Serikali yapiga Marufuku kuuza viwanja vya ukubwa wa 20 kwa 20

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,653
218,143
Waziri wa Ardhi , Mh Anjelina Mabula ametoa Marufuku hiyo alipotembelea Maonesho ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea Kwenye Barabara ya Kilwa Mjini Dar es Salaam.

Amesema sababu kubwa ya kuzuia uuzaji wa viwanja vya ukubwa huo ni kuharibu Mipango miji , kwa vile viwanja vinavyopimwa ni vidogo mno kiasi kinachosababisha mrundikano wa watu wengi kwenye eneo moja.

Amewaasa wenye makampuni ya kuuza viwanja wapunguze Tamaa inayowasukuma kuuza viwanja vidogo vidogo ili wapate faida kubwa.

Nakala : Kwa Wakazi wa Mbagala, Vikindu na Chamazi.
 
Waziri wa Ardhi , Mh Anjelina Mabula ametoa Marufuku hiyo alipotembelea Maonesho ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea Kwenye Barabara ya Kilwa Mjini Dar es Salaam .

Amesema sababu kubwa ya kuzuia uuzaji wa viwanja vya ukubwa huo ni kuharibu Mipango miji , kwa vile viwanja vinavyopimwa ni vidogo mno kiasi kinachosababisha mrundikano wa watu wengi kwenye eneo moja .

Amewaasa wenye makampuni ya kuuza viwanja wapunguze Tamaa inayowasukuma kuuza viwanja vidogo vidogo ili wapate faida kubwa .

Nakala : Kwa Wakazi wa Mbagala , Vikindu na Chamazi .
20x20 miguu?
 
Safi sana..watunge sharia kabisa..mana matamko bila sheria ni kujirisha upepo.

Hivyo viwanja ndio chanzo cha slums.

#MaendeleoHayanaChama
 
Uwanja wa Makao makuu ya Chadema Ufipa st ni 20 kwa 15 yaani sqm 300

Nchi ngumu sana hii
Wewe nawe!
Ukilala ukiamka Chadema..huna hoja nyingine??

Nje ya mada:
Ila na ninyi chadema ifike mahali muondokane na hii aibu. Chama kubwa kuendelea kupanga huko uswazi sio poa. Kama ni lazima kupanga basi iwe ofisi ya maana inayoendana na hadhi ya chama.
 
-Waziri ametoa katazo la kupima Viwanja vyenye ukubwa sq400,.
-Ameagiza vpimwe Viwanja vya kuanzia ukubwa gani?
- Waziri ametoa mwongozo gani au vigezo gani vya kupima Viwanja vya high density, medium density na low Density.
-Waziri anajua kuwa hata maeneo yalipimwa,kuna baadhi ya wananchi wanauza maeneo ya wazi na barabara za mitaa kinyume na Sheria na taratibu.

Ushauri
1). Waziri afanye operation ya kuhakikisha kuwa wananchi wote waliovamia na kujenga kwenye maeneo ya wazi na barabara wanaondoshwa mara moja,
2). Watumishi wa Ardhi na Mipango miji wasimamie Sheria na kanuni,Kuna watu wengi wamevamia open space na wanajenga kwenye barabara eneo la Taliani na Nyeburu Chanika, Serikali isipodhibiti hali hiyo mapema,italeta usumbufu hapo baaadae
3).wenyeviti wa Serikali za mitaa wasimamia matumizi mazuri ya Ardhi,kwa kukemea vitendo wananchi wao kuuza maeneo ya wazi na barabara katika maeneo yaliyopimwa.
4). Waziri mwenye dhamana ya Ardhi awasiliane na Waziri wa Tamisemi,kuunda kamati au team ya matumizi bora ya Ardhi iliyopimwa.
 
Hili swala litawezekana kama siasa ikiwekwa pembeni.
Tatizo ni kuwa wakianza, chadema watasema wananchi waachwe, wanaharakati nao watasema watu wanaonewa
 
Back
Top Bottom