PRODA LTD
JF-Expert Member
- Oct 20, 2016
- 1,005
- 1,333
EU YAISAIDIA TANZANIA: Serikali yapokea msaada wa kibajeti wa Sh490 bilioni kutoka Umoja wa Ulaya zitakazotolewa kwa miaka 4 kuanzia 2017/2018.
======
Umoja wa ulaya kuipa Tanzania Shilingi billion 490 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Umoja wa ulaya umeingia mkataba na serikali ya Tanzania ya kuipatia misaada wa fedha za miradi ya maendeleo kiasi cha shilingi bilioni 490 kwa kipindi cha miaka minne baada ya kuridhishwa mipango wa serikali ya awamu ya tano.
Akizungumza baada kusaini makubaliano hayo, katibu mkuu wizara ya fedha na mipango bwana Dotto James amesema umoja huo utakuwa unatoan shilingi bilioni 120 kila mwaka wa fedha kuanzia mwaka huu wa fedha wa 2017/18,fedha ambazo zitaelekezwa katika miradi ya vipaumbele ikiwemo kilimo,viwanda na afya.
Mkuu wa ujumbe wa umoja wa ulaya nchini na nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki, Bwana Roeland van de Geer amesema licha kuwepo kwa changamoto mbalimbali umoja wa ulaya unahistoria ya muda mrefu na Tanzania, ambapo amesisitiza fedha hizo za msaada zilielekeze katika sekta za kimkakati ikiwemo kilimo na viwanda kwa lengo la kufikia azma ya Tanzania kuwa nchi ya viwanda ifikapo 2020.
Chanzo: ITV