maji au kwa vile jamaa ni home boy?!.

Paskali
Paskali huu mradi nioja ya ufisadi mkubwa kuwahi kufanyika...ni mwisho wa wizi. mradi unahusu mkopo kutoka WB ya zaidi ya $ 350 MILLION. Ikuwa ni kujengs miundo mbinu na ununuzi wa mabasi.
inakuaje unampa mtu binafsi mradi huu ? Hiu mradi unatakiwa kumilikiwa na setikali kwa asilimia 100. Hii ni service area serikali iendeshe.
kama kuna faida irudi serikalini.
hii ni miradi ambayo watu binafsi wanafaidi ikiwamo ccm.
wananchi wao wataumia kukamuliwa na trafic ili kulipa deni la WB huku faida ya mradi ikiingia kwa wafisadi....
 
Ukistaajabu ya Musa! ... nimeamini penye uzia penyeza rupia! , yaani hiyo asilimia 51 ya Jiji ndio imeuzwa kwa Simon Group kwa peanuts halafu Ngosha ameukubali. Pesa hiyo hata kununua tuu ile ardhi ya depot ya Kurasini hazitoshi achilia majengo, achilia assets nyingine za UDA! . Kabla ya kuuzwa kwa hizo hisa za Jiji, jee ilifanyika valuation kuitathmini thamani halisi ya UDA ndipo ikapatikana hiyo value ya 51% ?!.

Something fishy ila damu ni mzito kuliko maji au kwa vile jamaa ni home boy?!.

Paskali
Yeye amekubali kuuza mali za matrilion za uda kwa bilion 5....lakini atawataka wakulima wauze debe ya mahindi kwa ngombe wa 3
 
Kwa nini hii taarifa ya uongozi wa jiji umepokea 5.8bn Meya haisemi, kila siku watu wanatoa nyongo huku kuhusu Uda kumbe wao wameshachukua chao. Yaani Mstahiki meya na wabunge wote wa UKAWA wamekubali hii evaluation ya 5.8bn na wakanyamaza kabisa, acheni kutoa matamko ya kijinga lilieni vitu vya muhimu kama hivi.
 
Kwani hujaona kama imewezekana mkuu...nashangaa kwa nn zile pesa zilizosombwa kwa sandarusi hazirudishwi wakati bado Tanesco inadaiwa na pesa walimzawadia kalasinga...mh lifanyie Kazi hili suala tafadhali.
Hizo haziwezi kurudi kwa vile zinajulikana zilipokwenda, zinazoweza kurudi ni zile zisizojulikana wapi zimeenda!
 
Back
Top Bottom