Serikali yapiga marufuku wataalamu kutoka nje wanaokuja kufanya kazi ya kupima na Upangaji ardhi

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Serikali imepiga marufuku wataalamu kutoka nje ya nchi wanaokuja kufanya kazi za upimaji, upangaji na umilikishaji ardhi na kuagiza kuanzia sasa shughuli zote zitafanywa na kampuni za ndani ili kupunguza gharama kubwa zilizokuwa zikitumika katika shughuli hizo.

Kwa mujibu wa taarifa ya serikali inasema kwa sasa iko katika utekelezaji wa mpango wa kupima, kupanga na umilikishaji wa ardhi mpango amabo unatarajia kutekelezwa ndani ya miaka kumi huku ukitarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi tirioni 2.3.

Kauli hiyo ya serikali imekuja wakati wa uzinduzi wa bodi ya waalamu wa mipango miji na vijiji iliyoko chini ya uenyekiti wa Prof. Wilibad Kombe ambapo wamesisitizwa kuhakikisha wanatumia taaluma zao kumfanya kila mtanzania awe na umiliki wa ardhi tofauti na ilivyo hivi sasa.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi, mwenyekiti wa bodi iliyomaliza muda wake.

Pamoja na masuala mengine ameitaka bodi hiyo mpya kuhakikisha inashugulikia changamoto ya uhaba wa rasilimali watu.
 
yaani mpaka wageni waje kupima ardhi yetu sisi tufanye nini sasa
 
Kati ya vitu vya maana hili ni mojawapo, Ardhi university wanazalisha wataalamu wengi sana kila mwaka wa upimaji ardhi lakini walikua wanategemea ajira za serikalini. Kuwa na board yao inayojitegemea itaongeza wigo wa ajira mana sasa itakua rahisi mtu kusajiri kampuni na kufanya kazi as private company. Hongera Lukuvi under guidance of JPM hili ni bonge la karata mmecheza.
 
Serikali iliruhusuje hii fedheha kwa wataalamu na utaifa wetu? Kweli wau nchi ni wananchi
 
Jambo zuri.. mi nimeajiliwa na kampuni za nje kutengeneza systems za ardhi ila hapa bongo ndo ukiwaeleza utaalamu wako wanakuona upo chini zaidi ya wa nje .
 
Hizi ni siasa tu, sidhani kama kulikuwa na wataalamu wowote wa mipango miji kutoka nje. Nyumba zimebanana mipango mibovu, barabara karibu zote hazina vision zaidi ya kuforecast uchaguzi tu, mtu unaweza kutudanganya kuwa tulikuwa na wataalamu wa.nje kweli?, imagine bara bara kubwa tulizonazo ni njia nne, nazo ni mjini tu, fine mtasema hatukuwa na pesa, je tukipata tutajenga wapi hizo barabara watu wameshajenga mwisho wa siku tunaishia kulipa fidia tu. Haya dar tulishakosea kwenye mipango, mikoa mingine je kama mwanza, arusha, mbeya, kigoma hata mtwara, kuna plani, gani? kwa nini mtu ukiwa south africa, au ulaya miji ya zamani unakuta mji ulipangwa miaka 1900 huko na zaid. Acheni kutufanya watoto wadogo.
 
Binafsi sizani kama kuna tatizo lolote tukitumia expertise kutoka nje kwa sababu matatizo tunayokumbana nayo sasa wenzetu walishatatua from 1800's, wanaweza wakaja kama consultants na wakashirikiana na wataalamu wetu ambao natumai na wao watajifunza kitu.
 
Jambo zuri.. mi nimeajiliwa na kampuni za nje kutengeneza systems za ardhi ila hapa bongo ndo ukiwaeleza utaalamu wako wanakuona upo chini zaidi ya wa nje .

Kwani uongo, siku moja niliwahi kwenda Wizarani nikakutana na wahusika nikawambia hivi vifaa vyenu mnayvo peleka Nairobi au kuwaita wa Kenya kuja kuvifanyia matengenezo na calibration - kampuni yangu ina uwezo wa kuvishughulikia, jamaa kumwambia hivyo sura yake ilibadirika ghafla one could sense hataki kabisa kusikiliza ushauri huo - wamejamaa viburi na dhalau na visingizio kwa nini vinapelekwa nje!!!

Baada ya kujaribu kuelimishana nikaona anaingiza mkono kwenye drawer na kutoa sub assemblies za electronic equipment/instruments, akaniuliza unaona kitu hiki kwa mfano - unafikiri kinafanya kazi gani? Nikamwangalia - baadae nikamuliza kwa upole hivi ndugu unanionyesha power supply ya SERVERS kwani ndio unaona kitu cha maana sana kuliko ushauri wangu niliokupa - nakwambia attitude zao za ajabu sana.

Baada ya kuona anaendelea na ngonjera zake na lame excuses nikampa business card yangu - kaisomaa, ghafla lugha ikabadirika akawa mpole oh ndugu husijali ntajaribu kuzungumza na Director au Katibu mkuu kuhusu ushauri wako, utapewa feedback mradi umetuachia address yako na namba ya simu - wako kimya mpaka leo.

Ujio wa Mh. Lukuvi na Dk.Magufuli unaweza kubadirisha mambo mengi katika Wizara hii, wakiwa ondoa Miungu watu Wizarani wanao jali ulaji tu wa 10% na kuwatilia vikwazo Watanzania wenzao wenye ujuzi mkubwa wa kiufundi na teknolojia wasifanikiwe kuinua Uchumi wa Taifa hili basi hao hawatufai hata kidogo. Bravo Mzalendo Lukuvi, Bravo JPJM.
 
1465572536760.jpg
 
Back
Top Bottom