Ritz
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 49,681
- 39,013
Wanaukumbi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (TAMISEMI), Mhe. George Simbachawene, amepiga marufuku utolewaji wa leseni kiholela kwa wageni wanaojiita ni wawekezaji.
Simbachawene ametangaza uamuzi huo jana Jijini Dar es Salaam, wakati alipokutana na Wafanyabiashara katika mkutano wao mkuu wa jumuiya ya Wafanyabiashara nchini(JWT).
Waziri huyo wa TAMISEMI, ameongeza kuwa kuna baadhi ya wageni wanaodai kuwa ni wawekezaji lakini mitaji yao ni midogo na hairidhishi kuitwa wawekezaji kwa kuwa kuna watanzania wengine nchini wanamitaji kama hiyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya wa Wafanyabiashara nchini, Johnson Minja, amesema serikali itafute mfumo bora wa ukusanyaji wa mapato sio kutumia nguvu katika ukusanyaji wa mapato kutoka kwa wafanyabiashara hao.