Serikali yapiga marufuku matangazo ya tiba za asili na tiba mbadala

Radhia Sweety

JF-Expert Member
Aug 10, 2011
4,434
1,765
Taarifa kwa vyombo vya habari

Ndugu mwanahabari

Wizara ya afya kuanzia leo 24 Desemba 2015 imepiga marufuku matangazo yote yanayohusu tiba asili na tiba mbadala kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Kwa wale wenye vibali wanatakiwa kuviwasilisha vibali na matangazo yao kwenye Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala ili vifanyiwe mapitio.

Utoaji wa elimu ya afya kwa umme unaofanywa na watoa huduma za tiba asili na tiba mbadala kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii umepigwa marufuku hadi hapo utaratibu mwingine utakapotangazwa.

Watoa huduma za tiba asili na tiba mbadala nchini kote wanaagizwa wawasilishe kwenye Baraza nyaraka zote muhimu ndani ya wiki mbili kuanzia leo Desemba 2015. Baadhi ya nyaraka hizo ni zile zinazohusu kuuza dawa za asili na tiba mbadala, nyaraka za kumiliki mashine zinazotumika katika kufanya uchunguzi katika tiba asili na tiba mbadala

Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala linaagizwa katika kipindi cha siku 14 kuanzia leo 24 Desemba 2015, lipitie nyaraka zote zikapowasilishwa zinazohusu usajili wa watoa huduma, usajili wa vituo vyao, ikiwa ni pamoja na maduka ya dawa za asili na dawa za tiba mbadala, usajili wa dawa zote zinazotumika katika huduma hizo na usajili wa mashine zote zinazotumika katika huduma za tiba asili na tiba mbadala.

Taarifa hiyo imetolewa na Dismas Lyassa kwa niaba ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Hamis Kigwangala na kusainiwa na M.O John, Kaimu Katibu.
 
serikali imepiga marufuku watoaji wa tiba mbadala kujitangaza na kutangaza kazi zao kwenye media source efm
 
Taarifa kwa vyombo vya habari

Ndugu mwanahabari

Wizara ya afya kuanzia leo 24 Desemba 2015 imepiga marufuku matangazo yote yanayohusu tiba asili na tiba mbadala kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Kwa wale wenye vibali wanatakiwa kuviwasilisha vibali na matangazo yao kwenye Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala ili vifanyiwe mapitio.

Utoaji wa elimu ya afya kwa umme unaofanywa na watoa huduma za tiba asili na tiba mbadala kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii umepigwa marufuku hadi hapo utaratibu mwingine utakapotangazwa.

Watoa huduma za tiba asili na tiba mbadala nchini kote wanaagizwa wawasilishe kwenye Baraza nyaraka zote muhimu ndani ya wiki mbili kuanzia leo Desemba 2015. Baadhi ya nyaraka hizo ni zile zinazohusu kuuza dawa za asili na tiba mbadala, nyaraka za kumiliki mashine zinazotumika katika kufanya uchunguzi katika tiba asili na tiba mbadala

Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala linaagizwa katika kipindi cha siku 14 kuanzia leo 24 Desemba 2015, lipitie nyaraka zote zikapowasilishwa zinazohusu usajili wa watoa huduma, usajili wa vituo vyao, ikiwa ni pamoja na maduka ya dawa za asili na dawa za tiba mbadala, usajili wa dawa zote zinazotumika katika huduma hizo na usajili wa mashine zote zinazotumika katika huduma za tiba asili na tiba mbadala

Taarifa hiyo imetolewa na Dismas Lyassa kwa niaba ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Hamis Kigwangala na kusainiwa na M.O John, Kaimu Katibu.

hapo sijapaelewa MASHINE ZITUMIKAZO KTK TIBA ASILIA.
hapa panatatizo!
unakuta mganga wa kienyeji nae ana ultra sound,au ana mashine ya kutolea sumu mwilini wats shits is it?
IPO HAJA YA SEREKALI KUJIPANGA ZAIDI HASA JUU YA MIPAKA YA HIZI KAZI/
 
wanawanyima haki yao ya msingi.
kama mtu anakibali cha uganga wa asili kwa nini asiwe huru kujitangaza? .
 
Vipi kuhusu waganga wa jadi ambao kila kona ya jiji wameweka mabango yenye ujumbe na picha za kuvutia wateja?
 
Mkuu nashukuru kwa taarifa hii muhimu, hongera sana kwa Dr Kigwangala, serikali ya awamu hii inafanya kazi kwa weledi, sijawahi ona duniani kote ma mmbumbumbu wakijitangaza na kujitukuza kama wanavyofanya wanganga wa kienyeji hapa Tanzania, wote wanajificha kwenye mwavuli wa tiba mbadala and %&$t hivi tiba mbadala gani hujui anatomy na physiology ya mwanadamu?

Dawa moja inatibu kisukari, pressure, ukimwi, ulcers, sukari type 2, figo na nguvu za kiume.... where in hell is this even possible?

Pongezi sana Dr Kingwangala na wizara ya afya, kwa muda huu mfupi tunaweza sema kuwa nchi imepata viongozi
 
Naunga mkono hoja walijitangaza mpaka aliyesomea udaktari wakaonekana si kitu kwa madaktari hao feki, sasa kimya kimya
 
..... kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.[/QUOTE]

Kwaiyo wale wa mabarabarani na vituoni ruksa.
 
Mwaka kaleta balaa........ndio basi tena sasa........hakuna namna nyingine.........
 
Kuna kituo kimoja cha radio hapa Mbeya nahisi kitafungwa maana wenyewe matangazo yao ni ya waganga wa kienyeji tu!
 
Watu walikwisha poteza imani na tiba za hosp. Zetu wakapeleka kwa waganga wa kienyeji.. safi sana
 
Back
Top Bottom